Mdahalo wa Wagombea Urais: CCM wakishiriki wataambulia aibu

koryo

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
639
276
Nawashauri wenzangu wa CCM wasije wakahudhuria mdahalo huu watakuja kupata AIBU ya mwaka. Wataulizwa maswali kuhusu SERA zao kuhusu Afya, Elimu, Maji, Utawala bora, rushwa na watashindwa kujibu kila kitakachoulizwa.

Mfano wataulizwa katika Sekta Afya sera yenu inasemaje?. Watajibu tutajenga zahanati kila kijiji, Kituo cha Afya kila kata, Hospitali ya kila Wilaya. Wataulizwa tena katika miaka 54 mlikuwa wapi?. KIMYA. Swali la pili, katika sera yenu kuhusu viwanda mnasemaje?.

Watajibu kuwa Tanzania itakuwa nchi ya viwanda. Wataulizwa tena, mbona mliviua? KIMYA. Swali la tatu wataulizwa kuwa Wizi wa fedha za umma mtachukua hatua gani?. Watajibu tutawashughulikia ipasavyo wezi wa mali ya umma. Watulizwa tena mbona hamjachukua hatua kwa wale waliokwapua fedha za escrow? KIMYA.

Juzi juzi kulikuwa na mdahalo kati ya vyama kwa kweli CCM ilipata aibu ya mwaka. Walimleta Ndugu moja Anayeitwa Cheyo ambaye aliwaletea aibu ya mwaka.

Mdahalo huo ulitawaliwa na majibu mazuri kutoka kwa Dr. Kessy kutoka Ukawa, Mwigamba kutoka ACT na mwingine wa UDP. Nawahakikishia kuwa katika mdahalo huu CCM mtapata aibu ya mwaka. Mjishauri sana kuhusu mdahalo huu.
 
Mtekelezaji mkuu alikuwa Lowassa pamoja na Mr Zero...watatueleza kwanini waliingiza nchi shimoni
 
Mtekelezaji mkuu alikuwa Lowassa pamoja na Mr Zero...watatueleza kwanini waliingiza nchi shimoni

Hilo jina Mr Zero unalitamka kwa kujifurahisha tu lakini hakuna Mtu anawachoma Sindano kama Sumaye na mnatamani Afe maana zile siku saba za mwisho wa kampeni ataanika Uozo wote kuhusu EPA,escrow, buzwagi, sukari, wizi pesa za ununuzi wa kivuko cha 1978 kwa billion 8, na zile billion 251 zilizoibiwa wizara ya Ujenzi kwa kulipwa kandarasi Hewa, mabehewa Feki, ATC ilivyofirisika, mikataba ya Gesi na uovu mwingine mwingi.
 
koryo

Mabehewa feki, kivuko cha 1978 kwa billion 8, mikataba ya Gesi, sukari, malipo hewa billion 251 wizara ya Ujenzi, chenji ya Rada, Chenji bunge la katiba, chenji ya katiba ya warioba billion 6, EPA, buzwagi, Mali na mabilion ya marehemu Gadafi ambazo ziliibiwa na kufichwa na membe kisha kugawana na wachache, uuzaji nyumba za serikali na madhambi mengineyo mengi.
 
Last edited by a moderator:
Nawashangaa UKAWA kwa nini hawataki kupiga hilo bao la wazi kabisa ! CCM hawawezi jibu swali lolote kwa sababu ndiyo wametufikisha hapo. Tuhuma zao za ufisadi ya Lowassa hazina mashiko na ni moja ya aibu yao kutuhumu bila kchukua hatua,
 
🚗🚲 ni mda wa viongozi kutumia usafiri wa nafuu kwenda maofisini na yale magari yote ya bei mbaya yapigwe minada.
 
Hilo jina Mr Zero unalitamka kwa kujifurahisha tu lakini hakuna Mtu anawachoma Sindano kama Sumaye na mnatamani Afe maana zile siku saba za mwisho wa kampeni ataanika Uozo wote kuhusu EPA,escrow, buzwagi, sukari, wizi pesa za ununuzi wa kivuko cha 1978 kwa billion 8, na zile billion 251 zilizoibiwa wizara ya Ujenzi kwa kulipwa kandarasi Hewa, mabehewa Feki, ATC ilivyofirisika, mikataba ya Gesi na uovu mwingine mwingi.

nchagga mangi sina MR ZERO Sumaye
 
Nawashangaa UKAWA kwa nini hawataki kupiga hilo bao la wazi kabisa ! CCM hawawezi jibu swali lolote kwa sababu ndiyo wametufikisha hapo. Tuhuma zao za ufisadi ya Lowassa hazina mashiko na ni moja ya aibu yao kutuhumu bila kchukua hatua,

Tatizo huwa ni waandaaji wa mdahalo kuleta maswali ya kumbeba mtu wao. Miaka yote ccm wamekuwa wakikimbia inashangaza mwaka huu wanajitia kimbelembele ingawa ni kimagumashi, Je kuna nini? Isijekuwa ni mwendelezo wa mabilioni waje kumchafua Lowassa na kufifisha speed ya mabadiliko.

Mdahalo na utafiti vyote tutavifanya wenyewe 25/10/2015
 
Back
Top Bottom