Mchungaji wa loliondo ametumwa na Mungu yupi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchungaji wa loliondo ametumwa na Mungu yupi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Foreina, Mar 11, 2011.

 1. F

  Foreina Member

  #1
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Sipingi na wala sitapinga wagonjwa kumiminika kwenda Loliondo kupata dawa ya magonjwa sugu inayotolewa na Mch. Mstaafu Ambilikile. Lakini kama anayosema ni kweli basi Mungu aliyempa uwezo huo atakuwa ni Mungu ambaye mm simuabudu. Tujiulize ni Mungu gani atampa mtu kuponya watu na kumzuia mtu huyo kuitoa dawa hiyo nje ya mazingira yale aliyopo? Mungu wa Mch. Mwasapile ni mchoyo kwa sababu kulazimisha dawa hiyo itolewe eneo moja tu ni uchoyo na upendeleo. Najiuliza wagonjwa mahututi walio kule Mtwara wataweza kusafiri mpaka Loliondo kupata hiyo dawa. Uchoyo mwingine wa Mungu wa Mwasapile ni kwamba kama dawa yake haiwezi kutolewa na mtu mwingine then Hospitali zetu za kule Songea haziwezi kunufaika nayo. Je mchungaji akipatwa na umauti sasa ni nani atatibu badala yake kama ni yeye tu anaruhusiwa na huyo Mungu wake kutibu? Bado Yesu alipewa uwezo wa kuponya lakini alikuwa anaweza kutoa uponyaji popote duniani? Nahitimisha kwa kusema Mch. Mwasapile ni mungu-mtu na anatumia matatizo ya binadamu vibaya na naapa kuwa Mungu wa Mchungaji huyu siwezi kumuabudu.
   
 2. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Wewe ni dhehebu gani: waislam huelekea kibra, huhiji macca- mji mtakatifu. Taja dini yako, nitarudi baadae.
   
 3. Higash

  Higash JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Nakubaliana na wewe kua humkubali mungu wa mwasapile kwani miungu inatofautiana, kwani hujui hata mungu wa waislam na wakristo ni tofauti kabisa? Hivyo pia na wahindu na wamizimu, so muache mchungaji atoe dawa wenye imani watapona wewe baki na mungu wako haitadhuru chochote.
   
 4. TheChoji

  TheChoji JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2011
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 672
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  Mi sijakuelewa. We ulitaka huyu mzee awe anazunguka nchi nzima? Au ulitaka kila kata iwe na mchungaji mwenye uwezo wa kuponya? Kabla huyu mzee hajaanza kutoa dawa, wagonjwa mahututi wa mtwara walikua wanaenda wapi? Mi nadhani tushukuru walau tumepata huyo mmoja, akifa Mungu atainua mtu mwingine.
   
 5. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #5
  Mar 11, 2011
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  mod anzisha JUKWAA LA LOLIONDO thread za babu zimekuwa nyingi mno!
   
 6. gmosha48

  gmosha48 JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,956
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Pole ndugu. Mambo ya Mungu ni Magumu kweli kuelewa. Kwanza unatakiwa kuamini, halafu kuelewa kufuate baadaye! Na utaelewa tu, kama Munggu mwenyewe atakupa hiyo neema ya kuelewa.
   
 7. Ba Martha

  Ba Martha JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwani Jesus au mtume Muhamad enzi zao walizunguka dunia nzima....?watu wote na makabila yote duniani walipata huduma zao?..Acha kukurupuka wewe..:ballchain:
   
 8. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Aisee nimecheka mno.
  Itabidi hilo jukwaa la loliondo likianzishwa pia jukwaa la maandamano nalo lipewe nafasi.
   
 9. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #9
  Mar 11, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Ndiyo maelekezo aliyo pewa! Na amemtii mungu. Labda mungu anamakusudi na loliondo maana kuna mambo mengi but maendeleo yake duni kabisa.
  Mungu wa mchungaji ni yule yule aliye amua kuwakomboa wana wa izreel kutoka utumwani.
  Leo neema kasikia kilio cha wa TZ maana hawana pesa za kwenda india na soth africa kutibiwa.
   
 10. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #10
  Mar 11, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Tukale mkate wa uziimaa na damu ya uzimaaaa ya uzimaaaa
  TUKANYWE KIKOMBEEEE CHA DAWA YA UZIMA CHA BABU CHA UZIMAAAAAA!!!!
  Doubting Thomases are everywhere but JESUS NEBER SAID GOODBYE, BY HIS BLOOD YOU WILL BE REDEEM TO LIFE AGAIN!!!!!!
   
