Mdau Anataka Kuanzisha TV - Iwe na Vipindi Gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mdau Anataka Kuanzisha TV - Iwe na Vipindi Gani?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Allien, Jun 6, 2009.

 1. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2009
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Wana JF,

  Kuna mdau anataka ku-invest katika TV Station DSM na sasa anaandaa Mchanganuo kwa ajili hiyo ili kuufikisha katika vyombo husika by January 2010.

  Anapenda TV atakayoianzisha iwe na mambo yafuatayo:

  • Iwe na vipindi vya kuvutia sana kiasi kwamba kila anayefungulia asihamie channel nyingine.

  • Iwe inaelimisha katika mambo ya msingi ambao Watazamaji watajifunza na yatawasaidia.

  • Isaidie Kupiga Vita Ufisadi

  • Isaidie kubadilisha Attitude ya Watanzania katika kujiletea maendeleo

  • Isaidie katika kuondoa umasikini kupitia vipindi vyake

  • Isaidie katika suala zima la Ujasiliamali.

  • Pia Entertainment, Michezo, Vipindi vya watoto nk. nk.

  Inatakiwa zaidi ya 60% ya vipindi viwe local programs (Local Content) na chini ya 40% vinaweza kuwa vipindi vya nje (Foreign Content).

  Je ni nini mawazo yako juu ya vipindi mbalimbali na viendeshwe kwa staili gani ili kufanikisha malengo yake?
   
 2. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0

  Kuhusiana na hayo hapo juu kipindi kinaweza kuitwa YALIYOJIRI KUTOKA JAMIIFORUMS.

  Kipindi hiki chaweza kuwa cha nusu saa, kitarushwa siku za Jumatano na Ijumaa kuanzia saa tatu kamili usiku. Kipindi kitarudiwa kurushwa kwa muda wa saa nzima siku ya Jumapili kuanzia saa tatu usiku hadi saa nne usiku.

  Mtangazaji na mtayarishaji wa kipindi hicho naweza kuwa Uwiano Maalum, kama mdau mwenye TV atanitaka.

  Asante.
   
 3. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kama tutapata habari kutoka maeneo ambayo hayasikiki au hayafikiwi na vyombo vyengine...yaani vijijini uko, na mambo mengine ya taaluma na burudani kidogo tu.
   
 4. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2009
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145

  Mkuu;

  Unataka jamaa yangu afungiwe? Mzee wa Uchagani tu na porojo kidogo, anawakosesha usingizi. Ukileta yaliyojili kutoka JF si ndo watakufungia. ama?

  Hata hivyo wazo ni zuri. lakini je Wazungumzaji katika kipindi hicho watakuwa wa namna gani? Wanaweza Ku-Dare To Talk Openly?
   
 5. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2009
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Mkuu Junius;

  Sasa hivi bila shaka kuna vipindi kama hivyo katika TV zetu. Je unazungumzia viwe katika mfumo huo huo au mfumo gani? Au kuna ubunifu zaidi unatakiwa?
   
 6. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kama mdau ataogopa, ataniuzia muda then kama kushtakiwa nitashtakiwa mwenye kipindi. Hiyo TV iwe tofauti na ITV, Star TV au TBC. Hawa wako biased kiasi fulani hivi. Hiyo mpya iweze kupresent issues kwa uwazi, zinazolenga maendeleo ya wananchi kwa ujumla, elimu ya uraia na demokrasia kwa ujumla. Nyimbo zile zile za kuogopa kufungiwa zinasababisha kutomkomboa mwananchi wa tabaka la chini, kifikra.

  Yaliyomo kwenye kipindi hicho yatakusanya mawazo ya members hapa na kuyachambua kwa mtitiriko maalum. Ikibidi kutakuwa na mgeni maalum ambaye yuko responsible na suala husika litakalozungumziwa .ie waziri Masha na tuhuma za kufoji umri, Masha ataalikwa na kuweka ukweli, Mengi na kuoa...Mengi ataalikwa na kuweka ukweli, Michuzi kutumia safari za kikazi kwenda vekesheni, ataalikwa kuelezea jamii, Zitto na Dowans, naye ataalikwa kuelezea msimamo wake, umuhimu wa kujiandikisha na kupiga kura, m/wahusika wahamasishaji wataalikwa e.t.c, e.tc...
   
 7. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #7
  Jun 6, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Unaongelea freddy macha wa uk ? Yeye ndio anatafuta maoni ya watu au sio huyo unayeongelea njia rahisi ni kwenda katika kampuni za utafiti kama steadman , consumerinsight au research international wale wanadata nyingi sana
   
 8. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #8
  Jun 6, 2009
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145

  Mkuu Nakusoma Sana;

  Naona unataka kumkoma nyani nje ya JF sasa. Nadhani ni wazo zuri sana. wengi wanapowaalika hawa waheshimiwa au wahusika huwa wanauliza maswali nyoronyoro sana.

  Je, kuhusu vipindi vingine, ni yapi mapendekezo yako.
   
 9. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #9
  Jun 6, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Wazo zuri hili na tumpongeze mdau kwa kuthubutu hata kuwaza na kutekeleza wazo.
  Kwa kuanzia, mimi binafsi nitamshauri yafuatayo:
  1.Sipendi kuona jinsi redio na TV nyingi TZ wanavyoigana.Kuna wakati ungeshindwa kuelewa kama unasikiliza Radio 1 au redio TZ... Hii ilitokana na kule kuiba wafanyakazi kutoka tv/redio moja kwenda nyingine na kuwaruhusu kupeleka " uzoefu" wao wholesale.
  Ushauri - Mdau apeleleze TV zingine wana vipindi vya aina gani au mpangilio gani ili ajitofautishe ( differentiation)
  2.Mdau atengeneze niche yake kufuatia tathimini hiyo kwenye 1.hapo juu.
  Nitakuja na mawazo zaidi...
   
 10. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #10
  Jun 6, 2009
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145

  Shy; Asante sana Mkuu.

  Huyu Mdau si Fred Macha na wala sikuwa najua kama Fred Macha wa UK ana mpango wa kuanzisha TV.

  Wazo ulilotoa ni zuri sana. Je una details zozote za kampuni tajwa za utafiti na gharama zao?

  Pamoja na hilo, bado kama kuna mwana JF ana mawazo mazuri ya vipindi yanaweza kusaidia. Inakuwa kama ni utafiti mdogo pia.
   
 11. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #11
  Jun 6, 2009
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145

  WoS asante sana kwa mawazo bomba. Na hongera sana, naona unaendelea vema katika ile thread ya kumtafuta Superlady na Cerebrity wa JF.

  Ni kweli vipindi vingi sana vinajirudia rudia, hata style ya utangazaji pia. maoni yako yatafanyiwa kazi na mdau.

  Je, una specifiki choice ya vipindi ambavyo ungependa vibuniwe?
   
 12. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #12
  Jun 6, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ningependa kipindi cha kujenga viongozi wenye mtizamo wa kileo ( contemporary leadership) ambapo kutakuwa na mijadala moto moto kuibua vijana wenye uwezo wa kupembua mambo - kisiasa, kiuchumi, kijamii...
  Pia itakuwa ni fursa kuwatambua viongozi katika jamii - tuelewe viongozi siyo lazima watawala au wanasiasa - wanaweza kuwa watu wa kawaida kabisa waliofanya mambo ya kujivunia katika jamii zetu.Wanaweza kuwa wazee wa ukoo, wazee wa familia ambao hakuna mtu anawatambua kwa vile hawakuwahi kushika nyadhifa serikalini.Hii itakuwa fursa kuwaenzi na pia kuona ni kitu gani tunaweza kujifunza kusafisha uovu au uchafu unaochafua jamii zetu za sasa ( kupitia ufisadi/rushwa, uchu wa madaraka n.k.)
  Kipindi hiki kitaendelea kuwalea viongozi watarajiwa wake kwa waume... na TV inaweza kushirikiana na taasisi za mafunzo ili kuhakikisha kweli tunapata matunda na siyo porojo tu kama tulivyozoea waTZ.
  IN SHORT IM CRAVING FOR OUTPUT ORIENTED PROGRAMMES!
   
