Mdahalo wa mauaji ya tarime mgodini kufanyika saut na kurushwa na star tv | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mdahalo wa mauaji ya tarime mgodini kufanyika saut na kurushwa na star tv

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fred Katulanda, Jun 9, 2011.

 1. Fred Katulanda

  Fred Katulanda Verified User

  #1
  Jun 9, 2011
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 229
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Shirika la Iritongo Conflicts resolution and Development Initiative Movement (ICORMID) kwa kushirikiana na Star Tv kupitia kipindi chake cha HOJA YANGU, limeandaa mdahalo utakaowahusisha wanazuoni Jijini Mwanza ambao ni wenyeji wa Tarime na wa maeneo meingine kwa lengo la kujadili na kutoa TAMKO juu ya Hali ya Amani na Migogoro baina ya mwekezaji (North Mara Gold Mine) na wazawa wa wilaya hiyo.
  Mdahalo huo utahusisha washiriki zaidi ya 200 na utafanyika katika Chuo cha Mt. Augustine (SAUT) Malimbe Jumamosi Juni 11, 2011 kuanzia majira ya saa 3:00 asubuhi, Ukumbi ni M-1.
  Hii ni kwa mujibu wa mkurugenzi wa shirika hilo Samwel Magoiga.
   
 2. l

  lebadudumizi Senior Member

  #2
  Jun 9, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Serekali na wawekezaji wanausika na mauaji mdahalo wa nini ?.
   
 3. Mosachaoghoko

  Mosachaoghoko Senior Member

  #3
  Jun 9, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huwezi kufanya mdahalo huku waathirika wakubwa hajajua kuwa ni kwanini serikali yao hajasema chochote kuhusu serikali kuiba miili ya marehemu na kuitupa barabarani
   
 4. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #4
  Jun 9, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Vijana mje na hoja za kueleweka, twategemea kupata mambo tokana na huo mdaharo!
   
 5. chipanga

  chipanga JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 661
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 60
  ninge klick pale kwenye thanx lkn ngoja nikupe THANKS halisi!
   
 6. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #6
  Jun 9, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ni muhimu ufanyike huo mdahalo na mawazo ya watu yasikike, maana serikali haiwezi toa tamko kwa sababu inahusika na mauaji hayo kwa njia moja au nyingine. Vijana wanazuoni tunategemea mje na hoja bzenye mashiko siku hiyo.
   
 7. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #7
  Jun 10, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Wewe hutaki midahalo ya kisomi unataka nini? Basi tulia great thinkers wakitoa maoni siku hiyo na wewe utaambulia la maana ili hata umwelezapo mjukuu wako kuhusu mauaji hayo ujenge hoja za kumwezesha kukuelewa, siyo jazba mbele kama tai, lete hoja mkuu!

  PATIENCE IS A VIRTUE
   
 8. j

  jakamoyo JF-Expert Member

  #8
  Jun 10, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Serikali haija chukua hatua muafaka juu ya tatizo la tarime.
  Haijachelewa ilifanyie kazi kwani ni kero kwa watanzania wote.
   
 9. m

  matawi JF-Expert Member

  #9
  Jun 10, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hivi wasira si ndo msemaji wa wauaji? May be akiona mdahalo atatoa tamko
   
 10. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #10
  Jun 10, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Serikali haiwezi kuongea cho chote, migodi yote ni kama Meremeta pinda alisema haishikiki. Budget mwaka huu na miaka yote haitagusa migodi. Kwenye migodi kote kuna maslahi ya wakubwa kila mwaka. Yanawekwa kwenye account zao za nje kwa majina ya makampuni feki. HII NDIYO SABABU wengine walifukiwa hai, serikali ilinyamaza, zaidi ya watu 70 wameuawa Nyamongo serikali haijasema kitu. ACHA WANA TARIME, WANAMAGEUZI ASILIA WAWEKE MAMBO HADHARANI. ILA nina wasiwasi, kama Startv hawatachakachua!
   
Loading...