JamiiTalks MDAHALO(Mitandao ya Kijamii): Mahususi kwa wanafunzi wa vyuo na wahitimu wa elimu ya juu wa Tanzania

Status
Not open for further replies.
MDAHALO KUHUSU MITANDAO YA KIJAMII KWA VIJANA TANZANIA

Katika mwendelezo wa kuibua mawazo na mijadala katika suala la matumizi ya Mitandao ya Kijamii na Mtandao wa Internet kwa ujumla, JamiiForums imeandaa mdahalo kabambe kuhusu Mitandao ya Kijamii nchini Tanzania.

Lengo kuu la mdahalo ni kuibua hoja za msingi kutoka pande mbili zinazokinzana na kuzijadili kujua ukweli, maana, faida na hasara zake. Baada ya mdahalo wabobezi katika fani husika huchambua hoja zilizotolewa kitaalamu na wote kutoka na wazo moja litakalotusaidia katika maisha yetu na hata uhamasishaji kwa wengine.

Mdahalo utakaofanyika jijini Dar es Salaam siku ya Jumamosi tarehe 13 Oktoba 2018, utahusisha wanafunzi wa Vyuo na Wasomi mbalimbali kutoka fani mbalimbali.

=> Je, wewe ni mwanafunzi au mhitimu wa Elimu ya juu? Una umri wa kati ya miaka 20 na 35? Unapendelea kushiriki mijadala kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii(social media)? Basi unaweza Kushiriki.

Maombi ya ushiriki yatafanyika mtandaoni kwa kufuata kiunganishi hiki >> JamiiTalks Debate Application

Mwisho wa kupokea maombi ni Ijumaa tarehe 5 Oktoba 2018 saa 11 jioni.

Karibuni.

Mdahalo uliopita >> "NAFASI ZA MITANDAO YA KIJAMII NCHINI" - Yaliyojiri katika Mdahalo wa Wanachuo New Africa Hotel - JamiiForums
Mbona dotcom tu na sisi BBC (wahenga) nafasi yetu iko wapi?
 
Mkuu,

Una uhuru wa Maoni, hivyo Asante kwa kuchangia. Tuna mipango, mikakati na taratibu zetu ambazo zinatulazimu kufanya hivyo. Ukisoma hoja za Post hizo za awali zilizojibiwa, utaelewa.

Hata hivyo hulazimishwi kuelewa, upo huru kuandaa mdahalo na uendeshe kwa misingi na taratibu utakazozipenda.

Hili la kusema wasomi na wanafunzi wa elimu za juu na pingana nalo na ni ubaguzi kabisa. Siku hizi sayansi na teknolojia imekuwa hata ambao hawajaenda shule wanatumia mitandao iweje wabaguliwe.

Yawezekana huyo ambaye hajaenda darasa akawa na hoja zenye mashiko za kuibadili jamii nzima yenye mkanganyiko juu ya matumizi ya mitandao.

Kamwe huwezi kupima uzito wa pamba na mawe kwa kutizima mwonekano wa nje kw kusema pamba ni nyepesi zaid kuliko mwawe ili hali zote zinau uzito sawa. Zote ziwekwe katika mizani zipimwe kwa usawa, ndivyo hivyo hivyo katika mdahalo huo.

Wote wapewe fursa
 
Mkuu,

Utakuwa haipo katika dunia ya leo ama inawezekana si mpembuzi wa masuala yanayotuzunguka na umeelemea kuangalia siasa ama hoja za Kishabiki zaidi.

Unajua idadi ya watu wanaopoteza maisha sababu ya Mitandao ya Kijamii? Unajua kuna watu wanaoibiwa, rubiniwa na kuathirika vibaya tokana na Mitandao hii?

Inawezekana hujui kwamba Tanzania na nchi nyinyi za Kiafrika tume ‘Leap-Frog’ katika technolojia na hivyo kufanya wahanga wawe wengi kuliko wanufaika. Jamii kutambua hili kunatakiwa kuwe na mazungumzo (si matumizi tu).

Wasomi wetu ina maana mmekosa mada yenye mashiko kabisa!? Hiyo mada ni ya watoto wa sekondary sio kwa level ya university! Badilisheni mada mtapata washiriki wengi. Badala ya kujadili udikteta na hatima yake kwa nchi za Africa Mashariki, mnaongea habari ya face book na Insta??!
 
Wanaogopa kufungiwa maana mwafrika Unafki ni sehemu ya Maisha yake kuongea asichoamini
 
Hili la kusema wasomi na wanafunzi wa elimu za juu na pingana nalo na ni ubaguzi kabisa. Siku hizi sayansi na teknolojia imekuwa hata ambao hawajaenda shule wanatumia mitandao iweje wabaguliwe.

Yawezekana huyo ambaye hajaenda darasa akawa na hoja zenye mashiko za kuibadili jamii nzima yenye mkanganyiko juu ya matumizi ya mitandao.

Kamwe huwezi kupima uzito wa pamba na mawe kwa kutizima mwonekano wa nje kw kusema pamba ni nyepesi zaid kuliko mwawe ili hali zote zinau uzito sawa. Zote ziwekwe katika mizani zipimwe kwa usawa, ndivyo hivyo hivyo katika mdahalo huo.

Wote wapewe fursa
Mkuu nenda shule acha kelelee!!
 
Wasomi wetu ina maana mmekosa mada yenye mashiko kabisa!? Hiyo mada ni ya watoto wa sekondary sio kwa level ya university! Badilisheni mada mtapata washiriki wengi. Badala ya kujadili udikteta na hatima yake kwa nchi za Africa Mashariki, mnaongea habari ya face book na Insta??!

Du wajinga mko wengi sana. Na dalili za udikteta usidhani mpka Uwe Mwenyekiti wa Chadema kukaa kwenye chea bila uchaguzi. Inaanza na Watu kama nyie msioheshimu mipango ya wengine Kisa kujiingiza kwenye maono ya kuambiwa. We ujinga wako usipende kutuaminisha. Tuko Tanzania. Na Tanzania hatuna tatizo La udikteta. Kama kweli unaelewa maana ya udikteta. Watu wanaibiwa sana. Watu wanatukana sana. Pengine we UMo badala ya kufaidika na nia ya kuanzishwa Mtandao. Mitandao ni Hela. Ni fedha. Ni opportunity . Je kwako Watu kupata ujuzi na mbinu za kupata Hela ni ujinga . Ujinga ni huo unapandikizwa nakukufanya uache kutafuta maisha yako. Siasa ndugu yangu waachie wanasiasa wanajua wanachotafuta. Do grow up.
 
....kwa povu hizi ukweli umefika jinga kabisa
 
Naona debates zinarudi nchini kivingine..

Midahalo ya kisomi inasaidia sana kushape fikra za vijana.. Naamini in the long run, itasaidia pia kuwajengea watanzania wote kwa ujumla, uwezo wa kuhoji na kujadili masuala nyeti ya kijamii na kitaifa kwa weledi mkubwa tofauti na ilivyo sasa..

Natamani kuona lengo hili linafanikiwa kwa kasi maana hali ni mbaya sana kusema ukweli..
 
FB_IMG_1538402820288.jpg
 
Sidhani kama kuna tatizo maana hiyo ipo Public, sio kama id's zetu humu, Personaly naona iko safe!
 
Kwani wamekwambia uandike ID yako ya humu ndani mkuu?

Wamesema uwaambie Kama utashiriki.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom