MDAHALO WA IJUMAA: Waziri Mkuu akiachwa na wengine kubadilishwa itaridhisha?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Badala ya kuvunja baraza kama wengine wanavyotarajia au kutegemea Rais anaweza kufanya tu mabadiliko makubwa (major reshuffling) ambayo yatagusa karibu wizara zote lakini yasimguse Waziri Mkuu. Hii itakuwa ni katika kuonesha kuwa ana imani na Waziri wake Mkuu lakini hana imani na mawaziri wengine na itakuwa ni njia rahisi ya kupunguzia serikali mzigo wa kikao cha Bunge kumpitisha Waziri Mkuu mpya au kutengeneza WM wa zamani ambaye ataanza kupata mafao ya ki-waziri mkuu mapema zaidi kuliko kama angeachwa kumaliza ngwe nzima.

Najiuliza zaidi kuwa kama WM ataachwa kura ya kutokuwa na imani naye bado itaendelea kwani ilikuwa predicated na wazo kwamba mawaziri wakijiuzulu au kuondolewa basi WM hatopigiwa kura ya kutokuwa na imani naye...?
 
Diapers%2BAnd%2BPoliticians%2BShould%2BBe%2BChanged%2BOften%2BBoth%2BFor%2BThe%2BSame%2BReason.jpg

hivi wewe huchoki?
 
Je, watakaoteuliwa hawawezi kufanya ufisadi?

Ngereja kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri alipiga kelele sana kuhusu extension ya mkataba wa TICTS, na alimpiga madongo mazito Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi zama hizo. Few years later, na yeye amekuwa fisadi na si ajabu ni fisadi kuliko hata huyo Waziri wa wakati huo.

Kama hakuna hatua zitakazochukuliwa kwa waliofanya ufisadi, then ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu. Hata tubadilishe Waziri Mkuu au kuweka mawaziri wote wapya, hakuna la maana, sana sana wanazidi kutafuta namna ya kujificha.

Kikwete alipoingia madarakani alikuja na almost wote wapya, kama kubadilisha mawaziri ingekuwa suluhu, basi walioingia zama za JK wasingefanya ufisadi.

Ufisadi ni mwendelezo. Mwanakijiji nikukumbushe tu kwamba Mama Zakhia Meghji alipohojiwa kuhusu gharama kubwa za Ujenzi wa Twin Towers, alisema kwamba ni gharama za kawaida na kwamba Tanzania inaingia gharama hizo kwa kuwa wanataka kujenga Jengo la Benki Kuu ambalo lina hadhi. Sikutegemea kauli km hiyo, lakini sidhani kwamba aliisema toka moyoni, alikuwa akifunika madudu fulani, japo baadaye walikuja kumfunga Liyumba.

Mama Meghji huyo huyo alitaka kufunika uozo wa KAGODA, sijui ni kitu gani kilikuja kutokea akabadilisha kauli yake kwamba alikuwa misled na Ballali.

Baada ya Msabaha kufanya madudu ya Richmond, alihamishwa. Akawekwa Karamagi, yeye ndo akaua kabisa, akahamisha mkataba wa Richmond na kuwapa Dowans. Wote wakaondoka, tukaletewa Ngeleja ambaye wote tunajua madudu yanayoendelea Wizara ya Nishati na Madini. Juzi amediriki kulidanganya Bunge kuhusu Kiwira. Madudu ya Kiwira yalifanyika zama za Mkapa na Yona, ajabu ni kwamba Ngeleja anaendelea kufunika uozo huo kwa kupulizia perfume.

Kama tunataka ku-deal na tatizo la ufisadi na uwajibikaji wa mawaziri, suluhisho sio kubadilisha Baraza au kuleta awamu nyingine ya CCM, bali ni kuleta utawala mpya kabisa wa chama tofauti. Chama tofauti kikiingia kina jeuri ya kufumua uozo wote uliofanywa zama za Mwinyi, Mkapa, na JK. Lakini kama ni mawaziri wa CCM, tusitegemee lolote la maana.

Ufisadi wote mkubwa unaofanyika, una mikono ya Ikulu. Ufisadi mkubwa uliofanyika zama za Mkapa, JK ameshindwa kushughulikia, maana akisema ashughulikie mwisho wa siku Mkapa na watu watakwenda Segerea na JK hayuko tayari hilo. Hata akija mwingine yeyote kutoka CCM, stori itakuwa ni hiyo. Mawaziri wakipewa "ulaji" [wakiteuliwa] wanaendeleza ufisadi kwa kuwa wanaamini kwamba yeyote mwingine atakayekuja kuteuliwa hatakuja kufunua mdomo kumwangamiza, so wanaendelea kutafuna kama mchwa au dumuzi (scania).
 
Badala ya kuvunja baraza kama wengine wanavyotarajia au kutegemea Rais anaweza kufanya tu mabadiliko makubwa (major reshuffling) ambayo yatagusa karibu wizara zote lakini yasimguse Waziri Mkuu. Hii itakuwa ni katika kuonesha kuwa ana imani na Waziri wake Mkuu lakini hana imani na mawaziri wengine na itakuwa ni njia rahisi ya kupunguzia serikali mzigo wa kikao cha Bunge kumpitisha Waziri Mkuu mpya au kutengeneza WM wa zamani ambaye ataanza kupata mafao ya ki-waziri mkuu mapema zaidi kuliko kama angeachwa kumaliza ngwe nzima.

Najiuliza zaidi kuwa kama WM ataachwa kura ya kutokuwa na imani naye bado itaendelea kwani ilikuwa predicated na wazo kwamba mawaziri wakijiuzulu au kuondolewa basi WM hatopigiwa kura ya kutokuwa na imani naye...?

Mkuu kwa jinsi hoja ile ilivyoanzishwa inaonekana tatizo kubwa si waziri mkuu bali wale mawaziri. Ilisemwa kwamba Mawaziri wanaotuhumiwa kwa ufisadi ndani ya wizara zao wajiuzulu na kama hawajiuzulu basi wamuweke rehani waziri mkuu. Mawaziri hawakujiuzulu hivyo ukaanza mchakato wa kumuweka rehani waziri mkuu kwa kuanzisha mchakato wa kupeleka hoja ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na PM. Hivyo basi mawaziri wakiondoka/wakiondolewa watakuwa wametimiza lile sharti la kwanza kwamba mawaziri wajiuzulu (wajuizulu ama waondolewe/wasiwepo) hivyo basi basi waziri mkuu ataondoka rehani.

Hapa kuna mtego mwingine tena. Waziri Mkuu alikuwa anawekwa rehani kwa kushindwa kuwasimamia mawaziri hivyo wakiondoka wakaja wengine waziri mkuu atakuwa amepata uwezo wa kuwasimamia? Naona vicious cycle hapa
 
itabidi ajifunze kutokana na makosa yaani aanze kuwasimamia ipasavyo.
Mkuu kwa jinsi hoja ile ilivyoanzishwa inaonekana tatizo kubwa si waziri mkuu bali wale mawaziri. Ilisemwa kwamba Mawaziri wanaotuhumiwa kwa ufisadi ndani ya wizara zao wajiuzulu na kama hawajiuzulu basi wamuweke rehani waziri mkuu. Mawaziri hawakujiuzulu hivyo ukaanza mchakato wa kumuweka rehani waziri mkuu kwa kuanzisha mchakato wa kupeleka hoja ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na PM. Hivyo basi mawaziri wakiondoka/wakiondolewa watakuwa wametimiza lile sharti la kwanza kwamba mawaziri wajiuzulu (wajuizulu ama waondolewe/wasiwepo) hivyo basi basi waziri mkuu ataondoka rehani. Hapa kuna mtego mwingine tena. Waziri Mkuu alikuwa anawekwa rehani kwa kushindwa kuwasimamia mawaziri hivyo wakiondoka wakaja wengine waziri mkuu atakuwa amepata uwezo wa kuwasimamia? Naona vicious cycle hapa
 
Nimeuliza hili kwa sababu dalilii ya kukamilika kwa illusion kunakaribia! Kwamba, wataingia wengine na WM atabakia, JK atabakia na tutaambiwa "tuwape nafasi" na kuwa "hawa wanafaa"!!!
 
Serikali ya sisiemu yote ni janga la kitaifa,we fikiria prezda anashirikiana na mawaziri kuiibia nchi.
 
Nigekuwa Pinda, hiyo nafasi nisingeikubali tena. Nina wasiwasi hata Lowasa atakuwa "aliingizwa town"
 
Nimeuliza hili kwa sababu dalilii ya kukamilika kwa illusion kunakaribia! Kwamba, wataingia wengine na WM atabakia, JK atabakia na tutaambiwa "tuwape nafasi" na kuwa "hawa wanafaa"!!!

Itakuwa imekidhi haja ya mtoa Hoja ZK aliyesema, '' Naomba mnisikilize kwa ukamiki, sie tuna mamlaka na mtu mmoja tu na huyu ni waziri mkuu, kwa kuwa ameshindwa kuwawajibisha hawa mawaziri (Ubavu ambao hana kwa mfumo wa utawala wa ******) sie tutamwajibisha'' mwsiho wa Nukuu

Pili, Mdahalo wa IJUMAA Ungenoga sana kama ungeangazaia Mdudu anayeitafuna Mahakama Nchini maamuzi yanajulikana hata kabla ya hukumu tena wiki mbili kabla, hapa nazungumzia heart breaker ya leo SINGIDA, sitaki kuamini kinachokwenda kutokea leo. WEKA MASIKIO WAZI
 
Msitu ni ule ule, ngedere ni wale wale, sitegemei watakaoteuliwa upya kama watafanya maajabu chini WM. Nachofikiri ni kuondolewa kwa malipo ya WM pindi anapoachia chaka na awe kama wazee wengine wanaostaafu na kuishi kwa kutegemea pensheni zao badala ya kuendelea kuifilisi nchi.
 
