Mdahalo WA JK: WANA CCM TUSAIDIENI KUULIZA MASWALI HAYA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mdahalo WA JK: WANA CCM TUSAIDIENI KUULIZA MASWALI HAYA

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mtaka Haki, Oct 28, 2010.

 1. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ninawaomba wana CCM mnaoweka maslahi ya nchi mbele ya Chama mumuulize Mpendwa wetu mgombea wa CCM maswali haya kwa niaba yangu na ya wanachi wengine ili akanushe uvumi unaoenezwa juu yake katika haya yafuatayo.

  Maswali ya muhimu.
  1. Wapinzani wako wamekuwa wakisema kuwa wewe sio makini na kwa sababu hiyo unaweza kujikuta umesaini jambo hatari kwa taifa. Je kuna ukweli juu ya matukio haya? Kama wewe ni makini na watendaji wako sio makini basi kwa matukio yafuatayo tunaomba utuambie ulichukua hatua gani kuonyesha umakini wako?

  a) Ulisaini sheria ya uchaguzi kwa mbwembwe bila ya kuisoma huku ikiwa imechakachuliwa.
  b) Ulipokea cheki yenye tarakimu tofauti na maneno kwa shukrani na kukubali kupigwa picha huku ukiionyesha.
  C.) Uliwahi kumwita mkurugenzi wa wilaya moja kuja kuchukua gari na alipofika ulikasirika na kushangaa anawezaje kuchukua gari la mkurugenzi mwingine?
  d) Ulishangilia kwa makofi riport iliyokuwa ikisomwa mbele yako kuwa shs Bilioni 3 zilitumika kwa matundu ya vyoo vya shule nne kwa matundu manne kila shule kwa gharama ya shs Milioni 700 kwa jumla ya shs Bilioni zaidi ya 3.
  e) Uliwainua mikono na kuwaita ni watu safi watuhumiwa wa ufisadi na wengine wakiwa wamefika hata segerea.
  f. Ulisaidiwa na serikali ya uingereza kugundua ubadhirifu na wizi wa mabilioni ya Rada na bado mtuhumiwa ndiye mwenyekiti wa kamati ya maadili ya CCM Taifa.

  2. Uliwaahidi waislamu katika ilani ya CCM ya mwaka 2005 kuwa ungewapatia mahakama ya kadhi. Je Kwa kuwa haiko kwenye ilani waislamu watarajie nini?
  3. Je ni nini msimamo wako wa Tanzania kujiunga OIC?

  NA YALE MTAKAYONIONGEZEA HAPA CHINI TUWAOMBE WANA CCM WENYE KUTANGULIZA MASLAHI YA TAIFA KULIKO YA CHAMA. OBAMA ALIKATAA KUMPIGIA KAMPENI MGOMBEA WA CHAMA CHAKE HUKO Rhode Island kwa kuwa haamini kama ni mfuasi mzuri wa siasa za chama chao.
   
 2. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naomba mniongezee maswali angalao mawili tuwaombe wazalendo watakaokwenda watuwakilishe.
   
 3. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  KAMENDE AMEPOST JUU YA KUHARIBU UCHAGUZI NAOMBA HILO LIWE PIA NI SWALI LA HAKI LA KUMUULIZA RAISI WETU MPENDWA. Kuna wana CCM wengi kama waliompa taarifa Kamende wanaoweza kutusaidia kumuuliza maswali haya kesho kuondoa utata.
   
 4. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2010
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  aliahidi nyumba za serikali zilizouzwa kipindi cha mkapa angezirudisha serikalini, hakufanya hivyo, alikwamishwa na nani.
   
 5. M

  Mutu JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  hana jeuri ya kujibu maswali hayo,
  tatizo hata wakimtengea maswali na majibu bado mkwere ni mkwere hamna kitu
   
 6. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nashukuru Jogi kwa hilo. Labda tuseme kama ulishindwa kurudisha nyumba ulizoahidi na ukashindwa kuwapa waislamu mahakama ya kadhi. Kama ahadi kidogo zilikushinda tutakuaminije kwa ahadi nyingi hivi? Wapinzani wako wanasema eti kwa kuwa ni kipindi chako cha mwisho je wewe unawahakikshiaje watanzania kuwa utatekelezaje? Je kuna Swali lingine la kukosa umakini?
   
 7. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Akili anazo kujibu hayo maswali? si mpaka aandikiwe naye asome tu kama Kasuku?
   
 8. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Watauliza live wale watakaoingia katika mdahalo. Utaenda?
   
 9. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Maswali zaidi? Au yanatosha. Natamani angalao moja kati ya haya yaulizwe na yajibiwe. Na kwa kuwa hupewa taarifa hata za hapa basi ajibu tu kwa kutoa humu humu JF.
   
