Mdau aadhimisha miaka 50 ya uhuru wa tanzania kwa kuuza bidhaa za kitanzania kwenye magulio ya ulaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mdau aadhimisha miaka 50 ya uhuru wa tanzania kwa kuuza bidhaa za kitanzania kwenye magulio ya ulaya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shilingishop, Dec 15, 2011.

 1. S

  Shilingishop New Member

  #1
  Dec 15, 2011
  Joined: Dec 13, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  STORI ZA KWENYE BAO TUKINYWA KAHAWA NA KASHATA


  MDAU AADHIMISHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA KWA KUUZA BIDHAA ZA KITANZANIA KWENYE MAGULIO YA ULAYA


  Wengine wakiwa wanaadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania kwa sherehe, siasa nyingi, vigelegele, mivinyo na vinubi, mimi na mtoto wangu tulikuwa tanaadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa nchi yetu Tanzania kwa kuuza na kutangaza bidhaa za Kitanzania kwenye magulio ya wenzetu ulaya. Niliona kuliko kwenda Pub, au kusikiliza hotuba za kusadikika ni bora kwenda kuuza bidhaa za rafiki yangu "Fundinguo" kwenye masoko ya wenzetu kama wao wanavyouza bidhaa zao nchini mwetu. Wadau wenzangu, Kamwe Tanzania hatutaweza kuendelea kiuchumi au kijamii kama hatutajitahidi kuzalisha bidhaa zetu wenyewe kwa ajili ya matumizi yetu ya ndani na pia kwa ajili ya kuuza nchi za nje. Ni muhimu pia kujenga utamaduni wa kutumia vitu vilivyozalishwa na kutengenezwa nchini mwetu kwa jasho letu, mikono,akili, nguvu na rasirimali zetu zilizozagaa kwenye kila kona ya nchi yetu kuliko kutegemea bidhaa kutoka china. Kwa kufanya hivi ajira zitaongeza kwa vijana na watu wote, kipato kitaongezeka, uchumi wetu utakua na Tanzania itaendelea. Achana na maneno ya siasa , hii dhana ni halisi kwa maendeleo ya nchi wala haina chegachenga kama maneno meeeengi ya wanasiasa wanaotaka ubunge au Uraisi ili walipize visasi kwa maadui zao, wamiliki migodi, washibishe matumbo yao, walipe madeni yanayowakabili na kadhalika. Kuendelea bofya hapa http://shilingishop.blogspot.com

  Shilingi Shop,
  Idara ya stori za kwenye bao tukinywa kahawa na kashata.
   
Loading...