Mdee ahoji watumishi waliofukuzwa kwa vyeti feki kutolipwa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Sakata la watumishi waliofukuzwa kazi kwa vyeti feki limetinga bungeni baada ya mbunge wa viti maalumu Halima Mdee kuhoji nini mstakabadhi wa malipo ya mafao yao.

Mdee amehoji hilo leo Jumatatu Juni 7 2021 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka wa fedha 2021/22.

“Ni dhuluma kwenye kichaka cha kusafisha. Hatukuwa na mfumo wa tracking, watu walichukua vyeti vya watu wengine na kusoma wana mpaka madigrii. Mnadhani is it fair (ni haki ) kutowalipa,”amesema.

Amemtaka Waziri wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba kueleza mstabadhi wa watumishi hao.

Mdee amesema Serikali inajificha katika kichaka cha kufanya uhakiki wa madeni, jambo linalowaumiza makandarasi na wadai nchini na kuongeza deni kwa Serikali.

Amesema kwa mujibu wa sheria inapopita siku 90 baada ya uhakiki kufanyanyika Serikali inatakiwa kulipa na riba, lakini hilo halifanyiki.

Mdee amesema anaungana na Kamati ya Bajeti kuitaka Serikali kuweka ukomo wa muda wa kuhakiki madeni wanayodaiwa ili makandarasi na wadeni wengine waweze kulipwa.

Pia, ametaka Dk Mwigulu kulieleza Bunge ni lini Serikali itapeleka michango ya watumishi katika mifuko ya hifadhi ya jamii.

Chanzo: Mwananchi
 
Mbona hili jambo lina miaka likuki au ndio Fukua fukua za yule aliyetangulia?
Waziri leta majibu kwani nawewe ulikuwa mtetezi saana wa yulee!
 
Ni kweli kuna wengi sana zamani wwmetumia majina ya watu wengine wakasoma.

Wakati wa uhakiki hawakuwa na vyeti vya kidato cha nne.

Mfano ninamfahamu mtu aliyekwenda kusoma akitokea kwenye ajira kama mhudumu wa afya masomo ya afya kwa kutumia cheti cha ndugu yake,na alipokuja kazini,aliendelea kutumia jina lake lililofanana kidogo na lake.Wakati wa uhakiki alifukuzwa kazi na amesoma miaka mitano chuo cha afya na akafaulu.

Hakika ilikuwa dhuluma sana na double standard ya kufuru.Kwani kuna wengi wapo huko serikalini wana madaraka hawakuguswa.Tunawajua.
 
Hii kitu alianza kuiongea Mrisho Gambo, Leo tena Halima Mdee. TUCTA wao wapo kimya. Nafasi za hawa watu hadi leo hawajaajiriwa wengine. Kuna umuhimu kweli wapewe stahiki zao ili waajiriwe wengine kuziba nafasi zao.
 
Pale mtu feki anapoulizia watu feki!

Haya yanawezekana Tz pekee
 
MBUNGE FEKI ANACHANGIA FEKI.
WATUNGA SHERIA WANAPIGA MAKOFI

HAKUNA MUONGOZO WALA UTARATIBU
HALIMA HATA UCHANGIE POINT GANI NI UCHAFU ULIOJITAKIA
 
Kwamba mtu anacheti feki akaajiriwa kwa cheti feki halafu alipwe fedha kwa ufeki. Kwanini asiwashauri waende kufungua kesi Ili wapate haki Yao kamili kabisa.
 
Back
Top Bottom