Mdahalo wa Muungano na Tanzania Tunayoitaka 'The Tanzania We Want'

Lukansola

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
5,437
1,597
Haya wana jamvi, tarehe 11 Septemba 2011 tena kuna mdahalo wa Muungano wetu na Tanzania Tunayoitaka. Hii ni jumapili tarehe 11 September kuanzia saa 11:00 mpaka saa moja usiku.

Wanaotaka kadi za kuhudhuria mdahalo huu wapige simu namba 0718 607403 (kwa wakazi wa Dar es Salaam) wazungumzaji wakuu wa mdahalo huu ni Mh Tundu Lissu, Juma Duni, Haji Waziri wa Afya Zanzibar na Mohammed Chomboh Mbunge wa Magomeni Zanzibar.

Mdahalo wa Muungano 11 Sept - - YouTube

Source: Star Tv
 
Mbona Zanzibar wawili,Tanganyika mmoja ,hawa waandaaji vipi bwana
 
.

hao wazanzibar wana wakilisha nchi yao, kwasababu tanganyika sio nchi watawakilishwa na mtu mmoja tu, no more Q's
 
Waandaaji wanaturusha,mbona bara hayupo ccm representer?i doubt the essence of this nomination.
 
nina amani kuwa watanganyika tutawakilishwa vema, namkubali lissu.
 
Zanzibar ina watu wachache kuliko mkoa mmoja wa Katavi inawakilishwa na watu wawili wakati Tanganyika inawakilishwa na watu wawili!! Au wameona Tundu Lissu anawatosha? Nasikia Prof. Chris Peter Maina naye atakuwepo kutoa changamoto za kisomi!! Sasa umeme uwepo ili wa mbali nasi tuambulie siyo nyinyi wa Dar. Manake uhakika wa kuufaidi mdahalo ni kwenda pale unapofanyika vinginevyo utakuwa na hamu ya kushuhudia kupitia Luninga mara Mr. Megawat anachukua megawat zake!!
 
<br />
<br />
Nakushauri uhudhurie maana mzee wa megawati lazima atavuta megawat zake!
 
Mbunge wa magomeni ni wa ccm kwa hiyo ccm wapo. Lkn hii ishu sio ya vyama nafikiri bali ya nchi mbili zanzibar na tanganyika so hao wajumbe ni vyema watete nchi zao kuliko vyama vyao.

Kama tundu lissu ni mwanasheria ingefaa na zanzibar engeitwa mwanasheria awadh wakaja wakapambana lkn hata hivyo babu juma ataweza vizuri tu.
 
Good hata kama kuna Mtanganyika mmoja bado wasemaji wote watatoa maoni ya vyama vyao.
Namkubali Duni haji huyo jamaa ni kichwa aliizimisha Zanz wakati wa Kitimoto cha Pascal Mayala hadi akafungwa jela na Kamandoo Salmin
 
sasa huu mdaharo unahusu muungano Tanzania au mtazamo wa nani anatoka wapi au vyama kuonyesha msimamo wa vyama juu ya muungano. tunaomba waandaaji watuweke waze naona watu wameanza kupotosha mantiki ya mdahalo
 
Tunataka vyama waonyeshe misimamo yao juu ya Muungano. Mfano CCM wanataka Muungano wa Serikali mbili, CUF Muungano wa Serikali tutu, Chadema wanataka Serikali za Majimbo nafikiri hizo ndio hoja tunazozitaka. kwani tumeona kwenye mdahalo uliopita Chadema walishindwa kupambanua Itikadi yao Marando alichemka kwa mujibu wa Itikadi yao
 
Mbona Zanzibar wawili,Tanganyika mmoja ,hawa waandaaji vipi bwana
<br />
<br />
Tanganyika m1?!! Kwa taarifa yako hata hivo Zanzb wameonewa maana kwa kumuweka Lissu hapo vilihitajika vichwa 6 vya wazenj kupambana nae. Kumuwekea Lisu hivo vijamaa vi2 naona wamemdharau.
 
Haya wana jamvi, tarehe 11 Septemba 2011 tena kuna mdahalo wa Muungano wetu na Tanzania Tunayoitaka. Hii ni jumapili tarehe 11 September kuanzia saa 11:00 mpaka saa moja usiku.

Wanaotaka kadi za kuhudhuria mdahalo huu wapige simu namba 0718 607403 (kwa wakazi wa Dar es Salaam) wazungumzaji wakuu wa mdahalo huu ni Mh Tundu Lissu, Juma Duni, Haji Waziri wa Afya Zanzibar na Mohammed Chomboh Mbunge wa Magomeni Zanzibar.

Mdahalo wa Muungano 11 Sept - - YouTube

Source: Star Tv

Hapo hapatatosha kabisa...............maana kichwa kimoja Tundu Lissu katika sheria ni vichwa 10,000 vya akina Werema na Kombani.......
 
Kwa Zanzibar wangemchukua yule mwandishi wa BBC wa zamani mzee Salim Said Salim. Niliona ana uchungu sana na uZANZ kwenye chaneli 10
 
Haya wana jamvi, tarehe 11 Septemba 2011 tena kuna mdahalo wa Muungano wetu na Tanzania Tunayoitaka. Hii ni jumapili tarehe 11 September kuanzia saa 11:00 mpaka saa moja usiku.

Wanaotaka kadi za kuhudhuria mdahalo huu wapige simu namba 0718 607403 (kwa wakazi wa Dar es Salaam) wazungumzaji wakuu wa mdahalo huu ni Mh Tundu Lissu, Juma Duni, Haji Waziri wa Afya Zanzibar na Mohammed Chomboh Mbunge wa Magomeni Zanzibar.

Mdahalo wa Muungano 11 Sept - - YouTube

Source: Star Tv
Mh.Tundu Lissu namwaminia....and i can guess through him mdaharo utakabiliwa na changamoto za hoja mzito.
 
Hapo hapatatosha kabisa...............maana kichwa kimoja Tundu Lissu katika sheria ni vichwa 10,000 vya akina Werema na Kombani.......
Wameogopa kuwaweka jamaa wengi wasishtukie wamebezwa,jua kula na vipofu bwanaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom