MDAHALO: Wahitimu wanaongezeka kuzidi nafasi za kazi, tutegemee kipi?

Singida ndio home

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
3,192
3,353
Kwa sasa hakuna mtu asiejua kwamba tatizo la ajira limekuwa kubwa mno, imefikia kipindi mpaka imekuwa mandatory mtu ujitolee bure kabisa bila kupata mshahara ili tu ujaribu bahati yako ya kuajiriwa kwa experience, Nafasi za kazi zinmekuwa chache sana huku wahitimu kila mwaka wakiwa wanarundikana kwenye kundi la jobless graduates

JE, HALI HII IKIENDELEA TUTEGEMEE YAPI?
 
ya misri kutokea, na nayaombea kweli. dharau zimezidi hakuna tofauti ya msomi na aliyekimbia umande.

usaili wanachukuana wenyewe, kama huna refa wafwaaaa. ya misri yaje tu
 
Kuna options kadhaa

✓Kujiajiri..Wahitimu watumie maarifa walioyapata vyuoni kujiajiri .Ukijiajiri kwenye fani yako itapendeza

✓Kuwa bora..Hapa mhitimu unakua bora kuliko wenzio kwenye eneo lako.Ukiwa shuleni usome vizuri lakini pia utafute sehemu za kujitolea kuongeza uzoefu na uwezo wa kuapply skills za shule in real practice
 
Mwaka 2007 Edward N. Lowassa aliwaambia serikali ya CCM kuwa Vijana wasomi wanaokosa ajira ni bomu linalosubiri kulipuka

Ila kwakuwa wanajifanya wanajua sana inaanza kula kwao
 
Kwa sasa hakuna mtu asiejua kwamba tatizo la ajira limekuwa kubwa mno, imefikia kipindi mpaka imekuwa mandatory mtu ujitolee bure kabisa bila kupata mshahara ili tu ujaribu bahati yako ya kuajiriwa kwa experience, Nafasi za kazi zinmekuwa chache sana huku wahitimu kila mwaka wakiwa wanarundikana kwenye kundi la jobless graduates

JE, HALI HII IKIENDELEA TUTEGEMEE YAPI?
Itabidi sehemu ya wahitimu ibadilike kuwa kazi ili kubalance mzani!
 
Kwa sasa hakuna mtu asiejua kwamba tatizo la ajira limekuwa kubwa mno, imefikia kipindi mpaka imekuwa mandatory mtu ujitolee bure kabisa bila kupata mshahara ili tu ujaribu bahati yako ya kuajiriwa kwa experience, Nafasi za kazi zinmekuwa chache sana huku wahitimu kila mwaka wakiwa wanarundikana kwenye kundi la jobless graduates

JE, HALI HII IKIENDELEA TUTEGEMEE YAPI?
Huhitaji kuwa Mtaalamu wa maroketi kujua kuwa kuna moja kati ya mawili yatatokea:
1. Serikali ikiweka sera nzuri watu watajiajiri na itakuwa baraka kwa nchi
2. Serikali ikiacha sera hizi mbovu ziendelee watu watakosa kazi na aidha ujambazi na utapeli vitaongezeka au kutakuwa na vurugu na nchi kuwaka moto!
 
Kwa sasa hakuna mtu asiejua kwamba tatizo la ajira limekuwa kubwa mno, imefikia kipindi mpaka imekuwa mandatory mtu ujitolee bure kabisa bila kupata mshahara ili tu ujaribu bahati yako ya kuajiriwa kwa experience, Nafasi za kazi zinmekuwa chache sana huku wahitimu kila mwaka wakiwa wanarundikana kwenye kundi la jobless graduates

JE, HALI HII IKIENDELEA TUTEGEMEE YAPI?
Tatizo la ajira lipo kila mahali duniani, muhimu mtu kujitambua kua ajira sio lazima uajiriwe na serikali, waweza kujiajiri, ushauri kwa serikali kurudisha elimu ya ufundi katika shule za msingi ili kuwapa maarifa na kujiamini watoto wetu tutapiga hatua tu.
 