Mimi napendekeza asiondoe waziri yeyote na pia asimwonoe WM ili serikali yake iliyotukuka iendelee kuchapa kazi.
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
 
Msitu ni ule ule, ngedere ni wale wale, sitegemei watakaoteuliwa upya kama watafanya maajabu chini WM. Nachofikiri ni kuondolewa kwa malipo ya WM pindi anapoachia chaka na awe kama wazee wengine wanaostaafu na kuishi kwa kutegemea pensheni zao badala ya kuendelea kuifilisi nchi.

cha msingi ni kuimarisha checks & balances. bunge likiendedelea kutimiza majukumu yake ya kikatiba kutakuwa na mabadiliko.
 
Mkuu kwa jinsi hoja ile ilivyoanzishwa inaonekana tatizo kubwa si waziri mkuu bali wale mawaziri. Ilisemwa kwamba Mawaziri wanaotuhumiwa kwa ufisadi ndani ya wizara zao wajiuzulu na kama hawajiuzulu basi wamuweke rehani waziri mkuu. Mawaziri hawakujiuzulu hivyo ukaanza mchakato wa kumuweka rehani waziri mkuu kwa kuanzisha mchakato wa kupeleka hoja ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na PM. Hivyo basi mawaziri wakiondoka/wakiondolewa watakuwa wametimiza lile sharti la kwanza kwamba mawaziri wajiuzulu (wajuizulu ama waondolewe/wasiwepo) hivyo basi basi waziri mkuu ataondoka rehani.

Hapa kuna mtego mwingine tena. Waziri Mkuu alikuwa anawekwa rehani kwa kushindwa kuwasimamia mawaziri hivyo wakiondoka wakaja wengine waziri mkuu atakuwa amepata uwezo wa kuwasimamia? Naona vicious cycle hapa

Kimbunga: Kwa maelezo yako sasa naona Waziri mkuu atawekwa rehani ambayo itakuwa inapanda bei kadri tunavyoelekea 2015, tutarajie misuguano zaidi ndani ya CCM ikisaidiwa na nguvu ya umma, wabunge hawawezi kukaa kimya wakiona wanainchi wanazidi kuwa hoi kisa wao wanatoka upande wa CCM, Wengi wao wamepita kwa taaabu sana na CCM yao toka majimboni kwao hilo wanalijua vizuri tu, hivyo hawatakubali 2015 kazi iwe kubwa mara mbili na amini maneno yangu kabla ya uchaguzi wa 2015 upinzani utavuna mavuno makubwa sana mpaka watakosa maghala.
 
waziri mkuu kaachwa na hajaguswa bali kuna mabadiliko makubwa katika baraza la mawaziri. ambapo j. makamba, H.kigwangala,S.masele C.tizeba na wengine wamo katika baraza la mawaziri...na kesho ndio kuna press conference pale ikulu..leo asubuhi kurugenzi ya mwasiliano ikulu itavialika vyombo vya habari hapo kesho saa tisa alasiri pale ikulu.
 
Itakuwa imekidhi haja ya mtoa Hoja ZK aliyesema, '' Naomba mnisikilize kwa ukamiki, sie tuna mamlaka na mtu mmoja tu na huyu ni waziri mkuu, kwa kuwa ameshindwa kuwawajibisha hawa mawaziri (Ubavu ambao hana kwa mfumo wa utawala wa ******) sie tutamwajibisha'' mwsiho wa Nukuu

Pili, Mdahalo wa IJUMAA Ungenoga sana kama ungeangazaia Mdudu anayeitafuna Mahakama Nchini maamuzi yanajulikana hata kabla ya hukumu tena wiki mbili kabla, hapa nazungumzia heart breaker ya leo SINGIDA, sitaki kuamini kinachokwenda kutokea leo. WEKA MASIKIO WAZI

nasubiri hukumu itoke then tutajulishana mchawi ni nani...maana mchezo mchafu ulikuwepo
 
Naona System Ndio Tatizo!! sisi wenye nchi Tunachotaka na Hawa Wahujumu Uchumi Tuwaone wakifuatiliwa na Takukuru na Kwenye Mahakama wakijibu tuhuma zao!! Sio watu waendelee Kuponda Mali walizochuma Kifisadi (usd 410,000 kwa miezi 16!!!!!) Halafu tusema kubadilisha inatosha!! That is a joke!!
Pia waziri Mkuu ameprove failure ya kuwasimamia mawaziri wenzake na sioni sababu yoyote ya yeye Kuendelea Kuwepo
Tumkumbuke mzee wa kararacha alionjeshwa Unaibu mkuu kidogo ila alifanya wonders!! Sasa iweja kwa huyu full Waziri Mkuu unashindwa Hata kuwajibisha mkurugenzi wa Halmashauri? Kuna Haja gani sasa ya Huyu Mtendaji?
 
halafu moja mbili tatu........watabadilishwa wizara tu na sio kuondoshwa. katika 50 labda 20 tu ndo watakuwa wapya, na hao wapya wana historia ya kuvurunda kwenye maofisi kabla ya kuingia kwenye siasa, ni swala la mda tu..............ngoja tusubiri.
 
Back
Top Bottom