MDAHALO SHIRIKISHI: Ushindi wa Joshua Nassari Arumeru Mashariki Umeletwa na Wana CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MDAHALO SHIRIKISHI: Ushindi wa Joshua Nassari Arumeru Mashariki Umeletwa na Wana CCM

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 3, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kwamba, bila wana CCM Joshua Nassari asingeweza kushinda kiasi kikubwa hivyo; CCM imepata kura pungufu karibu 7000 kulinganisha na 2010 wakati CDM imepata karibu 6000 zaidi kulinganisha na 2010. Idadi ya wapiga kura katika chaguzi zote mbili imetofautiana kwa watu kama 4000 hivi! Ina maana kuna wana CCM walioipigia kura CCM 2010 lakini wakageuka na kupigia CDM safari hii!!

  Kwenye mambo ya kampeni wanaita "the x factor".. ndio hao!
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  hilo ni kweli kabisa kwani huwezi kulazimishwa kumkubali mtu msiyemjua ni ngumu sana kama msipo iba ndicho kilichotokea alumelu..
   
 3. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mwanakijiji kuna watu huwa hawapendi kushiriki Mageuzi Mpaka wasikie kwamba "Mbona yamefanyika Sehemeu Nyinge?". Naamini kabisa Ushindi wa CDM katika Majimbo ya Mbeya, Mwanza, Iringa na Arusha yalileta Mwamko Mkubwa hata kwa Wale waliokuwa hawaamini katika Mabadiliko na kuipigia CCM. Sasa huu uchaguzi umekuwa Fursa kwa wale walioipigia Kura CCM kwa Uoga wa Mabadiliko Kulipiza Kisasi.

  CCM is dying maana Pamoja na Mkuu Kututangazia Matokeo Mapema Bado kulikuwa kuna Wana CCM waliokuwa wanasubiri Kile walichozoea kukiita "Kura za Vijijini"

  Mkuu Kwa Kifupi Ushindi wa Nasari Haujaletwa na CCM wala CDM bali ni WANA ARUMERU WENYEWE Ambao kwa Pamoja wameamua kuiambia CCM kwamba "You can fool some people some times but you can't fool the people all the time"
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Apr 3, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Kwani hakuna "independents"? Inawezekana hao "independents" ndiyo walikuwa swing voters waliompatia ushindi bwana Nassari....
   
 5. J

  JacksonMichael JF-Expert Member

  #5
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 339
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huwezi kutoa tathmini kama hiyo kwa kuwa huja-merge waliopig kura this time(2012) na 2010 kwa kutumia ID zao.
  kwa kuwa waliopiga kura ni nusu ya watu wote waliojiandikisha kupiga kura! na hivyo ndivyo inawezekana watu wapya kabisa ambao hawakupiga kura kabisa lakini walikuwa na sifa zote za kupiga kura ndio waliokuwa na mwamko wa kupiga kura this time na wale baadhi ya waliopiga kura 2010 wamekata tamaa na hawakushiriki kupiga kura, Who knows?

  Tathmin yako inalack mathematical and statistical backup!, HAKUNA MDAHALO HAPO.

  Ni hayo tu
  The "wakojacko"
   
 6. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #6
  Apr 3, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  mkuu mwanakijiji sababu za ushindi wa chadema ni nguvu ya umma pekee!
  Ungekuwepo arumeru ungewaona vijana hasa makondakta wa daladala,vibarua wa mashamba ya maua na wanawake wauza nyanya(hawa wote hawana kadi za vyama) walivyopiga kampeni halafu wakajitolea uhai wao kulinda kura.
   
 7. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #7
  Apr 3, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kwanza kabisa ushindi wa Nassari ni matokeo ya sauti ya wana Arumeru. Pia kama ujuavyo vita vya panzi furaha ya kunguru.
   
 8. k

  katesh Senior Member

  #8
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nakubaliana na ww kbs kuwa ushindi wa nassari ni matokeo ya makundi ndani ya ccm. Wanaobeza acha wabeze lkn ukweli ndio huo.
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Apr 3, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Mdahalo shirikishi kwa kimombo ndiyo 'interactive debate'?
   
 10. Shukurani

  Shukurani JF-Expert Member

  #10
  Apr 3, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 253
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji
  Siamini katika hili, Ushindi huu ni matokea ya wananchi kuchoka kusikia habari zile zile. maneno mengi pasipo vitendo ambayo yametawala ndani ya CCM. Darasa alilotoa Dr Slaa mwaka 2010 alipopata nafasi ya kuzunguka nchi nzima haya ndiyo matunda yake yanaanza kuonekana. Wananchi wanaanza kuamini kuwa bila CCM maisha yao yataendelea kama kawaida. Kule mwanza, 2010, watu walikuwa radhi kupigia kura jiwe kuliko CCM. Tukubali jamani, wanaCCM wavurugane wasivurugane wakati wao unahesabika. Kumbuka brother, kwa wale waumini wa philosophy wanakuambia "HAKUNA UTAWALA UTAKAO SIMAMA MILELE" UTAWALA WA ROMA HUKO WAPI? HUKO ZAMBIA, KENYA LEO WAKO WAPI? Haya ya Arumeru ni upepo unaotuelekeza 2015.
   
 11. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #11
  Apr 3, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mwanakijiji, it is a little bit hard to debate while not much is known as to why more than half of registered voters did not make it to the polling stations. More than 120,000 were registered and it is about 60,000+, why is it so? Why would you say CCM imemsaidia mgombea wa CHADEMA kushinda, and not TLP, NRA or other parties? What did candidates say during the campaign trail, did they say anything different, may be one of them was more up to issues that matters most to voters and the constituent, and the other was more to the image of the party. Kuna mengi tunapaswa kuyajua kwanza kwenye mjadala huu shirikishi kabla ya kuyashirikisha kwenye mjadala.
   
 12. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #12
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  kwa kiasi fulani ndio, CCM imechangia ushindi wa CHADEMA.

  Mchakato wa kumpata mwakilishi wa chama chao sioni kama ulikuwa wa haki. Inawezekana waliacha mtu ambaye angekuwa mwakilishi bora.

  Mpasuko katika mchakato tu wa kupata mwakilishi ulileta mgawanyiko ndani ya chama. Kuna ambao walikuwa hawataki mwakilishi huyo ashinde ili kumdhoofisha aliyempigia debe.

  Hata ukiangalia kwenye kampeni za huko, kuna kundi fulani wheter CCM B or C hawakujihusisha kabisa.

  Strategy yao pia imewaangusha hasa kwa kuanza kushambulia watu badala ya kujenga hoja na kushindwa kurekebisha kosa hili mapema.


  Kwa upande mwingine, CDM walikuwa na nafasi yao kama chama kinachogombea.

  Kwanza mgombea wao alishasimama tena kugombea hapo kitu nachoona kilimpa urahisi sababu kama mwanasiasa mchanga hata kule kusimama jukwaani kwa kujiamini ina marks zake.

  Ushiriakiano wa siafu waloonesha CDM hasa katika kusimamia kura zao kwa uaminifu bila kukubali kununuliwa.

  Busara za kujua udhaifu wa adui na kuutumia against adui, yale matusi ya CCM yamewagharimu na CDM hata kama walijibu, ilikuwa strategic sana.

  Kuhusu 'x factor' naona, hata wanachama wenye kadi ya uanachama fulani huwa wanaangalia mtu wanayempigia kura.
  'Undecided voters'

  Lakini pia kuna dhana ya uchakachuzi, siwezi itetea sana hapa japo ipo kwenye background ya akili yangu. Hatuna details za yaliyofanyika 2010.
   
 13. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #13
  Apr 3, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hizi chaguzi za ki ccm ccm huwezi kuzifanyia statistical analysis kuna kura
  zingine zinaingia zikiwa ndani ya chupa za chai na hot pots sasa sijui hizo mahesabu yake ndo yakoje.
   
 14. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #14
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  No matter the situation was, people wanted to see new face apart from that one of the noble class,status quo and of high profile clan.

  Binafsi naamini ilikuwa ni nafasi mwafaka kwa Nassari kupewa nafasi ili nae ajaribu badala ya hadithi zile zile za tuta.......
   
 15. Lavie

  Lavie Member

  #15
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wameshindwa tu hizo zingine ni propaganda. Hakuna mweleka usio na sababu.
   
 16. bullet

  bullet JF-Expert Member

  #16
  Apr 3, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Wana Arumeru wangekuwa watu wa ajabu kumchagua Sioi! Kwanza walimchagua baba yake ambaye hakuwahi hata kuapishwa! Leo wamchague mwanae ambaye hata hakujipigia kura! It would have been far ahead the monarch system! Watu walioelevuka kama Arumeru hawawezi kamwe kufungwa boya kiasi hicho! Ushindi wa Nasari ni wa wana Arumeru! They are fed na kudanganywa tangu uhuru! Wameamua kushirikisha ubongo na uamuzi wao!
   
 17. M

  Mr Emmy JF-Expert Member

  #17
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 1,201
  Likes Received: 289
  Trophy Points: 180
  Do u Mean Arumeru? au alumelu ni kitu gani hebu fafanua
   
 18. U

  Uswe JF-Expert Member

  #18
  Apr 3, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  MM nilikua nakaribia kuanza post hapa kuwaomba wanaJF kwamba tuache kumshambulia bwana Lusinde, badala ya kumshambulia kwa maneno makali makali tunahitaji kumpongeza na pengine kujenga ushawishi ili awe MKURUGENZI WA CAMPAIGN WA CCM KWA 2015.

  Baada ya kutafakari niligundua kwamba Lusinde alifanya kazi kubwa sana katika ushindi wa nassari kuliko mwanaCDM yeyote, kuliko hata ile timu ya campaign ya CDM

  Ni kweli MM ushindi huu mnono na mtamu umeletwa na CCM!
   
 19. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #19
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  CCM hawana uwezo wa kushinda mijini na semi urban bila kuchakachua kura.Wananchi wakishirikishwa kulinda kura na kujiamini CCM hawawezi kuchomoka kamwe.
  CCM wanajua kuwa wanaopiga kura hawawezi kuzidi 60% ya waliojiandika, mdio maana hununua shahada na kutengeneza kura kwa kushirikiana na Tume ya uchaguzi na kusaidiwa na dola hutengeneza vituo hewa (rejea Arumeru East juzi) ili kujiongezea kura.
  Wizi,ufisadi na uchukuaji kura ndio unaowapa ushindi CCM.
  AZIMIO LA JIPYA LA ARUSHA: ONDOA CCM TANZANIA!
   
 20. M

  Mr Emmy JF-Expert Member

  #20
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 1,201
  Likes Received: 289
  Trophy Points: 180
  Zambia walijaribu kuwapa nchi wapiinzani kwa kukiondoa chama Tawala Cha Mh Kaunda kilicho pigania uhuru wa nchi hiyo lakini hatimayake wameona machungu ya kutawaliwa na wapinzani mimi napenda kuita magenge ya watu wachache yanayojifanya kuwa na ngozi ya kondoo sasa hivi ili yakabidhiwe nchi kwa kutumia madhaifu ya vyama Tawala ambayo yanarekebishika. ZAmbia baada ya kuonja miongo kadhaa ya utawala wa upinzani wakaamua kukirudisha madarakani chama cha mzee kaunda kiongozwa na Mh Satta.

  Kenya leo hii hawana amani ya kisiasa hii inatokana tu na Magenge ya wanasiasa wachache kipindi cha mwaka 2002 Raila Odinga, Kibaki na Rutto wakiungana na kuanzisha chama cha upinzani National Rainbow Coalition (NARC) ambacho kilifanikiwa kukiondoa madarakani KANU but miaka 4 baadae Genge hilo la wanasisa liligawanyika tena kwa maslahi binafsi na kuunda chama cha ODM na Party of National Unity. ambacho kiliunganisha mabaki ya NARC na vyama vingine kama KANU, ford Kenya NK. katika uchaguzi wa mwaka 2007 chama cha kibaki PNU kwa kushirikiana na KANU kilishinda uchaguzi huo ambao ulizua utata na kusababisha kuundwa kwa serikali ya mseto na chama cha upinzani ODM cha R. Odinga na Rutto.

  Baada ya Magenge yote kuonja utamu wa nchi ya Genge la NARC, PNU na ODM ambao walikuwa wapinzani kuibuka tatizo lingine la uasi ndani ya magenge hii nikutafuta tu njia ya kuitafuna nchi ya Kenya ikaanza kwa Railla Odinga kutofautiana na swahiba wake wa Karibu William Rutto na Kibaki kutofautina na Uhuru kenyeta na hiyo imesababisha siasa za kenya kuwa za hovyo kabisa na sasa Wakenya wanaikumbuka KANU yao and I hope soon KANU itarudi madarakani kama ilivyokuwa kwa zambia.

  Maoni yangu kwa Watanzania tumeona mapungufu katika CCM cha kufanya sio kubadili chama ila ni kubadilisha mfumo na watu/ wanachama wenye sifa chafu ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kali za kinidhamu na kisheria na kusisitiza mabadiliko ndani ya chama kulingana na wakati na kizazi kilichopo sasa.

  Kubadilisha chama na kuweka wapinzani ( magenge ya watu yalioanzisha vyama vya siasa kwa masilahi binafsi na kufanya vyama vya siasa kama makampuni binafsi ni hatari kwa kataifa letu unaweza usione leo lakini kizazi kinachokuja kitakuja kupata tabu. Tuungane pamoja sasa kufanikisha mabadiliko ndani chama mapinduzi kwa mustakabali wa Taifa letu
   
Loading...