MDAHALO: Wahitimu wanaongezeka kuzidi nafasi za kazi, tutegemee kipi?

Umejiajiri kwenye sekta gani kwa hapa Bongo?



Ushaijaribu japo kidogo hii nadharia yako kwa hapa Bongo? Unaweza kutushirikisha matokeo yake?
Si kujaribu na wala sikufikia kuwa na digrii lkn naelekea kumiliki shule yangu ya Kiingereza kwa awali na msingi
IMG_20170917_145251.jpg

Tujifunze kufanya kazi kwa kujitoa na kuaminika.Maendeleo si tukio
 
Lazima ujitume ktk kila fursa itakayokujia.Heshimu na shirikisha watu ktk mawazo yako.
Nidhamu ndiyo msingi wa mafanikio
 
Nchi imefirisika ikiajiri italipa nini hao waajiriwa tutegemee mapinduzi hasa ya kisiasa kama misri na zimbabwe
 
Hiyo ni idea ya 2006.
Kumbuka jambo la msingi sana ktk kufanikiwa ni kusamehe.
Weka muda wako mwingi kufikiria utakavyofanikisha dhamira yako na si utakavyopambana na kuwalipiza wanaokukwamisha.
 
Mimi nadhani hali ikiendelea hivi basi ubunifu utakuwa mkubwa sana na tutegee vijana kubuni mawazo makubwa ya kibiashara na kutoboa. Lakni watakuwa ni wachache wale wenye akili pana . wale wenye mindset ya kuajiriwa wataendelea kulaumu huku muda ukiwatupa mkono na mwishowe wataweza kuingia katika vitendo hatarishi kama kula unga na wizi.
 
Mimi nadhani hali ikiendelea hivi basi ubunifu utakuwa mkubwa sana na tutegee vijana kubuni mawazo makubwa ya kibiashara na kutoboa. Lakni watakuwa ni wachache wale wenye akili pana . wale wenye mindset ya kuajiriwa wataendelea kulaumu huku muda ukiwatupa mkono na mwishowe wataweza kuingia katika vitendo hatarishi kama kula unga na wizi.
Natamani vyombo vya habari viache tabia za kuwafuata wanaowaita wasomi na wachambuzi.Ugonjwa wa vijana unaanzia hapo.Hata hao tunaowaita wasomi wakubwa wanaugonjwa huo.Angalia wengine wanaingia kwenye vyama,wengine wanahamahama vyama na wengine hawaoneshi njia bora za kuwajengea vijana kujiamini ktk kujitegemea.
Watu wa habari watafute watu waliofanikiwa ili kuwapa moyo na mawazo vijana wanaochipukia.Ni lazima vijana waandaliwe kuyapokea maisha yatakavyokuja na kuyatumia hayohayo kufanikiwa.
 
Lazima ujitume ktk kila fursa itakayokujia.Heshimu na shirikisha watu ktk mawazo yako.
Nidhamu ndiyo msingi wa mafanikio
Uko sasa hihi kabisa Mkuu tatizo letu wengi kuwa waoga na kuto jishughulisha tuache uvivu tupige kazi tutafanikiwa.
 
Kuna options kadhaa

✓Kujiajiri..Wahitimu watumie maarifa walioyapata vyuoni kujiajiri .Ukijiajiri kwenye fani yako itapendeza

✓Kuwa bora..Hapa mhitimu unakua bora kuliko wenzio kwenye eneo lako.Ukiwa shuleni usome vizuri lakini pia utafute sehemu za kujitolea kuongeza uzoefu na uwezo wa kuapply skills za shule in real practice
Hizi zinaitwa porojo za kupaka gari maputi ili ling'ae na kumbe halikunyooka vema.....

Hizi ni dalili za mawazo ya kukubali kuwa tumeshindwa kupambana na tatizo la ajira. Ajira tanzania ni tatizo kubwa sana ambalo linatakiwa kuongezwa katika list ya maadui qa taifa kama ujinga, magonjwa, njaa, na umasikini!

Mwanafunzi wa chuo kikuu hakusoma ili aje kujitolea bila malipo kwasababu alisoma ili aje kuuza muda na effort zake.....hayo maneno mngemwambia kipindi ana apply, sidhani hata kama angethubutu kujiunga na chuo.

Kwann tunafanya mizaa na watoto wa taifa letu. Kwann serikali hawakai chini kama familia na wadau wake kuhakikisha wanapambana na hili. Hivi hii tanzania mashirika ya serikali kama kumi yakianza kazi serious na yakatangaza ajira kadhaa na mkaisaidia sekta binafsi kusimama, hivi hamuoni baada ya miaka michache makampuni yataanza tafuta vijana wa kuajiri?!

Kwann tunaishi kisanii hivi?!
 
Tatizo la ajira lipo kila mahali duniani, muhimu mtu kujitambua kua ajira sio lazima uajiriwe na serikali, waweza kujiajiri, ushauri kwa serikali kurudisha elimu ya ufundi katika shule za msingi ili kuwapa maarifa na kujiamini watoto wetu tutapiga hatua tu.
We na wewe mitaji inatoka wapi?!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom