Mchungaji wangu ni heri utubu kwani uliyonifanyia yatakupeleka motoni.

Sasa hapo huyo mchumba wako kama angekuwa hakutaki na anamtu toka mwanzo si angekucha kawaida tu??au aliforciwa kuolewa na wewe..

Pole sana mkuu,wapotezee wote..na alichofanya mchungaji si msimamo wa kanisa..
 
Nchi haiwezi kuendelea kama ina watu tena mwanaume zwazwa kama wewe!!! Yaani unapewa bahasha na wewe unaifikisha kama ilivyo unazidiwa na watoto wa primary wanabadilisha matokeo
 
Kama ni kweli sema kanisa unalosali, na taja hilo kanisa lilipo pamoja na huyo mchungaji
 
Kama wiki tatu zilizopita niliandika Uzi ululioelezea namna nilivyopata mchumba wangu kwenye kanisa moja la kisabato na jinsi mchungaji alivyotuandikia barua ili tukampe daktari ili tupime UKIMWI kama maandalizi ya ndoa yetu mimi na huyo mchumba wangu.

Pia nilieleza zaidi kuwa baada ya kupima katika hospital moja inayomilikiwa kanisa la kikatoliki na baadaye tukapewa bahasha yenye majibu ili tukampe mchungaji kwa sharti la kutokuifungua.

Nafikili mnakumbuka kuwa baada ya kumpa mchungaji bahasha ile aliomba wazazi wetu waje na akawaambia eti Mimi nimeathirika na mwenzangu mzima hivyo ndoa hakuna.

KUMBE UKWELI NI KWAMBA:
Mchungaji wangu alinifanyia hujma ili nisiweze kufunga ndoa na binti yule kwa kile kinachoaminika kwamba mchumba wangu yule alikuwa na mahusiano na mtoto wa huyo mchungaji wa kisabato kwa muda mrefu bila mimi kujua.

Na jumamosi iliyopita ndoa yao imetangazwa kanisani huku na mimi nikishuhudia hadharani, imeniuma sana.

Kwa hiyo mchungaji wangu akishirikiana na dokta wa kikatoliki walinifanyia hujma ya kunisingizia nina UKIMWI ili tu kunitenganisha na mchumba wangu ili tu mtoto wa mchungaji aweze kumuoa mchumba wangu huyo.

Hii kitu imenisikitisha sana na nimeamini wachungaji wengi ni feki sana na ni watenda dhambi wakubwa sana.

Baba wa aliyekuwa mchumba wangu amenisimulia kila kitu kilichokuwa kimepangwa na mchungaji huyo. Ni dhambi sana.

Ni bora utubu tu mchungaji umetenda dhambi sana.
Asante wasabato

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom