Jaguar
JF-Expert Member
- Mar 6, 2011
- 3,438
- 1,026
Mzee mmoja alikuwa anadaiwa madeni mengi yasiyolipika.Katika wote wanaomdai,kuna jamaa aliyemkopesha sh.5000
ndo alikuwa anamsumbua kila siku kumdai pesa yake.Siku moja alfajiri yule jamaa akamuibukia yule mzee huku akisema leo iwe isiwe lazima unilipe deni langu.Yule mzee akamwuliza yule kijana;kijana,hivi kati ya mtu mrefu na mtu mfupi nani huanza kudondokewa na matone ya mvua?.Kijana akajibu;mrefu.Mzee akasema;Hata katika ulipaji wa madeni ni hivyo hivyo,niache nimalize kuwalipa wale wanaonidai madeni makubwa kwanza,nikiwamaliza hao nitakufikiria na wewe.Yule kijana akatikisa kichwa na kuondoka moja kwa moja.