Mdahalo kati ya Freeman Mbowe na Hamad Rashid ITV

kiraia

JF-Expert Member
Nov 20, 2007
1,716
999
Wadau nimepokea email na nawasilisha kwenu kama nilivyopokea.

Wapendwa,
Salamu kwenu nyote na nashukuru kwa jinsi Jukwaa hili linavyojumuisha watu wakabadilishana mawazo juu ya mambo tofauti ya maisha.

Napenda kuchukua nafasi hii, kwa niaba ya Vox Media kuwatangazia kwamba Jumamosi hii, yaanii Novemba 27, 2010, kuanzia saa moja jioni hadi saa tatu usiku, tutakuwa na mdahalo kati ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani aliyemaliza muda wake, Hamad Rashid Mohamed, Mbunge wa Wawi (CUF), kuhusu masuala yahusianayo na kambi hiyo bungeni.

Mdahalo huo utarushwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha ITV (saa moja mpaka tatu usiku). Kwa kuwa kadi zilizopo ni chache, wengi wenu mnashauriwa kuwa kando ya televisheni zenu kwa ajili ya kushuhudia.
Karibuni na ahsanteni.
 
Kuna tetezi ya kuwa mbali na kuwepo mawaziri vivuli watakaoteuliwa na chama kinachounda kammbi rasmi ya upinzani, yaani chadema, kutakuwepo pia mawazili maruhani, watakaoteuliwa kutoka vyama vinginevyo vya upinzani vyenye wabunge. Tofauti na mawaziri vivuli, majina ya mawaziri hao yatabakia kuwa siri lakini yatakuwa yanajulikana kwa uongozi wote wa chama tawala na vyombo vyake. Kutokana na hayo, kauli za mawaziri hao zitapewa umuimu mkubwa na vyombo hivyo kuliko zile za mawaziri vivuli.
 
Hizi siasa zetu jamani! badala upinzani uwe kitu kimoja kupambana na chama tawala kunufaisha maslahi ya wananchi, wanapambana wenyewe kwa wenyewe!Nashindwa ku-imagine jinsi gani baba January anachekelea hili!
 
Utakuwa mdahalo mzuri coz mmoja wao anaweza kuwasilisha mawazo ya chama tawala
 
Sure midahalo kama hii ni muhimu kwa zama hizi za ukweli na uwazi, hili ni fundisho kwa CCM, wanaogopa nidagalo kama mama mkwe, wanajua madhambi na uchafu wao.:whoo:
 
Kuna tetezi ya kuwa mbali na kuwepo mawaziri vivuli watakaoteuliwa na chama kinachounda kammbi rasmi ya upinzani, yaani chadema, kutakuwepo pia mawazili maruhani, watakaoteuliwa kutoka vyama vinginevyo vya upinzani vyenye wabunge. Tofauti na mawaziri vivuli, majina ya mawaziri hao yatabakia kuwa siri lakini yatakuwa yanajulikana kwa uongozi wote wa chama tawala na vyombo vyake. Kutokana na hayo, kauli za mawaziri hao zitapewa umuimu mkubwa na vyombo hivyo kuliko zile za mawaziri vivuli.
nionavyo mimi cuf si chama cha upinzani sasa hivi hawa jamaa ni sesemi b
 
Wadau nimepokea email na nawasilisha kwenu kama nilivyopokea.
Kama imetoka hapa JF na kwa bahati mbaya sijaisoma naomba Mod uiondoe

Wapendwa,
Salamu kwenu nyote na nashukuru kwa jinsi Jukwaa hili linavyojumuisha watu wakabadilishana mawazo juu ya mambo tofauti ya maisha.

Napenda kuchukua nafasi hii, kwa niaba ya Vox Media kuwatangazia kwamba Jumamosi hii, yaanii Novemba 27, 2010, kuanzia saa moja jioni hadi saa tatu usiku, tutakuwa na mdahalo kati ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani aliyemaliza muda wake, Hamad Rashid Mohamed, Mbunge wa Wawi (CUF), kuhusu masuala yahusianayo na kambi hiyo bungeni.

Mdahalo huo utarushwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha ITV (saa moja mpaka tatu usiku). Kwa kuwa kadi zilizopo ni chache, wengi wenu mnashauriwa kuwa kando ya televisheni zenu kwa ajili ya kushuhudia.
Karibuni na ahsanteni.
Kama ni kweli basi hii imeconfirm cuf sio wapinzani tena. Duh yan nashidwa kuelewa watu wa nchi hii kabisa. Sasa hapo mada inakuwa nini mana jamaa wa cuf ni "mpinzani" na Mbowe ni Upinzani. Au ndo mdahalo kat ya wapinzani feki na wapinzani halisi? Somebody help me here wakuu.
Yani wataongelea nini na kupambanisha nini? Hii kwangu haija kaa sawa kabisa.
 
Ndani ya CUF kuna wapenzi wa madaraka na kuna watu hawawezi kukaa bila ya madaraka .Watu wote tegemeo la mageuzi ndani ya CUF wao ni madaraka kwanza ndiyo mfano Hamad Rashid naona hawezi kuishi Bungeni bila ya madaraka au anatimiza ahadi zao na makubaliano ya CCM ndiyo maana vurugu zote hizi .Maalimu kesha pata Ulaji kesha tulia na CUF kwisha kazi maana anatekeleza sera za CCM hawezi kupinga lolote na huku bara wanataka Chadema kuwa kama CUF hapana watuache wao waendelee na kusaka madaraka na kuingia makubaliano na CCM.Tutasikia hiyo weekend wao wana agenda gani .
 
CUF wanataka wawemo kwenye kambi ya upinzani. CADEMA wamebana. Sasa CUF wnakuja na vigezo vya kwanini wao nao wasiwemo kwenye kambi hiyo na CHADEMA wanakuja vigezo kwanini wawe wao peke yao. It will be very Intresting.
 
Back
Top Bottom