Mdee, Gekul, Silinde, Nassari, Butiku, Bulaya, Katambi, ndio wamenifanya niamini kwamba siasa Tanzania ni kuchumia tumbo tu sio kuwatumikia wananchi

Kimbakuli

JF-Expert Member
Jul 11, 2013
405
427
Tuliwaona ni makamanda walioiva mno, waliokuwa tayari kufa kwa ajili ya kutetea, haki za binadamu, demokrasia, katiba na n.k

Lakini mmoja baada ya mwingine wakaanza kusaliti kambi ya mapambano. Wakathamini fedha na madaraka kuliko kuwatetea wananchi, Aisee!!

Halafu leo utakuja kuniambia kuna wanasiasa wanapigania katiba, haki, demokrasia na maslahi ya nchi, Ah wapii.. Sitakuelewa.

Wanasiasa wengi wa nchi masikini wapo kwa ajili ya kutetea matumbo yao tu.

Kazi iendelee.
 
Ndio ujifunze kuiamini taasisi usiwaamini watu, hao huja na kutoweka, lakini taasisi iliyoundwa kwa misingi ya sheria haiwezi kuondoka.

Alichonitenda Dkt. Slaa sitamsahau yule mzee, niliamuamini nikajua huyu ndie Chadema haswa, lakini alivyokuja kuchukuliwa na TISS wakaenda kumficha hotelini pale ndipo "nilizima fegi"
 
Wanasiasa ni kama wachezaji soka.

Akiwa team A utasikia "nafurahi sana kuwepo kwenye club hii ni club ya ndoto yangu, nitajitolea kwa uwezo wangu wote kuisaidia team hii kushinda vikombe"

Ghafla team B ikipanda dau anahama halafu interview unasikia

"team B ndio team bora kuliko zote duniani na ndio team ninayoipenda toka utotoni ndio team ya ndoyo yangu nitajitahidi kupambana tushinde makombe mengi kadiri tuwezavyo".

Team C ikija mambo ni yale yale.

Pesa inahamisha akili.
 
Soma ule kijana. Kalia hayo hayo tu ka chura ndani ya maji. Tunaendaga shule ili tupambanie matumbo yetu na familia zetu. Unataka mpaka mkeo apambaniwe na mwingine! Unatgemea nini kitatokea!

Pambana na hali yako, ipambanie 👨‍👩‍👧👨‍👩‍👦‍👦👨‍👩‍👦‍👦👨‍👩‍👦‍👦 familia yako! Hakunaga uzalendo siku hizi mjomba. Ukipata fursa itumie japo si udharim ili kulinda fursa uliyoipata!
Soma ule babu!
Soma uleeeeeeeee!

Hapo ndo utajua kwanini wazazi wako walikusisitiza "" Soma mwanangu""
 
Alikatishwa tamaa mahali....
Ukiona Yanga hawakutaki si unahamia simba tu maisha yaendelee
Ndio ujifunze kuiamini taasisi usiwaamini watu, hao huja na kutoweka, lakini taasisi iliyoundwa kwa misingi ya sheria haiwezi ondoka.

Alichonitenda Dkt. Slaa sitamsahau yule mzee, niliamuamini nikajua huyu ndie Chadema, lakini alivyokuja kuchukuliwa na TISS wakaenda kumficha hotelini pale ndio "nilizima fegi"
 
Kuna mwingine anaitwa Lijualikali, kapoteana vibaya. And bahati Mbaya sana kwao aliyekuwa anawabeba huko kafa, Mama hana Time nao. Moto wataopelekewa na akina Nape lazima akili iwarudi.
Ha ha ha ha Walikua wanaziba nafasi za wana na ile CCM mpya yao. Yaan Leo hii Bashiru ambae alikua CUF ndo wakumuamini na kumfanya katibu akat ata Chipukizi ajawai pitia
 
Unamuacha wapi mbowe ambae alihongwa na Lowassa akamtimua Slaa?

Wanasiasa wa upinzani nchi hii ni wachumia tumbo tu hawana msaada ama nia ya kutusaidia kuiondoa ccm.

Wanataka demokrasia huku wao vi wenyeviti wa maisha wa vyama vyao.
 
Mkuu, kwa kuweka orodha 'kiduchu' kwenye 'heading' ya mada yako huitendei haki hoja nzima!

Utaachaje kwenye orodha hiyo watu kama Slaa (Dr Mihogo)!

Wote, wachumia tumbo wanafahamika wasiosimamia lolote wanaloliamini maishani mwao. Si akina Lipumba, Kalamaganda, Popole na wengi wengine.

Hivi sasa katika wanasiyasa wanaojulikana na kuvuma, hivi kuna hata mmoja unayeweza kuamini kwamba unaweza ukamwamini kwa lolote?
 
Tuliwaona ni makamanda walioiva mno, waliokuwa tayari kufa kwa ajili ya kutetea, haki za binadamu, demokrasia, katiba na n.k

Lakini mmoja baada ya mwingine wakaanza kusaliti kambi ya mapambano. Wakathamini fedha na madaraka kuliko kuwatetea wananchi, Aisee!!

Halafu leo utakuja kuniambia kuna wanasiasa wanapigania katiba, haki, demokrasia na maslahi ya nchi, Ah wapii.. Sitakuelewa.

Wanasiasa wengi wa nchi masikini wapo kwa ajili ya kutetea matumbo yao tu.

Kazi iendelee.
Tunahitaji sera mbadala nje ya CCM, Chadema imejengwa kitaasisi zaidi na ndio maana wameondoka watu maarufu sana lakini bado imeendelea kuwa imara, chama kimepitia kwenye misukosuko mikali sana kuwahi kupitia chama chochote cha siasa lakini bado kimeendelea kuwa imara. So hata aondoke Mbowe bado Chadema itaendelea kuwepo.
 
Mkuu tema mate chini chama kipo ila sio imara kama zamani kimepoteza mvuto kwa kiasi kikubwa
 
Back
Top Bottom