 10. B

  Bull JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uwezi kumfananisha na Mchungaji Slaa, huyu ni mapepe kabisa

  Slaa hayuko makini kwa sababu:

  a - Kaacha mambo ya mungu akakimbilia siasa, nawakati huohuo kondoo wake wanazidi kupotea

  b - Kavamia na kuowa mwanamke wa mtu bila kufanya uchunguzi, hii ni hatari kwa mtu kama huyu kumpa madaraka angalau ya kijiji

  c - Alikuwa CCM, alipokosa ubunge kaamia chadema kwa ajili ya kujenga mtandao wa kanisa

  d - Kavunja sheria ya kikatoliki, kama yeye padiri haruhusiwi kuowa na pia kuacha, yeye mchungaji Slaa kavunja yote.

  e - Kakumbatia ukabila na udini ndani ya chama chake, kashindwa kabisa kuvunja mtandao wa cancer ndani ya chadema

  f - Hanakisomo na waliomzunguuka kama Mbowe nk. nchi hii haiendeshwi kwa kutumia elimu ya bibilia.

  g - na mengineyo

  Kumuachia Slaa nchi ni ku- commit suicide !!!!
   
 11. M

  Matata Member

  #11
  Oct 29, 2010
  Joined: Mar 28, 2006
  Messages: 23
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 5
  CCM wajanja wenye kuuliza maswali wameishapangwa. mdahalo huo ni geresha. Hapata kuwa na maswali magumu. Maswali yote yatakuwa ni ya kuonyesha kuwa ni mchapa kazi.
   
 12. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2010
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Kama angekuwa kule kwa Baba (USA) au kwa mama (UK) swali la kwanza lingekuwa mashimo manne ya vyoo alivyojenga wilayani kwake kwa TSH. Bilioni 3. Lapili aelezee kashfa zinazoikumba serikali yake, Latatu kwani hatamki kumaliza Rushwa kwenye Kampeni zake, La nne Je amejiandaaje (Kisaikolojia) kuondoka Ikulu Jumatatu. Latano je amefanikiwa kivipi kupeleka maisha bora kwa kila mtanzania katika miaka 5 ilopita kwa kasi na ari mpya, Je hizo ari na kasi mpya mbona hajazikampeni tena mwaka huu, au ndio ameishafanikiwa? Lasita, Je ameishatoa ahadi ngapi mpaka sasa hivi? akiweza kukumbuka then swali la nyongeza Je serikali yake (kama akichagulia) itahitaji fedha kiasi gani kukamilisha ahadi zake na itapata wapi pesa hizo? Lasaba kwanini kaiachia familia yake imkampenie badala ya kutumia wazee na viongozi wa chama? La nane anamchukilia vipi Dr. Slaa hasa ikizingatiwa kuwa Dr. Slaa anamlipua kwa mabomu ya rushwa n.k?Swali la tisa Je ni wakaazi wangapi wa Kigoma wanatumia safari za ndege za kimataifa mpaka apendelee kujenga uwanja mkubwa wa ndege badala ya kujenga barabara safi za lami viunganishi vya kigoma na Dodoma, Mwanza & Mbeya? Swali la kumi kwanini ameamua kujenga "Dubai" Kigamboni? Pesa itatoka wapi au nani ni mfadhili, je anatambua athari za ujenzi huo? Naona masaa 2 yatakuwa yameisha sasa.

  Ila kwa sababu wahandishi watakuwa wale wa TBC, Uhuru/Mzalendo, New Habari, na Daily News atapeta tu, sasa hivi (bila ya shaka) anapitia orodha ya maswali aliyopewa jana jioni.
   
 13. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,936
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  1. Nini maana ya Urais ni suala la kifamilia? 2. Je, katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepitwa na wakati?
   
 14. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mtaka Haki uko makini sana, nimependa maswali yako!...Itakuwa ni ajabu kama yote ama nusu ya maswali ya aina hii hayataulizwa!
   
 15. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #15
  Oct 29, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,390
  Likes Received: 3,719
  Trophy Points: 280
  Ahadi ulizotoa mwa huu zina gharama ya TShs. (au USD) ngapi...??
   
 16. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #16
  Oct 29, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,390
  Likes Received: 3,719
  Trophy Points: 280
  Lazima utakuwa hujaelewa nini muanzisha hii mada anataka..........!!!!
   
 17. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #17
  Oct 29, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
   
 18. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #18
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nawaomba msiache maswali haya wana ccm wenzetu kwa maslahi ya taifa.
   
 19. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #19
  Oct 29, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,390
  Likes Received: 3,719
  Trophy Points: 280
  Bajeti ya ziara za raisi nje ya nchi ni shilingi ngapi na katika hizo ametumia kiasi gani kwa miaka hii mitano iliyokuwa madarakani......???
   
 20. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #20
  Oct 29, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  mmeshampa madesa sasa, nyinyi mngetuma kwenye private message. Lakini hata hivyo naamini mkwere ni mkwere tu hamna kitu juu
   
Loading...