Mdahalo: Ndugai vs Lissu - Jumamosi Julai 30

Status
Not open for further replies.
Mh Naibu Speaker kajitangazia ushindi mnono wa hiyoo kesho! alijitangazia ushindi huo leo asbh wakati wa kutoa matangazo ndani ya mjengo.
Ilivyoonekana alikuwa na hofu khs mdahalo huo.
aliwaomba walipukaji wenzie wawepo kesho ndani ya mdahalo kumpa support kiaina wakati akitangaza mjengoni!, alionyesha hofu kubwaaa..!!!

huyo Bibie Mwendesha mdahalo inavyoonyesha ana usongo na walipukaji....., habari za chini ya jamvi nackia alikuwa ameajiriwa na Habari Corporations ya Rostam Aziz.
Baadae Mh Rostam akampiga chini kiaina! so still ana usongo na walipukaji mjengoni!

Muhimu 2waombe TANESCO chini ya Mh Ngeleja wasijeficha aibu kwao kwa kuuchukua Umeme wao!

Inaonyesha hujui unachokiandika. Na hapo kwenye red ndo kabisaa uongo wa mchana. Ni kweli alikuwa Mkurugenzi wa Habari Coorporation Ltd. Rosemary ali-resign yeye mwenyewe kwa sababu hakutaka kuingiliwa katika utendaji wa shirika kama MD.

Mimi kwa upatu wangu naona utakuwa mdahalo mzuri sana kama Lissu atapunguza jazba na kuzungumza vizuri kwani Ndugani ni mwanasheria mahiri sana na mtulivu sana katika kupambana na hoja.

Nazidi kusisitiza kuwa LISSU apunguze jazba ili mjadala uwe mzuri kwa faida ya wachangiaji na watanzania wote kijumla .

nawatakia mafaniio mema.
Kama ndungai ni mwanasheria mahiri na makini, na ametulia nina shaka na waliobaki..
TUACHE USHABIKI HATA KATIKA FANI TU HUWEZI HATA KIDOGO KUMFANANISHA NDUNGAI NA LISSU. ninakuelewa kutokana na mapenzi ya wazi.. Bora Ndungai asikimbie mdahalo.. Ukweli utauona

Waiting for this moment to come and see degrees of arguments and issues presentation , ila am sensing power blackout hiyo kesho ikifika!

OPTION,mdahalo urushwe kwnye redio pia,kwani endapo umeme utakatwa itakuwa easy kusikiliza mdahalo kupitia simu.
Huo mdahalo sidhani kama utatokea, lazima Ndugai ataingia mitini. Ila kama ikitokea unafanyika muulizeni Ndugai kuhusu kutelekeza mkewe wa ndoa na kumuacha anauza machungwa

Hatafika huyo. La sivyo atakodi magamba na kuwaandalia maswali ya kumuuliza LISU. CHONDE CHONDE, Mwakitwange usije ukawa unatumika na magamba, tunataka mdahalo wa haki na sio wa upendeleo.

Lissu amtolee uvivu huyu Naibu Spika na amuulize kama macho yake yana uwezo wa kuuona upande mmoja tu yaani upande wa CHADEMA & NCCR- Mageuzi.

Ni vizuri sana, lakini natoa rai ya kuwataka kuwa wavumilivu, kwa kuacha mhemko, Na swala la msingi zaidi ni maslahi ya nchi na si vyama kama tunavyoona sasa bungeni

Hawa waliondaa mdwalo nao waangalie kwanza kabla ya kuandaa midawalo. Hapo wangemuweka Ndugai na Mama Kiroboto

..namshauri Tundu Lissu ajiandae vyema kwa ajili ya mdahalo huo.

..Ndugai si mtu wa kumdharau ukizingatia kwamba alimdhibiti Freeman Mbowe ktk mahojiano waliyofanya pamoja.

..katika mdahalo wake na Mbowe, Job Ndugai alifanikiwa kujenga taswira kwamba wabunge wa CDM ni watu wasiojua sheria na taratibu za bunge, pamoja wajibu wao kama wawakilishi wa wananchi. The sad thing ni kwamba Mbowe alishindwa kujibu mashumbulizi hayo.

..tusimdharau Ndugai, he can do some damage to CDM's image and reputation. tusisahau kwamba he comes across as an innocenct, calm, and collected individual.

Sina cha kuongeza mkuu.

lissu inabidi awe mtulivu na ajipange,ndugai anajua pa kusimamia hasa kanuni.lissu ajipange wala tusimdharau ndugai na hatumsaidi lissu kwa sifa pekee.tumjenge kwa kumuongezea hoja hapa yeye si malaika

ikiwezekana wanaoweza kubandika matukio ya kufedhesha bungeni siku za nyuma tuweke hapa kumkumbusha lissu.ile si simba na yanga waungwana

Huo ni mdahalo kati ya serikari na wananchi.

Wananchi epukeni kwenda kuitetea serikari kwa maslahi ya ushabiki wa kichama.

Tunatakiwa tuhoji mstakabali wa maslahi ya kitaifa, sio tu kusema angalia serikari imefanya na tuna mikakati ya kufanya. Tunataka kuhoji serikari itawajibikaje kwa wananchi dhidi ya umaskini unaozidi kukithiri, ujinga unaojengwa kwa kuwepo makundi miongoni mwa watanzania, na afya zinazozorota kwa ukosefu wa mikakati thabiti ya kuboresha huduma. Na hata namna gani serikari itaondoa uonevu wa vyombo vyake vya dola n,k.

