Mdee awapa matumaini wakazi wa Babati

Wambugani

JF-Expert Member
Dec 8, 2007
1,757
276
Kama mlivyosikia bunge lililopita tumewasha moto bungeni juu ya ardhi na wabunge wa CCM wametuunga mkono, sasa tunasubiri bunge la mwezi wa nne, mwakani kisipoeleweka kaeni mkao wa kula kutwaa mashamba"alisema Mdee.
MBUNGE wa wa Jimbo la Kawe(Chadema), Halima Mdee,amewataka wakazi wa mkoa wa Manyara kujiandaa kutwaa ardhi na mashamba ya wawekezaji ambayo hayajaendelezwa kuanzia mwakani.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika uwanja wa michezo Babati, Mdee alisema haiwezekani ardhi yote yenye rutuba nchini kumilikishwa wageni wakati Watanzania wakitaabika.

Mdee ambaye ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alisema wawekezaji hao wamemilikishwa ardhi yenye rutuba kwa kulipa Sh 2000 tu kwa eka kwa mwaka, wakati wao wanatumia mashamba hayo hayo kuwakodishia Watanzania kwa Sh 100,000 kwa mwaka kwa eka.

"Kama mlivyosikia bunge lililopita tumewasha moto bungeni juu ya ardhi na wabunge wa CCM wametuunga mkono, sasa tunasubiri bunge la mwezi wa nne, mwakani kisipoeleweka kaeni mkao wa kula kutwaa mashamba"alisema Mdee.


Alisema tayari pia Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk Mary Nagu alitoa kauli bungeni ya wawekezaji kupewa mwaka mmoja kuendeleza mashamba la sivyo watapokonywa.


Mdee alisema Watanzania hawawezi kugeuzwa watumwa kwenye ardhi yao na sasa wamechoka ndio sababu CHADEMA, inataka taarifa ya bungeni juu ya ardhi yote iliyopo nchini, iliyotolewa kwa wawekezaji na iliyobaki
.

"Hapa Babati kuna ardhi zaidi ya hekari 250,000 inamilikiwa na wawekezaji Wazungu na Wahindi ambao hawaitumii ardhi yote badala yake wanakodisha kwa Watanzania"alisema Mdee.

Akizungumzia Halmashauri ya Babati, alieleza kusikitishwa na wakazi wa Babati kuwachagua madiwani wote wa CCM na mbunge wa CCM, ambao wameshindwa kuwatetea.

"Mbunge wenu kila siku yupo jimboni kwangu Mbezi Jijini Dar es Salaam, kwani ndiko anaishi muda mrefu, mlimuaacha Paulina Gekur sasa mnajuta"alisema Mdee.

Hata hivyo, alisema yaliyopita si ndwele wagange yajayo katika kuhakikisha wanachagua madiwani na wagombea wa Chadema katika chaguzi zijazo.

Awali Wabunge wa Viti Maalum , Paulina Gekul Rose Kamili na Cesilia Pareso, waliwataka wakazi wa Jimbo la Babati, kubadilika sasa na kutambua kuwa ukombozi wao upo Chadema.

Gekur alieleza kazi aliyofanya katika Halmashauri ya Babati, ikiwepo kuzuia ushuru holela wa machinjio, kuzuia wamachinga kuhamishwa bila utaratibu na kufichua ufisadi katika halmashauri.

"Ndugu zangu japo kuwa mimi nipo mmoja tu katika baraza la madiwani nadhani mnajua kazi kubwa ambayo nafanya kuwatetea"alisema Gekul.

