MDAHALO: Fatma Karume, Othman Masoud kuitikisa nchi Jumapili

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,278
25,846
Watakuwa wazungumzaji kwenye Kongamano lililoandaliwa na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) litakalozungumzia changamoto za kisheria katika uchaguzi mkuu uliopita. Suala kuu litakuwa kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar. Hapo ndipo patakapowaleta Mawakili Wasomi Fatma Karume na Othman Masoud.

Ukumbi ni Blue Pearl-Ubungo Plaza. Muda ni kuanzia saa nane kamili mchana hadi saa kumi na mbili kamili jioni. Wote mnakaribishwa. Ratiba kamili ni hii:
 
Attachments

  • Ratiba__Kongamano.doc
    338 KB · Views: 99
fatuma karume anafanya kazi nzuri kwa taifa lake ,michango yake inaonekana kwani huwa nasema endapo umesoma ukahitimu basi usomi wako uonekane kwa kubadili jamii iliyokuzunguka ,endapo jamii itabaki kama ilivyo na wasomi wapo usomi wao hauna maana, kwasababu matunda ya usomi wako hayajaonekana.rai yangu ulinzi uimarishwe hapo ubungo plaza .
 
Subiri polisi watatoa tamko muda si mrefu kuwa "HAKUNA KUFANYA KONGAMANO LOLOTE LA KISIASA KWANI WANANCHI WANA MHEMKO WA KISIASA BADO"

Hivyo kwa taarifa za kiintelijensia watazuia hilo kongamano kwani kuna hatari ya ALSHABAB KUVAMIA HAPO.
 
Watakuwa wazungumzaji kwenye Kongamano lililoandaliwa na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) litakalozungumzia changamoto za kisheria katika uchaguzi mkuu uliopita. Suala kuu litakuwa kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar. Hapo ndipo patakapowaleta Mawakili Wasomi Fatma Karume na Othman Masoud.

Ukumbi ni Blue Pearl-Ubungo Plaza. Muda ni kuanzia saa nane kamili mchana hadi saa kumi na mbili kamili jioni. Wote mnakaribishwa. Ratiba kamili ni hii:

Sorry- lakini siioni tarehe ya kongamano - si kwenye post yako wala ratiba
 
Wasomi wetu wawe wanatoa hoja za kuzuia mikwamo ya kisiasa kutokea badala ya kutuonesha umahiri pale matatizo yanapotokea. Mfano tuweke sheria zipi ili kuondoa uwezekano wa wasmamizi wa uchaguzi kutangaza mshindi wamtakae...
sio mpaka hali iwe mbaaya ndo wanaanzisha makongamano yenye chembechembe za uchochezi
 
Watakuwa wazungumzaji kwenye Kongamano lililoandaliwa na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) litakalozungumzia changamoto za kisheria katika uchaguzi mkuu uliopita. Suala kuu litakuwa kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar. Hapo ndipo patakapowaleta Mawakili Wasomi Fatma Karume na Othman Masoud.

Ukumbi ni Blue Pearl-Ubungo Plaza. Muda ni kuanzia saa nane kamili mchana hadi saa kumi na mbili kamili jioni. Wote mnakaribishwa. Ratiba kamili ni hii:
Huo Fatma asicheze ngoma asiyoifahamu.
Ukweli wa familia yake tokea kwa bibi yake utaanikwa hadharani.
 
Wasomi wetu wawe wanatoa hoja za kuzuia mikwamo ya kisiasa kutokea badala ya kutuonesha umahiri pale matatizo yanapotokea. Mfano tuweke sheria zipi ili kuondoa uwezekano wa wasmamizi wa uchaguzi kutangaza mshindi wamtakae...
sio mpaka hali iwe mbaaya ndo wanaanzisha makongamano yenye chembechembe za uchochezi

Bado tuna safari ndefu sana....hao tunaowaita wasomi wanapofika mahala pa kutoa mwelekeo muafaka wa kama haya unayosema wakifika kwa wanasiasa wanaishiwa nguvu, tamaa zinazidi busara, na wanashawishika kuweka pembeni maslahi ya umma. Matokeo yake sheria zinabakia dhaifu, na mambo yanakwenda hivyo hivyo. Aibu tupu!
 
Huo Fatma asicheze ngoma asiyoifahamu.
Ukweli wa familia yake tokea kwa bibi yake utaanikwa hadharani.

Mkuu Maso, inawezekana una mamabo unayoyaelewa wewe kuhusu Bi Fatma na ndio maana ukasema hivyo. Hoja hapa ni je lipo hitaji la kuzungumzia hoja hiyo ya uchaguzi uliofutwa? Kuna uhalisia wa hili...is it relevant? Kama Bi Fatma ana dhamira nyingine basi tupeane mwanga tuelewe sote!
 
About 2 years ago niliandika huu mtandaoni juu ya ubaguzi ulivyo hai Zanzibar.
Wengine walibeza na kuna wazanzibari walibisha kabisa kuwa mi muongo.
Leo jipu limejitokeza hadharani.
Zanzibar ni zaidi ya uijuavyo, huyo Fatma anakazania uchaguzi uliokiukwa kwa vile ana upande wake, na si wa CCM.
Ukichokonoa zaidi kila tamko kutoka visiwani, huwa linatoka upande fulani wa the discriminatory divide.
 
Subiri polisi watatoa tamko muda si mrefu kuwa "HAKUNA KUFANYA KONGAMANO LOLOTE LA KISIASA KWANI WANANCHI WANA MHEMKO WA KISIASA BADO"

Hivyo kwa taarifa za kiintelijensia watazuia hilo kongamano kwani kuna hatari ya ALSHABAB KUVAMIA HAPO.
Hilo ni kongamano la kisheria sio kisiasa. Wanataka watwambie sheria zinasemaje mtu mmoja anapochukua maamuzi binafi katika masuala ya nchi. ITV watuletee moja kwa moja
 
Intelejensia ya kipundupindu haikawii kufanya kazi.By the way Tv gani itakuwa live kwa mtanange?
 
About 2 years ago niliandika huu mtandaoni juu ya ubaguzi ulivyo hai Zanzibar.
Wengine walibeza na kuna wazanzibari walibisha kabisa kuwa mi muongo.
Leo jipu limejitokeza hadharani.
Zanzibar ni zaidi ya uijuavyo, huyo Fatma anakazania uchaguzi uliokiukwa kwa vile ana upande wake, na si wa CCM.
Ukichokonoa zaidi kila tamko kutoka visiwani, huwa linatoka upande fulani wa the discriminatory divide.

Kumbuka maslahi ya taifa Tanzania, na mustakabali wa Zanzibar upo katika utata (''at stake au at risk?")...way forward iwe ni kukabiliana na nguvu, shinikizo na mielemeo yote inayoashiria kupoteza mwelekeo. Simtetei Fatma, lakini ni kwa namna gani tunaweza kuchokoza, kujenga hoja na ikajadiliwa "objectively" na Watanzania wote?
 
Back
Top Bottom