 11. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #11
  Mar 11, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Baada ya Mtume muhamad S.A.W nani alichukua nafasi yake? Baada ya Yesu Kristu nani alichukua nafasi yake? Maajabu na miujiza ya Yesu mbona iliwafikia hata wasiohudhuria mikutano yake ila wenye imani? Nionavyo, Mungu anaweza kutumia kitu kinyonge kuonesha njia! Na baada ya hapo itatokea njia njingine! Muhimu kwa walioamini na kupona wabadili njia ya maisha yao kwa mfano kupunguza unywaji uliopitiliza na kwa ugonjwa wetu huu tupunguze kuchenga! Salaam
   
 12. M

  Mary Chuwa Senior Member

  #12
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mungu wa Mchungaji ni Mungu aliye HAI,anaishi hata sasa na hata milele,endelea kumwabudu Mungu wako ambaye sijui ni wa herufi kubwa ama ndogo maana hujakatazwa.
  Yesu alipaka tope kwenye macho ya kipofu na akaona,alifanya mengi tu,kama ingekuwa hivyo tuliopo Tanzania tusingemwamini kwani kipindi chake hakufika Tanzania.
  Sasa hivi watu wengi wamebadilika wanaweza kuchakachua dawa hiyo,au kuifanya biashara na kuwaumiza wengi,hivyo kulitunza hilo Mungu akamwonesha jinsi ya kufanya pia ,maana Mungu ninayemsoma kwenye Biblia na kumwamini hufanya njia pasipokuwa na njia.
   
 13. K

  Kenge (Eng) JF-Expert Member

  #13
  Mar 11, 2011
  Joined: Dec 7, 2006
  Messages: 502
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Sio lazima ila Mungu wa Babu ndo huyo huyo Mungu wa Ibrahim, Yakobo, Israel, nk.
   
 14. J

  Japhet Mosi JF-Expert Member

  #14
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 207
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naamini kuwa mambo ya Mungu wa Mchungaji wa Loliondo tumwachie yeye na wagonjwa na waumini wake wala mtu yeyote au Serikali ilimwingilie iwapo hakuna uvunjifu wa amani unaojitokeza. Hata Paulo hakuhubiri Israel bali kwa Mataifa ya Mediterrania wala hakufika Uingereza ila King James ndiye alituma watu waende kuandika bible
   
 15. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #15
  Mar 11, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Ni wengi tu huja kwa jina la kutumwa na Mungu!! na huwapata wawapatao... naogopa sana kusema ama kufananisha na Kibwetere, bado ni mapema mno, wakati utakapofika na imani zikawapunguka wale walioamini sasa ndipo itajulikana! Ila kwa sasa wacheni niwe TOMASO! maana wengi wa walioenda kwa babu wanagoma kupimwa ili kuthibitishwa afya zao je ni KWANINI?
   
 16. N

  Nanu JF-Expert Member

  #16
  Mar 11, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu Foreina,
  Wewe ukisema Mungu gani huyo anayempa mtu masharti atoe dawa sehemu moja au yeye mwenyewe tu na ukiweka reference yako Tanzania tu, je wale walio nje ya Watanzania (Wazambia, Wakenya, Waganda, n.k.) ambao sasa hivi wamefurika kwa babu watasemaje? Si nao watasema huyu si Mungu wetu kwamba kwanini dawa hiyo ipatikane Tanzania tu? Mambo ya maono na imani nadhani unahitaji zaidi hekima ya Kimungu uweze kuelewa. Labda Mungu alitaka kusikia pia Loliondo watu walimonyimwa ardhi yao na kupewa Waarabu, Mungu alitaka Loliondo kuwepo na barabara nzuri, Mungu alitaka Loliondo kuwepo na nyumba nzuri ya ibada, hospitali nzuri, shule nzuri, mawasiliano mazuri ya simu, n.k. Sasa bila dawa kutolewa Loliondo tu, je hayo yote yatafanyika vipi? Dawa asipoitoa Mchungaji peke yake, je utazuia vipi akina "babu" feki wasianza kujinufaisha isivyo?
  Kuna mengi ya kuangalia na kujiuliza: kwanini loliondo ipo ngorongoro, kwanini caldera iko ngorongoro, kwanini Kilimanjaro iko Tanzania na mkoa wa Kilimanjaro na ukihitaji kupanda lazima ufike Tanzania? Je hayo yote hayakufanywa kwa Nguvu na Mapenzi ya Mungu?
  Kila kitu na maana yake toka kwa Mungu!! Kingine wala huhitaji kwenda huko kama ni mbali kwako, maana sidhani kama ni mbali zaidi ya India tunakopeleka watu kila siku, au ni mbali kuliko Nigeria kwa TB Joshua tunakopeleka watu kila wakati. Hata mtua anayeishi Mtwara atauliza kwanini serikali imeweka hospitali kubwa ya Taifa -Dar es Salaam? (na hii ni ya wanadamu wanaofikiri kama mimi nawewe). sasa tujiulize kwanza mengi ya kibinadamu halafu baadaye tuyatafakari ya Mungu.
   
 17. K

  Kashaija JF-Expert Member

  #17
  Mar 11, 2011
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ulitaka uwezo huo apewe Sheh Yahaya ndo uamini? Nenda kanywe dawa, achana na imani zisizo na tija.
   
 18. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #18
  Mar 11, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  mnnnnh i will be back sooon mana nikimjibu huyu na siredi yake hii ya kipuuuzi naeza nkakufuru na kwaresma hiii.................
   
 19. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #19
  Mar 11, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Ukiwa huna nauli ya kukufikisha omba hata msaada, tuondole ujinga wako hapa
   
 20. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #20
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Ni mtazamo tu!
   
Loading...