Mdahalo wa Wagombea Uraisi Zanzibar, isipokuwa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mdahalo wa Wagombea Uraisi Zanzibar, isipokuwa...

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ally Msangi, Sep 22, 2010.

 1. Ally Msangi

  Ally Msangi Verified User

  #1
  Sep 22, 2010
  Joined: Jun 29, 2010
  Messages: 576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  [​IMG]Habari iliyoripotiwa na Sadick Mtulya kutoka Zanzibar na kuchapishwa katika gazeti Mwananchi inasema kuwa, Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wananchi - Civic United Front (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad leo amelazimika kusitisha kampeni zake ili kushiriki mdahalo.

  Wagombea wa urais wote watashiriki isipokuwa yule wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk Ali Mohamed Shein ambapo kutokushiriki kwake kunatokana na uamuzi wa chama chake kuwakataza wagombea wake kushiriki katika midahalo na kwamba, midahalo yao ni katika mikutano ya hadhara ikiwa ni pamoja na kutangaza mafanikio ya ilani ya 2005/2010 pamoja na mipango na matarajio ya mwaka 2010/2015.

  Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Demokrasia Kibandamaiti, Kaimu Katibu mkuu wa CUF, Salim Bimani alisema mdahalo huo utafanyika katika ukumbi wa Bwawani, Unguja.

  "Kesho (leo) wanaCUF mnatakiwa mtulizane kimya majumbani ili muweze kumsikia na kumuona vizuri Maalim Seif atakapokuwa katika mdahalo utakofanyika Bwawani,'' alisema Bimani na kuongeza kuwa Maalim Seif ataulizwa na kujibu maswali papo kwa papo kutoka ukumbini hapo na kwa njia ya simu kutoka majumbani.

  Bimani ambaye pia ni mkurugenzi wa mawasiliano na uenezi, alisema mdahalo huo utaanza saa 4:00 asubuhi. "Kutokana na mdahalo huo, kampeni za Maalim Seif zitasimama kwa leo na zitaendelea kesho kutwa,'' alisema Bimani.
   
 2. C

  Chamkoroma Senior Member

  #2
  Sep 22, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chadema tumieni nafasi hii kama TBC1 watatoa kwa TZ bara, wakati huo utakuwa muafaka kwa wale ambao hawajamsikia Dr.Slaa waweze kumsikia na kumuuliza maswali, kama sisiem wakisusia pilau basi kula waambie wafanya kazi watakula pilau kila wili kwa balance watakazo pata baad ya mshahara kupanda.
  Lkn mawazo ya mtu mmoja katika chama hasa Mzee Makamba anadhani kuwakataza nikujificha namwambia wamekubamba ni bora ujitetee kuliko kuficha uso, sisiem kama mkilazimisha kingi mwaka huu, basi mjue makamba hawezi gombea akafurukuta mbele ya Dr. Slaa 2015.
   
Loading...