MDAHALO: Kikwete akivunja baraza la mawaziri atathibitisha udhaifu wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MDAHALO: Kikwete akivunja baraza la mawaziri atathibitisha udhaifu wake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Feb 21, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Feb 21, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kumekuwepo na tetesiza uwezekano wa kuvunjwa kwa baraza ka mawaziri wakati wowote kuanzia sasa. Na wapo watu ambao wametoa wito kwa rais kufanya hivyo. Je hoja ya mdahalo huu ni ya kweli au siyo kweli na kwa nini?
   
 2. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  Hata asipovunja Baraza,Kikwete ni dhaifu na ataendelea kuwa dhaifu.Kuvunjavunja Baraza ni udhaifu ulipitiliza..
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Feb 21, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,494
  Trophy Points: 280
  mwacheni kwanza hadi avunje..mkiongea sasa hivi ataacha kulivunja
   
 4. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #4
  Feb 21, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  hUO UTAKUWA UDHAIFU USIO MFANO...LAKINI NI BORA ALIVUNJE ILI IONEKANE ANAHUJUMIWA NA WATENDAJI WAKE KULIKO KUBAKIA NA BARAZA HILI LA SASA.

  bARAZZA LIJALO AWAWEKE HATA WAPINZANI JUKWAANI NADHANI HALI ITAKUWA SHWARI TU
   
 5. N

  NgomaNgumu Senior Member

  #5
  Feb 21, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuvunja baraza la mawaziri ni moja ya maamuzi magumu. Vunja na kila alieshindwa kufanya kazi yake kwa ufanisi asirudi tena
   
 6. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #6
  Feb 21, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  ...sioni tatizo kulivunja ikiwa mawaziri wenyewe hawafanyi inavyopaswa kuwa. Baraza ni dhaifu kwa sasa na hawana maamuzi ya pamoja. Karibu kila waziri ana nia yake binafsi ambazo kimsingi hazina tija kwa taifa,

  Ni kuonyesha udhaifu kulivunja kwa sasa, ila ni mzigo zaidi kuendelea kuwa nalo kama halitendi inavyopaswa kuwa.
   
 7. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #7
  Feb 21, 2012
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kuvunja baraza itakuwa njia sahihi angalau kuja na timu nyingine itakayoleta tija kwa miaka iliyobakia ya utawala wake. na sababu za kufanya hivyo ni wazi zipo kutokana na mambo yaliyojitokeza karibuni,
  -Sakata la madaktari,
  -Sakata la Sitta na Mwakyembe
  Lakini pia sidhani kama kuna ufanisi wa kuendelea na mawaziri ambao dhahiri wameonyesha moja kwa moja kushindwa kutekeleza majukumu yao.
   
 8. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #8
  Feb 21, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  binafsi naona hakuna hata waziri mmoja anayefaa au alipaswa kuwepo katika hili baraza la mawaziri. Ukifuatilia sana utakuta hawana hata kazi za kufanya pale wizarani, kila kitu kinamalizwa na permanent secretary. Nchi za wenzetu kama uingereza hakuna kitu kinaitwa wizara wala waziri ila ni idara. Alivunje au asilivunje udhaifu upo palepale
   
 9. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #9
  Feb 21, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Kikwete ndio nani hapa Tanzania? au mna mzungumzia rais wa NEC na UWT? Who care about Kikwete katika hii nchi? Kikwete is most useless person katika hii dunia, bora hata mwanangu wa 3yrs ana akili timamu kuliko huyo kilaza wenu mnayemwita rais wa waliolala fofo, Wadanganyika na rais wenu mlieteuliwa na NEC pamoja na kampuni ya Mafisadi UWT.
   
 10. only83

  only83 JF-Expert Member

  #10
  Feb 21, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Siamini kama ni kweli kwasababu ya hoja zifuatazo moja,JK ni kati wa viongozi wasioweza kuchukua maamuzi magumu na ya kutikisa nchi namna hiyo,na wengine wanaweza sema mbona aliwezavunja mara ya kwanza? Mara ya kwanza alivunja ili kupunguza nguvu za white hair Pili,sidhani kama chama chake kinaweza kumkubalia kufanya hivyo,maana maamuzi kama haya lazima yapitiwe na washirika wake ambao wamemuweka madarakani Tatu,hawezi kukubali kurudia tena yaliyomkuta 2008 maana hiyo itakuwa ni udhaifu mkubwa sana kwake,ingawaje ata kuliacha hili baraza lake la sasa kufanya kazi ni janga pia.

  Kwa ujumla;sitegemei kuvunjwa kwa baraza la mawaziri kwa sasa,labda mabadiliko madogo ambayo yanaweza fanywa kuwatoa wagonjwa kama Dr Mwakyembe na wengineo.
   
 11. only83

  only83 JF-Expert Member

  #11
  Feb 21, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Cool down mkuu,tuliza mukhari wengi tunakerwa na huyu jamaa,ngoja twende nae tuone mwisho wake.
   
 12. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #12
  Feb 21, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  1. MM great thinker ataangalia wateule wapya na connections zao halafu atachanganya na za kwake then atatoka na jibu moja = weak/strong xx

  2. kuna watu hawatakiwi kurudi kwenye baraza jipya ..6, mwaki etc hawa ni kwa kosa la kuichonganisha serikali na wananchi wake ili nchi isitawalike

  3. vinara wa mbio za uraisi hawatakiwi kurudi barazani maana sasa 2012-2014 mbio ndio zitazidi kupamba moto na wengine piga ua watakuwa wanawahujumu mawaziri wenzao wenye nia kama yao ili kuonesha umma (wapiga kura za maoni) kuwa hawafai. Kwakifupi hakutakuwa na team work kwenye baraza iwapo wanamtandao watarudi, mawaziri wengi watakuwa busy kujijenga binafsi kwaajili ya 2015 na si kuwa busy kwa kazi ya uwaziri.

  4. wapambe wa wenye nia ya 2015 nao hawatakiwi barazani, tunahitaji watu wasio wanamtandao ili wawatumikie wananchi.

  USHAURI WA Narubongo KWA JK
  JK ukiona kila mbunge ni mwanamtandao basi tumia nafasi yako ya kuwateua wabunge kutoka uraiani ili waje wapige kazi ya uwaziri, sasa hivi hata ukiwatosa wanamtandao watabaki wanapiga mihayo tu.! unahitaji kuweka heshima kwa wananchi kwa sasa.

  MWISHO: Narubongo atalipongeza baraza jipya iwapo hayo ya juu yatazingatiwa, vinginevyo hapana ataunga mkono heading ya MM
   
 13. C

  Chintu JF-Expert Member

  #13
  Feb 21, 2012
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 3,402
  Likes Received: 856
  Trophy Points: 280
  Kuna mdahalo mmoja wa wagombea urais mwaka 1995 Mh Mrema aliongea point moja muhimu sana kama unakumbuka. Alisema watamnzania wasifanye utani katika kuchagua Rais, kwa sababu Rais ndiyo dira ya nchi itakavyoendeshwa. Mkichagua mtu wa mzahamzaha hata wezi na mafisadi wanajua kuwa aliyepo pale juu ni mtu wa mizahamizaha tu - hawamwogopi. mkimchagua mtu asiye na utani kuhusu ujambazi, hata majambazi pia yanajua kuwa aliyepo pale juu hana utani na majambazi, na alitoa mfano kuwa kipindi alichokuwa waziri wa mambo ya ndani alikuwa na uwezo wa kuwaamrisha majambazi warudishe silaha na walirudisha kwa sababu walimjua hana mzaha na ujambazi.
  Leo hii Mafisadi wakisikia Dr Slaa anaingia ikulu wala hutahitaji kuwaambia acheni ufisadi, utashangaa tu kila aliyekuwa fisadi anaanza kubehave. Sura ya Rais inabidi iwe na ujumbe kwa waovu wote ndipo nchi itaenda. Watu walishatilia mashaka sura ya Rais wetu tangu anaingia madarakani 2005, alipodokezwa kuwa watanzania wakiisoma sura yako hawaoni ujumbe wowote zaidi ya mizaha akang'aka na kusema wasubiri waone. Tukasubiri kweli,na bahati nzuri wala haikuchukua muda mrefu ikaja EPA si unakumbuka siku alipohutubia bunge kwa masaa matatu na kuhitimisha kwa kusema mafisadi wana haki zao, halafu akawapa muda warudishe walichoiba mwisho October? Sitta akasimama akamuangalia usoni hakummaliza kwa sauti iliyoonyesha wazi alivyombore akamuomba Mheshimiwa hizo sheria si utuletee tukutengenezee maana hiyo ndio kazi yetu kama bunge - Ile hutuba ilizuiliwa kujadiliwa na bunge na kuna tetesi walikataza isichapwe kwenye hansard kuepusha aibu. Kuna mengi yameendelea kutokea baada ya hilo ambapo Rais wetu ameendelea kuonyesha mizaha na udhaifu mkubwa. Mawaziri wanajua hivyo ndio maana wanaiogopa CDM zaidi kuliko hata aliyewateua. Hivi sasa nchi inaongozwa na CDM. Rais anaiogopa CDM, mawaziri pia wanaiogopa CDM kuliko hata aliyewateua maana wanamjua hana noma! Mi nadhani tatizo kubwa tulilonalo waTz ni Rais na wala si mawaziri. Nina imani mawaziri serious (e.g Magufuli) wanapata shida sana kufanya kazi chini ya Rais wetu, tuna Rais ambaye tunajua anavyovipenda tu lakini hatujui anachokichukia (ukiacha kile kigoda cha Mwl Nyerere).
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Feb 21, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Aweza kuvunja baraza bila ya yeye akabakia mbora?
   