tatizo la ajira lipo na ni tatizo la kimfumo ila ningeomba tu serikali wapanue investment ili sector binafsi pamoja na umma itasaidia kias kupunguza tatizo la ajira
 
Kwa sasa hakuna mtu asiejua kwamba tatizo la ajira limekuwa kubwa mno, imefikia kipindi mpaka imekuwa mandatory mtu ujitolee bure kabisa bila kupata mshahara ili tu ujaribu bahati yako ya kuajiriwa kwa experience, Nafasi za kazi zinmekuwa chache sana huku wahitimu kila mwaka wakiwa wanarundikana kwenye kundi la jobless graduates

JE, HALI HII IKIENDELEA TUTEGEMEE YAPI?
Ni ngumu kueleweka lkn inawezekana.
Tatizo kubwa la vijana wengi wa leo ni kuyaanza maisha kabla ya muda.Kijana akifika chuo tayari anaanza mahusiano ya kifamilia jambo linalowasumbua baada ya kumalliza masomo.Vijana wajue wanahitaji muda wa kusoma,muda wa kujiandaa na muda wa kuwa na familia.Vijana wa leo hawana saving.
Hebu tujiulize wale wanaokwenda kusoma nje na kujituma ,kujiwekea akiba na pia kuepukana na matumizi yasiyo ya lazima.Hiyo huwa kinyume na wale wanaosoma hapa nyumbani.

Lingine ni kutamani kazi za kuajiriwa.
Ni vyema sasa vijana wabadilike na kuwa wabunifu ktk kutafuta ajira.Ndio maana wenzetu hupenda kujiunga pamoja na kutengeneza taasisi au kikundi cha watu kutegemeana na taaluma wanazozichukua ili kujitolea ktk maeneo mbalimbali.Hii itawasaidia sana kutafuta uhitaji wa Taaluma zao,kujenga mtandao wa matumizi ya taaluma zao na kupata cv ya uzoefu.
Tujiepushe kama vijana kusubiri ajira ya serikali bali kujielekeza ktk ubunifu wa ajira na ni vyema kujua kuwa ni wakati gani ujiingize ktk maisha halisi.
Ushauri wangu ni waaache kuishi kwa maigizo wanapokuwa vyuoni.Maisha ni zaidi ya wanayoyaona.
 
Tatizo la ajira lipo kila mahali duniani, muhimu mtu kujitambua kua ajira sio lazima uajiriwe na serikali, waweza kujiajiri, ushauri kwa serikali kurudisha elimu ya ufundi katika shule za msingi ili kuwapa maarifa na kujiamini watoto wetu tutapiga hatua tu.
Umejiajiri kwenye sekta gani kwa hapa Bongo?

Lingine ni kutamani kazi za kuajiriwa.
Ni vyema sasa vijana wabadilike na kuwa wabunifu ktk kutafuta ajira.Ndio maana wenzetu hupenda kujiunga pamoja na kutengeneza taasisi au kikundi cha watu kutegemeana na taaluma wanazozichukua ili kujitolea ktk maeneo mbalimbali.Hii itawasaidia sana kutafuta uhitaji wa Taaluma zao,kujenga mtandao wa matumizi ya taaluma zao na kupata cv ya uzoefu.
Tujiepushe kama vijana kusubiri ajira ya serikali bali kujielekeza ktk ubunifu wa ajira na ni vyema kujua kuwa ni wakati gani ujiingize ktk maisha halisi.
Ushauri wangu ni waaache kuishi kwa maigizo wanapokuwa vyuoni.Maisha ni zaidi ya wanayoyaona.

Ushaijaribu japo kidogo hii nadharia yako kwa hapa Bongo? Unaweza kutushirikisha matokeo yake?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom