Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,175
Mchungaji Rwakatare amenakiliwa na gazeti la Uhuru linalomilikiwa na CCM akirejea kauli yenye utata ya kuwa JK ni chaguo la Mungu..........kauli hii ni tata ukizingatia upo ushahidi wa ya kuwa NEC haikufuata katiba ya JMT katika kumtangaza JK kuwa ni Raisi wetu..........Ibara ya Na. 41(5) inayoitaka NEC kufuata taratibu za sheria ya uchaguzi haikufuatwa.................................swali kwa kada wa CCM ambaye amejibanza kwenye viti maalumu ni je hivi Mungu anachagua watu ambao wanawadhulumu wapigakura haki yao ya kimsingi ya kuchagua viongozi wawatakao?
Kwa lugha nyingine, je Mwenyezi Mungu anaafiki dhuluma kwenye jamii............huyo ni Mungu wa wapi huyo? Na Mchungaji Rwakatare alikutana lini na Mungu kama siyo anajikomba kwa JK kwa kumkashifu Mwenyezi Mungu pale ambapo anapomwingizia maneno kinywani mwake ambayo hakuyasema.............
Ushauri wangu kwa Rwakatare..........mpe Kaisari yaliyo yake lakini hakikisha kwanza unampa Mwenyezi Mungu yaliyo yake na haya elezea ukweli kuwa ulijitungia..........