 15. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #15
  Feb 21, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  sioni udhaifu kama sheria inamruhusu kufanya hivyo.hawa mawaziri walipewa semina elekezi lakina hawaonekani kumsaidia rais.kama rais ni weak nilitegemea mawaziri na watendaji wawe strong.tukubali asilimia kubwa ya mawaziri ni mbumbumbu wasiowajibika.
   
 16. f

  falesy Senior Member

  #16
  Feb 21, 2012
  Joined: Mar 15, 2006
  Messages: 105
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Chintu uko sahihi kabisa na kumlinganisha SITTA na SLAA ni kumuonea SLAA kwani aliyezuia ile hotuba isijadiliwe ni nani kama siyo SITTA? kwa hiyo yale alisema kutukoga wabongo na Bongo zenye tongotongo (hatuoni)

  kuhusu Magufuli; Huyu ndo hovyo kabisa maana yeye ni mkandamizaji mkubwa wa demokrasia na hasa inapofikia kusema lolote kuhusu CHADEMA. Kumbuka maoni yake dhidi ya Mnyika; Dhidi ya Mbunge wa Ukerewe na dhidi ya CHADEMA kwa ujumla. I declare my interest; Mimi ni mwanchama wa CCM lakini unafiki wa Magufuli na viongozi aina yake dhidi ya demokrasia vinanikera sana. Sijafikiria kuhama CCM wala sidhani kama nitafikiria lakini lazima tujue nchi inaliwa na mijitu michache.

  Kikwete avunje baraza la Mawaziri; thubutu!!! Kuna kiongozi mmoja wa juu ndani ya CCM aliwahi kusema; Ukitaka Kikwete atoe maamuzi manzito basi ni lazima mumshikilie asipate nafasi ya kutoka hadi aamue vile mnataka na ndiyo maana kuvunja secretariet ya kamati kuu ya CCM ililazimu mikutano ya non-stop hadi saa 6 usiku ndipo akaamua kuvunja na hata aliposhauriwa baada ya kuvunja usimrudishe yeyote kati ya wale wa zamani; alipopewa upenyo tu; Aliwarudisha baadhi yao kama Pindi chana na Chiligati.

  Akivunja baraza hili; basi Waziri mkuu atakuwa Lukuvi na huo ndo utakuwa mwisho wa Ujenzi wa Mpanda University; Waziri wa Nishati na madini January Makamba naibu Kafumu Dalai; mambo ya Nje Emanuel Nchimbi naibu Sophia Simba (utani huu); Elimu ya Juu Prof Peter Msolla Naibu...

  Hawezi; Nasema hawezi!!!!!!
   
 17. satellite

  satellite JF-Expert Member

  #17
  Feb 21, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Serikali legelege na rais legelege tu hawezi kufanya maamuzi magumu
   
 18. N

  Ngoiva JF-Expert Member

  #18
  Feb 21, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa hili bora akiri nchi imemshinda, kwa kuonyesha uwajibikaji aachie ngazi. Hakuna anachokifanya zaidi ya kuongeza umasiki kwa wananchi
   
 19. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #19
  Feb 21, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye red mkuu umenena, nafikiri hata Kikwete mwenye atakuwa anajinyea kwenye suruali akisikia Dr.Slaa ametinga Ikulu na ndio utakuwa mwazo wa Mafisadi wote kuelekea Keko, Kikwete na Mkapa wakiwa ndio wa mwanzo kuelekea huko wakifuatiwa na Mafisadi wenzao.
   
 20. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #20
  Feb 21, 2012
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Kwani amevunja mara ngapi,na kuna kipi kipya kilichobadilika baada ya kuvunja,na kuunda upya,hana jipya!daima atakuwa ovyo tu!
   
Loading...