Mchungaji wangu ni heri utubu kwani uliyonifanyia yatakupeleka motoni.

GRAMAA

JF-Expert Member
Nov 1, 2014
1,155
3,398
Kama wiki tatu zilizopita niliandika Uzi ululioelezea namna nilivyopata mchumba wangu kwenye kanisa moja la kisabato na jinsi mchungaji alivyotuandikia barua ili tukampe daktari ili tupime UKIMWI kama maandalizi ya ndoa yetu mimi na huyo mchumba wangu.

Pia nilieleza zaidi kuwa baada ya kupima katika hospital moja inayomilikiwa kanisa la kikatoliki na baadaye tukapewa bahasha yenye majibu ili tukampe mchungaji kwa sharti la kutokuifungua.

Nafikili mnakumbuka kuwa baada ya kumpa mchungaji bahasha ile aliomba wazazi wetu waje na akawaambia eti Mimi nimeathirika na mwenzangu mzima hivyo ndoa hakuna.

KUMBE UKWELI NI KWAMBA:
Mchungaji wangu alinifanyia hujma ili nisiweze kufunga ndoa na binti yule kwa kile kinachoaminika kwamba mchumba wangu yule alikuwa na mahusiano na mtoto wa huyo mchungaji wa kisabato kwa muda mrefu bila mimi kujua.

Na jumamosi iliyopita ndoa yao imetangazwa kanisani huku na mimi nikishuhudia hadharani, imeniuma sana.

Kwa hiyo mchungaji wangu akishirikiana na dokta wa kikatoliki walinifanyia hujma ya kunisingizia nina UKIMWI ili tu kunitenganisha na mchumba wangu ili tu mtoto wa mchungaji aweze kumuoa mchumba wangu huyo.

Hii kitu imenisikitisha sana na nimeamini wachungaji wengi ni feki sana na ni watenda dhambi wakubwa sana.

Baba wa aliyekuwa mchumba wangu amenisimulia kila kitu kilichokuwa kimepangwa na mchungaji huyo. Ni dhambi sana.

Ni bora utubu tu mchungaji umetenda dhambi sana.
 
katika dini ya kiislaam...huwa tunasisitiza kama watu wamependana na sababu za kuoana zipo...waozeshwe haraka kabisa bila kuchelewa...kuepusha fitna kama hizo...(na fitna ndio hiyo)...

Sio kwamba uislaam haujali afya...lakini hata kama mkipima...nyie husika pekee yenu hayo majibu ndio yanawahusu...na ni makubaliano yenu wenyewe kama mmoja wapo ameathirika...lakini dini hairuhusu mtu kujiingiza kwenye shari mwenyewe...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KATIKA DINI YA KIISLAAM...HUWA TUNASISITIZA KAMA WATU WAMEPENDANA NA SABABU ZA KUOANA ZIPO...WAOZESHWE HARAKA KABISA BILA KUCHELEWA...KUEPUSHA FITNA KAMA HIZO...(na fitna ndio hiyo)...

SIO KWAMBA UISLAAM HAUJALI AFYA...LAKINI HATA KAMA MKIPIMA...NYIE HUSIKA PEKEE YENU HAYO MAJIBU NDIO YANAWAHUSU...NA NI MAKUBALIANO YENU WENYEWE KAMA MMOJA WAPO AMEATHIRIKA...LAKINI DINI HAIRUHUSU MTU KUJIINGIZA KWENYE SHARI MWENYEWE...

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbuka kwenye uislam kuna fursa ya kuoa mke wa pili. Hata kama uliboronga waweza kuoa tena.
Kwenye ukristo ndoa ni moja, hivyo ni vyema kuchunguza usije juta maisha yako yote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya ndo matokeo ya kushikiliwa akili na mchungaji ama padre ona sasa mke umekosa ila shukuru dunia kwa kuwa hujamuoa huyo binti
 
KATIKA DINI YA KIISLAAM...HUWA TUNASISITIZA KAMA WATU WAMEPENDANA NA SABABU ZA KUOANA ZIPO...WAOZESHWE HARAKA KABISA BILA KUCHELEWA...KUEPUSHA FITNA KAMA HIZO...(na fitna ndio hiyo)...

SIO KWAMBA UISLAAM HAUJALI AFYA...LAKINI HATA KAMA MKIPIMA...NYIE HUSIKA PEKEE YENU HAYO MAJIBU NDIO YANAWAHUSU...NA NI MAKUBALIANO YENU WENYEWE KAMA MMOJA WAPO AMEATHIRIKA...LAKINI DINI HAIRUHUSU MTU KUJIINGIZA KWENYE SHARI MWENYEWE...

Sent using Jamii Forums mobile app

Kawahiyo kama Binti wa kiislamu amempenda kijana wa kikristo anaruhusiwa kuolewa? Yaani kuwa mkristo?
 
Huyo bora ameolewa na aliyekuwa anampenda kwasababu kama angelasimishwa kuwa mkeo nakuhakikishia angezaa watoto wa yule baba na ndoa ingekusumbua sana
 
Hafu wao kutoa talaka nikuandika tu kikaratasi kwishney mwezi.mtukufu unaoa ukiisha talaka. Ndoa ya Kikristo mpaka mmoja afe
Kumbuka kwenye uislam kuna fursa ya kuoa mke wa pili. Hata kama uliboronga waweza kuoa tena.
Kwenye ukristo ndoa ni moja, hivyo ni vyema kuchunguza usije juta maisha yako yote.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom