Mdee anena kuhusu viongozi wa CHADEMA kutohudhuria mazishi ya waliokufa kwenye ajali ya MV Nyerere

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amezungumzia mtazamo na maswali yanayoulizwa kuhusu kutoonekana kwa viongozi wa kitaifa wa Chadema, katika mazishi ya watu waliofariki kutokana na ajali ya kivuko cha MV Nyerere mkoani Mwanza.

Mdee ambaye alikuwa miongoni mwa viongozi wa chama hicho waliohudhuria uzinduzi wa Sera za chama hicho wiki hii jijini Dar es Salaam, alikanusha taarifa za kutohudhuria kwa viongozi wa kitaifa wa chama hicho kwenye mazishi hayo akieleza kuwa huenda tafsiri ya viongozi hao ndio tatizo.

“Inategemea tafsri yako ya kiongozi wa kitaifa. Kwa mfano, sisi Chadema tuna ngazi ya Kitaifa kwa mantiki kwamba uongozi wa Taifa ambapo kuna Mwenyekiti wa Taifa. Lakini pia tuna viongozi wa kanda, hao viongozi wa kanda ni wajumbe wa Kamati Kuu, maana yake ni viongozi wa kitaifa,” Mdee aliiambia Dar24.

“Sisi Chadema tuna wabunge ambao nao ni viongozi wa kitaifa. Kwenye ule msiba walihudhuria viongozi wa Kanda ambao ni wajumbe wa Kamati Kuu, alihudhuria mbunge. Sasa kama mnatoa tafsiri ya kuhudhuria msiba kwa mtu aliyepewa nafasi ya kuzungumza pale kwenye TV live, sasa hicho ni kitu kingine,” aliongeza.

Thubutu! Angekanyaga kwenye jimbo lisilo lake angeishia mahabusu.
 
hqdefault.jpg

hapa nawaona wabunge wa kamati kuu wala sio wa kanda wakishiriki kumpumzisha kipenzi chetu, hawa jamaa kwa maigizo ni balaa
 
Inasikitisha sana uelewa wa Halima Mdee umeshuka kuwafikia nyumbu wengine

Kwa maoni ya mdee Chadema kutuma wawakilishi sawa ,ila Magufuli kumtuma waziri mkuu siyo sawa.

Alafu nyie chadema ,Mbunge aliyefiwa na ndugu zake kwenye ajali ndiyo muwakilishi wa chama msibani?

Kwa nini hamkutuma mwakilishi wa kanda kwenye mazishi ya mbwa wa Nassari?
 
Amejibu vizuri sana, CCM wanafikiri kiongozi wa kitaifa aliyehudhuria msibani ni yule anayeongea kwenye TV kama chakubanga, hawajui kulikuwa na viongozi wengi wa Chadema wa kitaifa ambao hawakupewa nafasi ya kutoa pole.

afterall kwa akili za CCM wangehudhuria kina Mbowe wangeambiwa wanatafuta kiki za kisiasa kwenye msiba, akili za CCM tunazijua zinapoanzia na zinapogotea.
 
Amejibu vizuri sana CCM wanafikiri kiongozi wa kitaifa aliyehudhuria msibani ni yule aliyeongea kwenye TV kama chakubanga, hawajui kulikuwa na viongozi wengi wa Chadema wa kitaifa ambao hawakupewa nafasi ya kutoa pole.

afterall wangehudhuria kina Mbowe wameambiwa wanatafuta kiki za kisiasa kwenye msiba, akili za CCM tunazijua zinapoanzia na napoishia.
Very weak defence !
 
Kwenye ule msiba walihudhuria viongozi wa Kanda ambao ni wajumbe wa Kamati Kuu, alihudhuria mbunge. Sasa kama mnatoa tafsiri ya kuhudhuria msiba kwa mtu aliyepewa nafasi ya kuzungumza pale kwenye TV live, sasa hicho ni kitu kingine,” aliongeza.
Viongzi wa kanda ya ziwa na mbunge wao ndio wafiwa waliofiwa na watu 226 hawakwenda pale kama wawakillishi wa chadema walikuwa pale kama wafiwa.Tunahoji chadema hawakutoa wawakilishi wa kwenda kuwafariji wafiwa uongozi wa kanda ya ziwa ,mbunge na wapiga kura wao waliofiwa.Yaani wafiwa ndio Halima Mdee anaita wawakilishi wa chadema msibani aiseeeeeee.Kweli akutukanaye hakuchagulii tusi
 
Hoja zenu zimepwaya sana ,uongozi wa kanda ulikuwepo na aliyefiwa alikuwa Mbunge wa Ukerewe siyo kanda nzima. Tafuta upupu mwingine. Au kaa kmyaa.
 
Yaani Mbunge mfiwa, ambaye pia alikuwa na ndugu zake wameondoka na hayo maafa ndio mwakilishi ? Wameshindwa hata kwenda kumfariji tu Mbunge mwenzao ? Miongoni mwa waliofariki pia viongozi kadhaa wa vijiji wa CDM. Mdee atakuwa alikuwa amevuta bangi zake kabla ya kuropoka kwa mwandishi.
Viongzi wa kanda ya ziwa na mbunge wao ndio wafiwa waliofiwa na watu 226 hawakwenda pale kama wawakillishi wa chadema walikuwa pale kama wafiwa.Tunahoji chadema hawakutoa wawakilishi wa kwenda kuwafariji wafiwa uongozi wa kanda ya ziwa ,mbunge na wapiga kura wao waliofiwa.Yaani wafiwa ndio Halima Mdee anaita wawakilishi wa chadema msibani aiseeeeeee.Kweli akutukanaye hakuchagulii tusi
Si afadhali hao hawakuhudhuria tu kuna wengine siku hiyo walifanya sherehe.
FB_IMG_1537947534216.jpg

But let me tell you my brothers and sisters, alipokuwa anatupeleka Magufuli huku mkishangilia karibu tutafika, ule ubaguzi wa wazi wa kiitikadi aliokuwa anauhubiri majukwaani eti sintopeleka maendeleo kwa watu waliochagua upinzani matokeo yake ndiyo haya, kwa hiyo msianze kulialia eti Chadema hawajafikia. Hii ni trela tu picha halisi inakuja.

Zanzibar ilianza hivi hivi enzi za komando ikafikia watu hawazikani, wanaswali misikiti tofauti na visima tofauti.

Leo tumeanza kutozikana kiitikadi kesho itakuwa kikabila mwisho tutahitimisha kidini, na mimi nafurahi kwa sababu majibu yameanza kutoka mapema kabla hajamaliza kipindi chake, tuendelee kushangilia.
 
Amejibu vizuri sana, CCM wanafikiri kiongozi wa kitaifa aliyehudhuria msibani ni yule aliyeongea kwenye TV kama chakubanga, hawajui kulikuwa na viongozi wengi wa Chadema wa kitaifa ambao hawakupewa nafasi ya kutoa pole.

afterall kwa akili za CCM wangehudhuria kina Mbowe wangeambiwa wanatafuta kiki za kisiasa kwenye msiba, akili za CCM tunazijua zinapoanzia na zinapogotea.
Bora ata ungekaa kimnya ...
 
Back
Top Bottom