Nao Pareso na Kamili walisema viongozi wa CCM wameshindwa kuwadhibiti watendaji wa serikali wasiwahujumu wananchi na suluhu ya maisha bora kwa wananchi ni kuchaguwa Chadema katika nafasi mbali mbali.
CHANZO: Gazeti la MWANANCHI
 
kamanda ukweli chadema ndo tegemeo jipya kwa wananchi syo hao mafisadi
 
Mdee na Gekul msisahau na Kata ya Nkaiti, wilayani Babati jinsi wafugaji wanavyonyanyaswa na Muhsin Abdallah almaaruf Sheni
 
Huyu MDEE amekuwa shujaa Babati??? Aache Uzushi ameshindwa kuwasaidia wapiga kura wake jimboni Kawe, leo anajifanya ni mtu makini ugenini. Huo ni unafiki wana MADALE amewapiga chenga hadi halali jimboni mwake anaogopa wapiga kura wake
 
kamanda ukweli chadema ndo tegemeo jipya kwa wananchi syo hao mafisadi

Hana lolote kawaacha kwenye mataa wana Madale leo anajifanya ana uchungu na watu wa Babati, arudi jimboni kwake ndipo tutamuona shujaa
 
Huyu MDEE amekuwa shujaa Babati??? Aache Uzushi ameshindwa kuwasaidia wapiga kura wake jimboni Kawe, leo anajifanya ni mtu makini ugenini. Huo ni unafiki wana MADALE amewapiga chenga hadi halali jimboni mwake anaogopa wapiga kura wake

nabii haheshimiwi nyumbani kwao.
 
Mdee ambaye ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alisema wawekezaji hao wamemilikishwa ardhi yenye rutuba kwa kulipa Sh 2000 tu kwa eka kwa mwaka, wakati wao wanatumia mashamba hayo hayo kuwakodishia Watanzania kwa Sh 100,000 kwa mwaka kwa eka.

I really admire this girl BUT, she is just like the rest, too much power at hand with little technical know how of their job. CHADEMA wangejaribu kuwaombea shule ungaibuni hawa wanasiasa vijana ili wakajifunze mambo ambayo wenzetu waliotutangulia kimaendeleo wameshayafanya kwa zaidi ya miaka 100 iliyopita ili tuachane na wanasiasa wanaotoa matamko au maamuzi ya kijinga-kijinga wanakapokuwa madarakani. Hawa pia ni rahisi sana kudanganwya na wageni.

Vyuo vyetu vinajitahidi lakini ni lazima tukubali kuwa vina mapungugu mengi na pia hakuna shule inayozidi uzoefu wa kujionea kwa macho yako binafsi yanayoongelewa au kuandikwa vitabuni.
 
Makamanda mwambieni Mdee watakaompigia kura ni watu wa Kawe; anahangaika sana kuzima moto wa jirani wakati kwake kunaungua!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Ukikosa matumaini ya kuchaguliwa tena ishu ni kuponda raha na kuzunguka nchi nzima
 
MAFILILI,

Acha hizo.Unamponda Mdee kwa kuwa unataka jimbo la Babati na unamuona mpinzani wako anachanja mbuga unajaribu kumchafua Mdee.

Piga kazi kaka acha hizo.Sheria za JF zingeruhusu tungekuanika mbaya.

Mdee na makamanda mlioko field endeleeni kupiga kazi tutakuja soon
 
Hivi hakuna sheria inayoruhusu Wabunge kubadilishana majimbo? I mean Mdee abadilishane jimbo na mbunge wa Babati? Just kidding
 
Mdee na Gekul msisahau na Kata ya Nkaiti, wilayani Babati jinsi wafugaji wanavyonyanyaswa na Muhsin Abdallah almaaruf Sheni

yaani mnanyanyaswa ndani ya nchi yenu mnakaa kimya mnaacha kulianzisha mnamsubiri Halima Mdee aje kuwasaidia acheni ukondoo piganieni haki yenu hata ijapobidi kufa mtaandikwa kwenye historia ya ukombozi wa taifa letu!
 
Kaza buti Dada yetu tunakukubali sana, achana na hawa watumwa wa shetani wanaokatisha tamaa!!

Uwezo wako ni mkubwa wa kujenga hoja na kuwapigania Watanzania, PIGA KAZI.
 
Back
Top Bottom