Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Badala ya kuvunja baraza kama wengine wanavyotarajia au kutegemea Rais anaweza kufanya tu mabadiliko makubwa (major reshuffling) ambayo yatagusa karibu wizara zote lakini yasimguse Waziri Mkuu. Hii itakuwa ni katika kuonesha kuwa ana imani na Waziri wake Mkuu lakini hana imani na mawaziri wengine na itakuwa ni njia rahisi ya kupunguzia serikali mzigo wa kikao cha Bunge kumpitisha Waziri Mkuu mpya au kutengeneza WM wa zamani ambaye ataanza kupata mafao ya ki-waziri mkuu mapema zaidi kuliko kama angeachwa kumaliza ngwe nzima.
Najiuliza zaidi kuwa kama WM ataachwa kura ya kutokuwa na imani naye bado itaendelea kwani ilikuwa predicated na wazo kwamba mawaziri wakijiuzulu au kuondolewa basi WM hatopigiwa kura ya kutokuwa na imani naye...?