Mdahalo: Ndugai vs Lissu - Jumamosi Julai 30 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mdahalo: Ndugai vs Lissu - Jumamosi Julai 30

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jul 29, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  TAASISI ya Vox Media Centre Tanzania na East Africa Business and Media Training Institute (EABMTI) kwa ushirikiano na kituo cha Star TV kesho wataendesha mdahalo wa kibunge, mada ni ‘Bunge la 10 na Tanzania tunayoitaka’. Taarifa kwa vyombo vya habari iliyopatikana Dar es Salaam jana kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Vox Media, Ansbert Ngurumo, inaeleza kuwa mdahalo huo utafanyika kwenye ukumbi wa Mtakatifu Gaspar mjini Dodoma.

  Kwa mujibu wa Ngurumo katika taarifa hiyo, wazungumzaji wakuu kwenye mdahalo huo ni Naibu Spika Job Ndugai na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani, Tundu Lissu, huku wananchi 200 wakipata nafasi ya kuwauliza maswali; mdahalo huo utarushwa hewani kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 1:50 usiku. Inaelezwa kwenye taarifa hiyo kuwa ni fursa nyingine kwa wananchi kujadili masuala nyeti yanayohusu uhai wa taifa kwa kumulika, kuhoji na kutafakari namna Bunge linavyowawakilisha.

  “Ni fursa yetu kupima utendaji wa wabunge na kuhoji kama wanakoelekea ndiko tunakopaswa…ni fursa pia kwa wazungumzaji wetu kusisitiza yanayopaswa na kukosoa yanayopotoshwa au kukosewa kuhusu Bunge, ni fursa kwa wabunge kujipima kwa maoni ya wananchi,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo. Katika mdahalo huo Mkurugenzi Mtendaji wa EABMTI, Rosemary Mwakitwange, ataongoza mdahalo huo kwa kushirikiana na wajumbe wengine wa taasisi hizo. Mwaka jana taasisi hizo ziliaandaa midahalo kadhaa wakati wa kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu iliyohusu wagombea urais wa Tanzania.

  Tanzania Daima
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Je, Ndugai ana ubavu wa kushindana hoja na Tundu Lissu? Hapa naona mlima na kichuguu.
   
 3. Eshacky

  Eshacky JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 966
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Asikimbie mtu, maana hapo hakuna kuruka aya!
   
 4. M

  MCHARA Senior Member

  #4
  Jul 29, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 111
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hakuna jipya kwani Tundu Lissu hawezi kufananishwa na Ndugai kwa lolote labda umri tu. Ndugai kilaza na kuthibitisha hilo mliona jana alivowatoa kafara wapigania haki za wananchi!
   
 5. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hapo ni kazi si utani .Ndugu gani ? Maana si Ndiugani.Jamaa ni mtupu na sina hakika kama atakubali mh
   
 6. Mkiliman

  Mkiliman JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 957
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Waiting for this moment to come and see degrees of arguments and issues presentation , ila am sensing power blackout hiyo kesho ikifika!


  OPTION,mdahalo urushwe kwnye redio pia,kwani endapo umeme utakatwa itakuwa easy kusikiliza mdahalo kupitia simu.
   
 7. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #7
  Jul 29, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Mama Mary, tafadhali uendeshe mdahalo huu vizuri, isiwe kama ule wa Freeman Mbowe na Hamad Rashid. Ulianza vizuri baadaye ukashindwa kuongoza kisa vimaneno na kulalamikalalamika kwa wana-CUF.
   
 8. M

  Marytina JF-Expert Member

  #8
  Jul 29, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Makinda kadhihirika ni boya hata Ndugai ni boya tuu jmosi atapeperushwa
   
 9. P

  Penguine JF-Expert Member

  #9
  Jul 29, 2011
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Eshacky,

  Acha kujifanya Nabii na Mtume,
  Unataka kuniambia kwamba ukiwa umelala ukajiwa ktk maono ukaona mtu kama vile Naibu Spika akiukimbia huo Mdaharo kwa kivuli cha kupata udhuru au sijakuelewa vizuri? ha, ha, haaaaaaaaa. asikimbie mtu hapoooooo, TANESCO msiokoe aibu kwa kutuzimia umeme muda huo ukitimu.


   
 10. F

  FJM JF-Expert Member

  #10
  Jul 29, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Lissu amtolee uvivu huyu Naibu Spika na amuulize kama macho yake yana uwezo wa kuuona upande mmoja tu yaani upande wa CHADEMA & NCCR- Mageuzi.
   
 11. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #11
  Jul 29, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  kwa sheria za bunge Tundu ataumbuka, hazijui, ama sheria za nje ya bunge Tundu anazifahamu sema tatizo lake hajui kujenga hoja kwa lugha ya kawaida huwa anajenga hoja kwa lugha ya jaziba sana. kitu ambacho mimi siamini kama mtu kujenga hoja mpaka utumie jaziba
   
 12. escober

  escober JF-Expert Member

  #12
  Jul 29, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 391
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  i cant wait to see this battle. najua utakuwa mdahalo wa upande mmoja sababu Ngugai yupo empty kumpambanisha na Lissu. by the way hawa jamaa si walikataa midahalo kwenye uchaguzi watakubali kweli kuja?
   
 13. suleym

  suleym JF-Expert Member

  #13
  Jul 29, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,717
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  huyu mama wakati mwingine huharibu mdahalao this tym awe fair, ukikumbuka ule mdahalo wa mbowe na hamad rashid unatilia shaka huu kama atauendesha vyema. KIKUBWA TANESCO TU WASICHEZE RAFU HAPA.
   
 14. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #14
  Jul 29, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Lissu yupo vizuri zaid ya ndungai-
   
 15. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #15
  Jul 29, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  Ndugai hawezi kushindana na lissu sidhani kama atakuja
   
 16. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #16
  Jul 29, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,394
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Wakuu, huo muda mbona mimi nauona ni mfupi sana! Yaani kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 1:50 usiku! Sidhani kama saa 1 na dk 50 zitatosha kujadili mambo ya msingi kabisa na pia hao watu 200 watakaokuwepo ukumbini kupata nafasi ya kuwasilisha michango yao. Nina mashaka ya muda kuisha wakati mdahalo ndo kwanza unaanza.
   
 17. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #17
  Jul 29, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,177
  Likes Received: 1,180
  Trophy Points: 280
  Kwa hisan ya TANESCO tutawasikia.
   
 18. L

  LAT JF-Expert Member

  #18
  Jul 29, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  aahhhh .... wataleta wale vitoto vidogo kwenda kujaza nafasi ..... ndugai hana charisma ya uongozi kama wa uspika
   
 19. e

  erneus kyambo Member

  #19
  Jul 29, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru Mungu CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO(CHADEMA) Tumepewa fursa nyingine kuonyesha uwezo wetu wa kuwatetea watanzania pia ni nafasi nyingine adimu ya kuuanika usanii wa chama cha magamba(ccm) hadharan, Pls wanaJF tusikosee hiiii! Jobless Ndugugani baada ya Mbowe kukushika na kukuaibisha juu ya tafsiri ya kambi rasmi ya upinzani bungeni,unashikwa pabaya tena kesho na Tundu Lissu . . . . . ,
   
 20. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #20
  Jul 29, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  la msingi ni kuomba umeme uwepo-maana wanaweza kuupoteza siku nzima
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...