TAASISI ya Vox Media Centre Tanzania na East Africa Business and Media Training Institute (EABMTI) kwa ushirikiano na kituo cha Star TV kesho wataendesha mdahalo wa kibunge, mada ni ‘Bunge la 10 na Tanzania tunayoitaka’. Taarifa kwa vyombo vya habari iliyopatikana Dar es Salaam jana kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Vox Media, Ansbert Ngurumo, inaeleza kuwa mdahalo huo utafanyika kwenye ukumbi wa Mtakatifu Gaspar mjini Dodoma.

Kwa mujibu wa Ngurumo katika taarifa hiyo, wazungumzaji wakuu kwenye mdahalo huo ni Naibu Spika Job Ndugai na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani, Tundu Lissu, huku wananchi 200 wakipata nafasi ya kuwauliza maswali; mdahalo huo utarushwa hewani kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 1:50 usiku. Inaelezwa kwenye taarifa hiyo kuwa ni fursa nyingine kwa wananchi kujadili masuala nyeti yanayohusu uhai wa taifa kwa kumulika, kuhoji na kutafakari namna Bunge linavyowawakilisha.

“Ni fursa yetu kupima utendaji wa wabunge na kuhoji kama wanakoelekea ndiko tunakopaswa…ni fursa pia kwa wazungumzaji wetu kusisitiza yanayopaswa na kukosoa yanayopotoshwa au kukosewa kuhusu Bunge, ni fursa kwa wabunge kujipima kwa maoni ya wananchi,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo. Katika mdahalo huo Mkurugenzi Mtendaji wa EABMTI, Rosemary Mwakitwange, ataongoza mdahalo huo kwa kushirikiana na wajumbe wengine wa taasisi hizo. Mwaka jana taasisi hizo ziliaandaa midahalo kadhaa wakati wa kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu iliyohusu wagombea urais wa Tanzania.

Tanzania Daima

Leo nimemsikia huyu Ndugai akitoa matangazo kikao cha asubuhi leo...amedai na hapa namnukuu...."KATIKA MECHI HII NAIBU SPIKA AMEKWISHA SHINDA" mwisho wa kunukuu....Yani huyu kilaza atapambana na Tundu mwanasheria aliyebobea,great thinker...Ndugai saizi yake ni akina Simbachawene,Kingwangala,Lusinde na vilaza wengine..........mtaona ukilaza wa huyu naibu spika wenu.....

Lissu hana ubavu kwa Ndugai, ni mgeni mno kwenye siasa. Na isitoshe Ndugai ni BOSS wa lissu

That brain, hivi si unajua JK ni boss wa Prof Mwandosya, lakini nani mwenye akili zaidi?
Ok, nabadilisha swali. JK ni boss wa Dr Magufuli, nani kilaza zaidi?
Labda nimekosea, ngoja niulize hivi. JK ni boss kwa Ananilea Nkya lakini nani anafuka pumba zaidi anapoongea?

Huna majibu ya maswali yangu, nyamaza kimya.

Huwezi kuwa na mdahalo wa kibunge madhubuti bila ya uwakilishi wa chama tawala.

Leo nimemsikia huyu Ndugai akitoa matangazo kikao cha asubuhi leo...amedai na hapa namnukuu...."KATIKA MECHI HII NAIBU SPIKA AMEKWISHA SHINDA" mwisho wa kunukuu....Yani huyu kilaza atapambana na Tundu mwanasheria aliyebobea,great thinker...Ndugai saizi yake ni akina Simbachawene,Kingwangala,Lusinde na vilaza wengine..........mtaona ukilaza wa huyu naibu spika wenu.....

Hapo tayari naona tatizo.

Mambo yanayotakiwa kuchukuliwa kwa gravity ya mustakabali wa nchi, watu ambao walitakiwa kuwa responsible wanayachukulia kama "mechi".

Wasukuma wangesema hizi habari nzima za parliamentary politics ni "mashikolo mageni".

Ofisi ya Spika, ambayo inamjumuisha Naibu Spika, inatakiwa kujichukulia kwa taadhima ya kutofungamana na upande wowote.

Kwa kushiriki katika vimidahalo hivi, vimidahalo ambavyo havieleweki na vimekosa balance - hakuna uwakilishi wa chama tawala, inaonekana kama ni ofisi ya Spika vs CHADEMA-, ofisi ya Spika inajiondolea hadhi hii.

Inavyoonyesha katika hao watu 200 mabunge ya magamba yanaweza kujaza nafasi zote ili kwenda kuzomea. Cha msingi na cdm wawahi au zimetolewa kadi za mwaliko?

Naomba Lisu atulie tu hakuna kitu ambacho magamba wanaweza kuongea mbele za watu wakasikilizwa kwa sasa. Hata kama angeenda Sugu, Ndugai angechemsha tu.

I suggest TANESCO wakate umeme wao geto kwangu mapema ili hiyo saa 1200 iwe zamu yangu kuwa na umeme. Pia nyinyi Star Tv jamaa anaehusika na Generator za kule kisarawe nae akumbushe kuwa makini mida hiyo manake hawa TANESCO mimi siwaamini kabisa

Refer uwanja wa Taifa Simba Vs Yanga

Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom