beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Sakata la watumishi waliofukuzwa kazi kwa vyeti feki limetinga bungeni baada ya mbunge wa viti maalumu Halima Mdee kuhoji nini mstakabadhi wa malipo ya mafao yao.
Mdee amehoji hilo leo Jumatatu Juni 7 2021 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka wa fedha 2021/22.
“Ni dhuluma kwenye kichaka cha kusafisha. Hatukuwa na mfumo wa tracking, watu walichukua vyeti vya watu wengine na kusoma wana mpaka madigrii. Mnadhani is it fair (ni haki ) kutowalipa,”amesema.
Amemtaka Waziri wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba kueleza mstabadhi wa watumishi hao.
Mdee amesema Serikali inajificha katika kichaka cha kufanya uhakiki wa madeni, jambo linalowaumiza makandarasi na wadai nchini na kuongeza deni kwa Serikali.
Amesema kwa mujibu wa sheria inapopita siku 90 baada ya uhakiki kufanyanyika Serikali inatakiwa kulipa na riba, lakini hilo halifanyiki.
Mdee amesema anaungana na Kamati ya Bajeti kuitaka Serikali kuweka ukomo wa muda wa kuhakiki madeni wanayodaiwa ili makandarasi na wadeni wengine waweze kulipwa.
Pia, ametaka Dk Mwigulu kulieleza Bunge ni lini Serikali itapeleka michango ya watumishi katika mifuko ya hifadhi ya jamii.
Chanzo: Mwananchi