 13. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #13
  Jun 6, 2009
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145

  Mmmmmmmmmhhhhhhhh!!!

  Du, mama upewe hiki kipindi nini. You sound so much sure of the output.

  Utapenda kiendeshwe kwa mtindo gani na kiwe vipi hasa. Tell us more . . . It is interesting . . . .
   
 14. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #14
  Jun 6, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Mdau anaweza kunitafuta kwa mawazo ya kina LOL.
  On a serious note kuna namna nyingi ila mimi siyo mtaalamu wa kupanga vipindi vya TV ila maoni yangu ni kama hivi:
  guest speakers wenye kujadili mada na kuichambua,makala na majarida,nk.
   
 15. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #15
  Jun 6, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kila la kheri. Pengine tutaomba kibarua huko.
   
 16. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #16
  Jun 6, 2009
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145

  Mkuu, huna maoni yoyote mbali na kuomba kibarua?
   
 17. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #17
  Jun 6, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Allien..
  Asisahau vipindi vya michezo kubalance programme zake ukiacha vya habari, uchambuzi na nakala mbalimbali, vipindi vya elimu( sheria, biashara,uchumi) na tusiwasahau watoto katika jamii(hapa ni tatizo kubwa kwenye uendeshaji wake, ubunifu hamna). Na ajipange na watangazaji wenye ujuzi wa kufikisha ujumbe au kukiendesha kipindi vizuri siyo spoti ya channel ten.
  Anaweza kupata idea nyingi za vipindi lakini awe creative kuivuta hadhira kwa matukio katika jamii yetu. Pia aangalie na wenzake(competitors) wanafanya nini katika hiyo taaluma ili kupata mwangaza na kujua wapi pa kurekebisha au kuongeza nguvu kwenye vipindi atakavyoandaa kupitia hiyo tv channel mpya.
  Zaidi, atukumbuke wazawa kwenye hizo ajira yaani atafute watu wenye ujuzi wa hiyo taaluma kutoka nchini kwake.
   
 18. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #18
  Jun 6, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  fred macha ameshirikiana na mtu mmoja kuanzisha TV huko UK nimesahau jina lake ila kwa sasa anatafuta sana watafiti mbali mbali kuhusu vipindi na mambo mbali mbali kuhusu TV hiyo , ni ya uingereza lakini itakuwa inaonyesha mambo halisi ya kiafrika sio propaganda za magaribi

  Hao consumer insight wako Nkurumah kuna mtu anaitwa James ni mkenya ndio Director kwa tanzania nafikiri tovuti yao ni www.ciaafrica.com , Hao research international wako Viktoria Director wao anaitwa Vuri ila kuna manaja mwingine anaitwa Tupelike Subiri nichek kama naweza kupata no zako ntakupa Pm
   
 19. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #19
  Jun 6, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Bila kusahau mimi mwenyewe ninatarajia kuanzia mwaka huu mwishoni hivi kuanza vipindi maalumu kwenye tv mbali mbali vya kuelimisha jamii bado najiweka sawa nafikiri tutaonana na huyo mdau huko mbeleni
   
 20. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #20
  Jun 6, 2009
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Mkuu Belinda, asante sana mama.

  Kama ulivyoona kwenye bandiko kuu, nia ni kuwa na kitu tofauti na vilivyozoeleka. Kama utakuwa na ideas juu ya mpangilio wa vipindi na uendeshaji wake, nitaomba pia utoe mchango wake. Na nadhani hapa ndipo panapotaka ubunifu zaidi.
   
Loading...