MDAHALO DOHARIA: Shule zisizo na madawati, madarasa na walimu wa kutosha zifungwe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MDAHALO DOHARIA: Shule zisizo na madawati, madarasa na walimu wa kutosha zifungwe?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Feb 29, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Feb 29, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Mzazi unaweza vipi kumpeleka mtoto kwenye shule ambayo unajua kabisa haina madawati, walimu, vyoo, au nyenzo mbalimbali za kufundishia? Na wananchi wanachukuliaje hali hii je shule hizi zifungwe au wananchi wafanye nini kuhakikisha kuwa hawategemeii makampuni kuwagawia michango ya madawati na kuwajengea? Au wanafunzi nao wagome? Je, walimu wanaofanya kazi kwenye mazingira ya aina hii waendelee ilhali wanajua kabisa siyo mazingira bora ya kutolea elimu? Au lengo limegeuka kumpitisha mtoto kwenye eneo linaloitwa "shule" bila kujali sana kama anasoma auanajifunza lolote?

  * Doharia: Sijui neno lina maana gani limenijia tu kichwanihivyo hivyo na sijui hata kama kuna hilo neno!
   
 2. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #2
  Feb 29, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hali ilivyo hivi sasa ni wazi kuwa sirikali haijali. Zile pesa alizo tumia mkuu kwenda Davos na Adis zingeweza kutengeneza madawati mangapi?

  Sirikali haitaki msome ili mpate elimu halafu muwakosoe. Inachotoa ni vyeti vya kumaliza masomo wakati mwenye cheti anabakia mbu mbu mbu.

  Wapi umeona tatizo lina tatuliwa na yule anaeliendeleza? Tutabakia wajinga tukisheherekea magorofa mengi na luninga na simu za mkononi kumbe........
   
 3. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #3
  Feb 29, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Sijui unazungumzia shule zipi maana kama ni za sekondari kila mzazi huchangia dawati mtoto wake anapokuwa amefaulu kwenda kidato cha kwanza. Nakiri kwamba upo upungufu wa vifaa kama vile maabara, vitabu, walimu na vifaa vingine muhimu kwa mazingira halisi ya kutolea elimu hasa katika shule za kata hata hivyo serikali inaendelea kuchukua hatua za vitendo kuondoa upungufu huo... kwa upande wangu naona ni bora shule hizi zisifungwe na kiukweli pamoja na kwamba wanafunzi wengi wanafeli tusisahau kuwa wapo wanaofaulu pia katika shule hizo hizo.
   
 4. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #4
  Feb 29, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Viongozi wa Nchi hii ni wa ajabu sana!
  Kwanza ni vyema tukajikumbusha chanzo cha mfumuko wa shule hizi ili tujue matatizo haya yalisababisahwa na nini. Baada ya Tanzania kufanikiwa katika jitihada zake za kuomba msamaha wa Madeni, waliambiwa fedha hizo (ambazo zilikuwa zilipwe kama madeni) zitumike kusaidia elimu. Zitatumika vipi? Serikali ikaamua kutengeneza mpango mkakati.

  Katika kikao kimoja (kati ya serikali na wadau) ilipendekezwa kuwa fedha hizi zitumike kupanua huduma katika shule za Serikali na Binafsi zilizokuwepo, kujenga shule chache zenye huduma nzuri na nyingine zitumike katika program za kuboresha watoahuduma yaan walimu. Kwa kuwa kilichokuwa kinapewa kipaumbele ni commission na maendeleo ya vitu, basi viongozi waliamua kujenga madarasa nchi nzima na matokeo yake ndio haya tunayoyaona leo ,(hakuna vitendea kazi wala walimu). Kwa tuliobahatika kufika huko kijijini, tumeona mengi. Hali ni mbaya kuliko hizo report tunazosomewa kama mafanikio ya serikali.

  Mimi bado msimamo wangu ni huo hapo juu, nasema zitafutwe shule chache kati ya hizo na ziboreshwe ili vijana wetu wapate huduma bora ya elimu, na hizo nyingine zibadilishwe matumizi kwani madhara yake ni makubwa kuliko faida zake. Moja ya madhara hayo ni chuki inayozijengeka kwa vijana hawa walioko kwenye shule hizi, (matokeo yake mtayaona 2015)
  Naposema zibadilishwe matumizi napendekeza ziwe vyuo vya kilimo au vocational training
   
 5. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #5
  Feb 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Wazo la shule za sekondari kwa kila kata lianzishwa na wananchi wa Njombe miaka ya 1980. Ili kusimamia shule hizo kulianzishwa shirika lililoitwa 'Njombe District Development Trust' kwa kifupi NDDT. Kwa shirika hilo lilihamasisha wazazi kujitolea kujenga shule za sekondari kila kata. Walianza na Tarafa za Igominyi ambako kulikuwa na shule za Uwemba na Kifanya, Njombe mjini kulikuwa na shule ya Mpechi, Wanging'ombe kulikuwa na shule ya Wanging'ombe, Makambako, Mtwango, Makoga n.k. Shule hizo zilijengwa kwa awamu na zilionesha mafanikio makubwa sana. Wananchi na wazazi kwa ujumla walijitolea sana. Nilifanya kazi katika moja ya shule hizi kwa miaka miwili, sikushuhudia upungufu wowote wa madawati. Kulikuwa na changamoto kadhaa hata hivyo zilikabiliwa vilivyo na wahusika. Serikali haikuweka mkono wake zaidi ya kuzipa usajili basi. Ni shule hizi zilizokuja kumpa ujiko mkubwa sana bwana Jackson Makweta kwani kama mbunge alishiriki katika uhamasishaji.
  Kosa kubwa lilikuja kufanywa na wanasiasa ambao walilibeba wazo hili kichwa kichwa na kulifanya kuwa la kitaifa bila matayalisho yoyote. Matokeo yake ni haya madudu tunayoyashuhudia hivi sasa. Kwasababu ya uduni wa elimu inayotolewa katika shule hizi naamini shule nyingi sana zitajifunga zenyewe muda si mrefu, kwani tumeanza kushuhudia baadhi ya shule hizi zimeanza kukosa wanafunzi ama kwa kuwa wanaochaguliwa kwenda huko hawaendi kwa kuwa waliona wenzao waliotangulia walifeli darasa zima!
   
Loading...