Mdahalo kuhusu hatma ya Tanzania - Katiba na Utawala Bora kutoka Mlimani City Dar es Salaam

Kamanda

Senior Member
Dec 5, 2007
150
176
Idadi ya watu ni kubwa, wanawake kwa wanaume. Wasomi kwa weledi wa kada mbalimbali. Muziki live na mchanganyiko wa mawazo kutoka kwa wachangiaji. Karibuni tuwe pamoja. Kampuni ya Maa Media kwa ufadhili wa Mfuko wa Habari Tanzania (TMF). Karibuni
 
Karibu mdahalo wa wazi unaanza na MC anazungumza kuhusu namna ya kuchangia, muda na mawazo ya wachangiaji, bila kuogopa, lugha zisizofaa wala kumhukumu mtu, bali ukweli, uwazi na zaidi sana mtiririko mzuri wa mawazo ya mchangiaji. Karibuni
 
In the prevelege for those who dont understand Swahili, here is what is going on live from Mlimani City in Dar es Salaam - Maamedia Center invites everyone to take part in the making of the first ever Nchi Yetu TV Show sessions. Towards the making, 10 very pertinent issues have been put across for discussion by the people, and the dialogues will be recorded for the ultimate Nchi Yetu TV Show episodes
 
Live kwenye FB, Jamii Forums, Twitter, blogs. Siyo ghafla imekuwa ikitangazwa mara kadhaa na idadi ya watu waliojitokeza inaonesha ujumbe ulifika sawia. Karibu tuwe pamoja kuchangia mustakabali wa mama yetu Tanzania
 
Mimi sijaelewa kabisa . Hebu kama ni mdahalo serious elezeni hapa kwa lugha inayoeleweka kwa urahisi na watu wote. Mambo ya muhimu tuwe makini ili yasionekane ni ya kitoto. Naomba tujulishwe vema. Mdahalo huo UNAFANYIKIA WAPI, LINI NA SAA NGAPI. Ahsante
 
Namuona Dk. Sengondo Mvungi ameingia hapa na anapewa eneo la kukaa tayari kwa kuanza. Idadi ya watu maarufu yazidi kuongezeka. Karibuni. Muziki wa kuweka mambo sawa wa B-Band ya Banana Zorro umeanza kutumbuiza kidogo.
 
Mambo yameanza hapa, wimbo mzuri unaoitwa nchi yetu ndiyo unafungua sasa na anayeimba ni Banana mwenyewe. Nawaona wahadhili haa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiwa wanaoneshwa mahali pa kukaa
 
Kuna watu humu ndani wanamambo ya kitoto kama vile shule kwao ni sawa na ALLERGY....mmeambiwa usimtukane mtu unatukana...by the way, una PhD ya kkutukana nini mzee utume CV nini???
 
Mada inayoanza ni kuhusu utawala bora na hapa inaoneshwa picha fupi kuhusu ufahamu wa wananchi kuhusu utawala bora. Picha imechukua maoni ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania. Katika picha hiyo, idadi kubwa ya wachangiaji wanaeleza kuwa Tanzania hakuna utawala bora
 
Wanaochangia katika filamu hiyo fupi (documentary) imebeba mchango wa wabunge walihojiwa, wasomi wa vyuo vikuu, wanafunzi na wanachama wa vyama vyote vya siasa, kikiwemo chama tawala, CCM na wote wanaeleza kuwa hakuna utawala bora Tanzania, tena wakieleza kuwa hali imekuwa mbaya katika miaka ya hivi karibuni
 
Mdahalo umeandaliwa na Maa Media Centre, unaongozwa na wanazuoni wa masuala ya siasa, ntakuletea majina ya waongozaji muda mfupi, ujao, kwa kuwa ni live (wanarekodi kwa ajili ya TV) hakuna kukatiza na mahala nilipokaa nipo mbele ya kamera
 
Banana amealikwa kutumbuiza na siyo mchangiaji, ingawa nadhani akipenda anaweza kuchangia. Tusubiri tuone
 
Ieleweke kuwa dhana nzima ya utawala bora unajikita katika uongozi wa kidemokrasia na siyo udikteta, anasema mwongozaji- Salma Amini
 
Wachangiaji wengi wanaeleza kuwepo kwa matabaka, rushwa, ubadhirifu, viongozi wanaoshindwa kuwajibika na wale wanaoshindwa kuwawajibisha kuwa ni vigezo vya kutokuwepo kwa utawala bora
 
Back
Top Bottom