Mchungaji Getrude Rwakatare amrithi marehemu Salome Mbatia

Mmmhhhhh!!!! mimi sijui.

NInachojua mimi huyu mama katuamsha Watanzania kwenye mambo ya shule. Ule ujinga wa kupeleka watoto wadogo Kenya na Uganda sasa
umeisha kwasehemu kubwa huyu mama kachangia kwa kuanzisha shule zake ambazo zina quality ya kutosha. Katoa ajira kwa Watanzania na si ajabu analipa kodi ya kutosha. Hivyo ndivyo vichwa tunavyotaka Tanzania na wala sio wale wajinga waliojaa kila sehemu Tanzania wanaokumbatia wageni kwa cost ya Watanzania.

Mimi ninamsifu kwa hilo maana nina uhakika nalo, sina uhakika na hayo ya madawa ya kulevya.

Sitaki kuongea sana juu ya yeye kuingia kwenye siasa wala habari za madawa ya kulevya maana sina uhakika n a lolote. Ninachojua ni kwamba kweli kawasaidia watanzania kuinua elimu (actually english medium na si elimu in its general term) ambayo watu wengi walikuwa wanaifata kenya na ug. Ila napinga hilo la ajira coz most of waajiwa wake ni wakenya na waganda, anayebisha akachunguze. wabongo wachache na hiki mi kinaniuzi sana.
 
Mtajadili kila kitu lakini mama mchungaji ndio keshapewa nafasi hiyo bila kutoa jasho. Hata mseme nini ukweli halisi hauwezi kubadilika. hayo ndio maisha bora kwa kila mtanzania tajiri atendelea kuwa tajiri na masikini ataendelea kuwa masikini.

Muda si mrefu mtasikia na Kakobe naye ndani ya CCM.
 
kodi halipi kajificha ktk kivuli cha dini...

shule nyingi za English Medium zimeajiri watu wa Nje ya tanzania..sijui wabongo wangapi wana kazi UG an KE
 
Mchungaji Rwakatale ni binadamu kama wewe,ana dini pia ni mwananchi anayetakiwa kutoa mawazo ya namna ya kuiendeleza nchi yetu kama wananchi wengine. Wachungaji si miungu ni watu.

Akina Daudi walikuwa ni wafalme na pia walikuwa viongozi wakuu wa Dini. Akina Musa waliongoza Taifa la Israel na pia walikuwa viongozi wakuu wa dini. Tatizo liko wapi? Tutashangaa iwapo tutaona kiongozi wa Dini anajiunga na ujambazi, anatoa rushwa,anakuwa na upendeleo, anakuwa na ukabila nk. Lakina siasa ni sehemu ya uongozi tunahitaji viongozi wa namna hii labda watakemea kwa nguvu zote rushwa ambayo kwa sasa inaonekana kuota mizizi kabisa.

Ninatamani siku moja nisikie Shekh Mkuu au kadinali Pengo au akina Kakobe moja wapo anakuwa Waziri mkuu au rais kabisa, ili tuone uongozi wao nakuwaje hawa watu ambao tunadhani wanakemea maovu kwa nguvu zote! Kutokana na hilo mwache Mchungaji Rwakatale awe mbunge!.
 
Mimi sina tatizo sana na uteuzi wa Dr. Rwakatare kama mtanzania wa kawida!! tatizo langu ni uteuzo wa mchungaji kwenye siasa za tz! si imeandikwa kwenye vitabu vitakatifu ambavyo mchungaji huyu huvihubiri kwamba ''hakuna awezaye kutumika mabwana wawili, kwa maana atamchukia yule na kumpenda huyu!! ukiacha hilo, huyu mtu ana uwezo ni tajiri wa kutupwa....kwa nini kakuwa achia kina mama wengine nafasi hiyo...kama anataka kila mtu anyanyuliwe kama anavyohubiri kila siku?
 
Ni kweli anajitahidi kuinua elimu lakin la ajira nakataa, wafanyakazi wake wengi ni Wakenya.

Mbona nasikia hizo shule sio zake? Nisaidieni kwa hili ukweli uko wapi?
 
Jamani sisi waumini wa kanisa la Dr. Rev. Rwakatare tunasijisikia vibaya mnavyoandika maneno mazito kuhusu mchungaji wa Mungu... Mshindwe kwa jina la...
 
Mtajadili kila kitu lakini mama mchungaji ndio keshapewa nafasi hiyo bila kutoa jasho. Hata mseme nini ukweli halisi hauwezi kubadilika. hayo ndio maisha bora kwa kila mtanzania tajiri atendelea kuwa tajiri na masikini ataendelea kuwa masikini.

Muda si mrefu mtasikia na Kakobe naye ndani ya CCM.

Kweli kabisa Sanda Matuta,

Mama Rwakatare kwani yeye malaika bwana asiingie kwenye ufisadi.
Rafiki yangu mmoja amerudi hapa toka bongo anasema kuwa mtaani siasa ndani ya ccm ni ufisadi. Yaani mtu akiingia kwenye siasa za ccm anatumia neno kuingia kwenye ufisadi.

Rwakatare wewe kula nchi mama, huwezi kukaa pembeni wakati watu wote wakitajirika ndani ya siasa. Haijalishi kama una pesa kiasi gani kwa sasa, mbona karamagi ni tajiri lakini bado amekula 10 percent za migodi!

Ingia kwenye ufisadi ili nawewe utajirike. Sahau kuhusu dini na uadilifu maana hivyo vilimpeleka Nyerere kaburini akiwa kapuku wa kutupwa!
 
Kilitime Wewe Nahisi Ni Mshirika C Muumini,, muumini Gani Umeshindwa Kumalizia Kwa Jina La Yesu,, hata Kilitime Jina Nalo,,

Haya Ubarikiwe Kwa Hili Mungu Huwafukuza Kwa Njia Nyingi Naona Wanaoendelea Kuandika Hivi Sasa Umeme Umezmika Kwao Wanashidwa Kujibu Bwanayesu Shusha Nguvu Zako Kwakila Mmoja Akujue Wewe Ni Mungu
 
Mshindwe Kwajina La Yesu Jamani Biblia Inasema Pamoja Na Kuwaita Mafisisadi Bado Tuheshimu Mmamlaka Ya Nchi,,sasa Kama Mungu Amemteua Mama Rwakatare Kwa Ajili Yenu Basi Naomba Tumheshimu Kama Biblia Isemavyo Ndio Hivyo Ashashika Mamlaka Tena
 
duh hii kali, mzee umenikosha
 
Sitaki kuongea sana juu ya yeye kuingia kwenye siasa wala habari za madawa ya kulevya maana sina uhakika n a lolote. Ninachojua ni kwamba kweli kawasaidia watanzania kuinua elimu (actually english medium na si elimu in its general term) ambayo watu wengi walikuwa wanaifata kenya na ug. Ila napinga hilo la ajira coz most of waajiwa wake ni wakenya na waganda, anayebisha akachunguze. wabongo wachache na hiki mi kinaniuzi sana.
Judy,

Asante kwa maelezo yako kuhusu ajira kwenye shule za huyu mama. Hilo ni tatizo la nchi nzima, ni tatizo la sheria zetu pia.

Ninaamini taratibu Watanzania wataanza kuwa na uwezo wa lugha wa kupambana na Wakenya kwenye baadhi ya kazi. Kwa kuanzisha tu hizo shule kwa vyovyote kuna faida kwa Watanzania, hata kama baadhi yao wanapata kazi za kufagia.

Mimi naamini ukombozi wa Mtanzania utatokana na uchumi wetu kuwa na uwezo wa kuajiri watu wetu wengi. Ndio maana naona huyu mama huenda kajitahidi kuliko wengi wetu hata kama ana mapungufu mengi kama tulivyo Watanzania wengi. Angalau kawafanya Watanzania
waelewe kwamba hata wao wanaweza kuanzisha shule na zikawa za maana, hawahitaji kupeleka watoto wao Kenya au Uganda kwa ajili ya kufuata Kiingereza tu.

Ni bora kuwa na akina Mama Rwakatare 100 kuliko kuwa kutokuwa nao.

Inasikitisha sana unapoona vijana mitaani ambao hawajala wala hakuna dalili ya kwamba watakula karibuni.
 
Mshindwe Kwajina La Yesu Jamani Biblia Inasema Pamoja Na Kuwaita Mafisisadi Bado Tuheshimu Mmamlaka Ya Nchi,,sasa Kama Mungu Amemteua Mama Rwakatare Kwa Ajili Yenu Basi Naomba Tumheshimu Kama Biblia Isemavyo Ndio Hivyo Ashashika Mamlaka Tena

mhh huyu yesu akiingia hadi kwenye ufisadi basi dunia hii haina matumaini tena.

Bila kumhusisha mama Rwakatare na dini yoyote ile, nampongeza kwa uamuzi wake wa kuingia kwenye ufisadi. Hii nchi ni yake na yeye inabidi aungane na matajiri wenzake kina Karamagi kuila na kuitafuna vizuri. Yeye ni binadamu kama mimi na hivyo kama ana nafasi ya kufanya ufisadi kwa nini akatae?

Go Rwakatare, nchi yote yako hiyo, wenzako wanauza maeneo ya kanda ya ziwa kwa wazungu, inabidi wewe utafute eneo lakuuuza haraka sana kabla hujakosa pa kuuza!
 
Huyu mama mafaili yake ya jinsi alivyopata zile pesa basi itabidi hii thread ihamishwe au itafungwa kwani tutambiwa kuwa tunaingilia PRIVATE LIFE yake ndio maana kama mna moyo basi tusubiri aapishwe kisha hapo ndio tutafungua Pandoras box

Sina haja ya kusema mengi sana lakini naweza kusema kuwa si kweli alianzia kwenye BIMBWI bali huyu yeye aliwahi tuu na mamabo yake ya NGO in 1989-1990 ambako alikuwa kipewa mitumba na makanisa ya wainjilisti like CHICAGO, USA.

Na katika kipindi hicho hico aliachana na MUMEWE ambaye kwa kweli alikuwa ni mzinzi tuuu(hilo simtetei yule mzee) lakini huyu mama kitu kilichomuinua ni GENOCIDE IN RWANDA na hapa ndipo itabidi tuingie deep na uhusiano wake na MOSHI MAJUNGU,ZILE INTL SCHOOLS ZAKE,dereva wake etc

kuna mengi sana ya kusema hapa na kama sikosei MWANAKIJIJI anamjua sana huyu mama ila najua kuwa hii ES atakuwa hana data nayo

Tusubiri aapishwe kisha ndio tutaanza kumchambua huyu Mchungaji turned Mwanasiasa
 
all in all ameshateuliwa kuwa mbunge and we will see her sworn in so nothing to do against. But only one thing i know ni kwamba mwisho wao umefika hata wakidandia viongozi wa dini bado watakwenda na maji tu.

Tuelimishane namna ya kupiga kura bora sio bora kura. Na kuanzia sasa watu waanze kuwa makini na hizi teuzi teuzi maana sidhani kama zina manufaa sana kwa kuwa walengwa ni wenye nazo na watu maarufu. Je hakuna mlalahoi mwenye busara ya kuongoza? au mali ndicho kigezo cha busara ya mtu???
 
mhh huyu yesu akiingia hadi kwenye ufisadi basi dunia hii haina matumaini tena.

Bila kumhusisha mama Rwakatare na dini yoyote ile, nampongeza kwa uamuzi wake wa kuingia kwenye ufisadi. Hii nchi ni yake na yeye inabidi aungane na matajiri wenzake kina Karamagi kuila na kuitafuna vizuri. Yeye ni binadamu kama mimi na hivyo kama ana nafasi ya kufanya ufisadi kwa nini akatae?

Go Rwakatare, nchi yote yako hiyo, wenzako wanauza maeneo ya kanda ya ziwa kwa wazungu, inabidi wewe utafute eneo lakuuuza haraka sana kabla hujakosa pa kuuza!

Mwafrika wa Kike,

Kwahiyo nikiukwaa ubunge 2010 kupitia CCM utaniandika hivyo hivyo?

Ufisadi ni mtu wala sio chama, chama kinaweza tu kutengeneza mazingira ya mafisadi kuneemeka kama mguu mchafu unavyoneemsha funza.

CCM ina watu wengi tu ambao hawana hata chembe ya ufisadi, inabidi muache kuwaweka wote pamoja au ndio samaki mmoja akioza wote wameoza? Kama ni hivyo basi kwa mazingira ya TZ wananchi wote tumeoza.
 
Mtanzania,

waulize walioko bongo sasa hivi wakuambie, nina video clip inaonyesha baadhi ya makonda wa mabasi yaendeyo dodoma wakipaita ufisadi.

.... haya waendao morogoro hadi ufisadi.....

Kuna clip ya video ya dreva tax wa dodoma wakipaita makao makuu ya ccm - ufisadi. Nilicheka juzi wakati nikiongea na cousin yangu kwenye simu (ndiye amenitumia hizo clips) akaniambia kuwa hata yeye anataka kuingia kwenye ufisadi. Nilivyomuuliza ana maana gani, akajibu kuwa kuingia kwenye siasa za ccm sasa hivi ni kuingia kwenye ufisadi.

Ufisadi na siasa karibu yatakuwa maneno yenye matumizi sawa. Waulize walioko bongo wakuambie hili. Hata kwenye treni la mkoani kuna watu kibao wanaiita dodoma ufisadi. Ninajaribu kuweka hizi clips pamoja na naongeza quality yake na ikiwa tayari kuna siku nitaziweka hapa.

Ukiingia kwenye ubunge 2010 ni kwamba umeingia kwenye ufisadi. WE jiandae tu mwenzangu!
 
mhh huyu yesu akiingia hadi kwenye ufisadi basi dunia hii haina matumaini tena.

Bila kumhusisha mama Rwakatare na dini yoyote ile, nampongeza kwa uamuzi wake wa kuingia kwenye ufisadi. Hii nchi ni yake na yeye inabidi aungane na matajiri wenzake kina Karamagi kuila na kuitafuna vizuri. Yeye ni binadamu kama mimi na hivyo kama ana nafasi ya kufanya ufisadi kwa nini akatae?

Go Rwakatare, nchi yote yako hiyo, wenzako wanauza maeneo ya kanda ya ziwa kwa wazungu, inabidi wewe utafute eneo lakuuuza haraka sana kabla hujakosa pa kuuza!

Nakuunga mkono Mwa-wa-kike
Tena imesemwa kwamba msifungwe nira na wasioamini, tokeni mkajitenge nao. Mnakumbuka kifo cha Yohana Mbatizaji?? Ni kwa kuwa alisimamia kweli dhidi ya mtawala, ja mama huyu alishawahi kusema ukweli wowote au kuusimamia?? i mean sijamsikia akikemea rushwa wala ufisadi, sana sana anahubiri kuhusu maisha bora na namna ufahari bila kuangalia upande wa pili. Ahubiri kuhusu kuchuma mali kwa hila wala nini....
Ooops nisije nikadhibitiwa bureee.. acha nifunge bakuli langu maana nikisema sana nitaambiwa naingilia praiveti za watu.

Ila mjue kuwa watu wengine wanatumia dini kama kichaka cha hulka na matamanio yao. Ili uwe mtu wa Mungu ni lazma uikane nafsi yako na uuze vyote ulivyo navyo kisha umfuate mungu.

eeeh mbona sinyamazi tuu...?

Pia angalieni sana siku za mwishi watatokea manabii wengi wa uongo wakisema Kristo yupo huku na watatokea hata makristo wengi ila msiwaamini maana yaacheni magugu na ngano vikue pamoja na mwisho magugu yatang'olewa na kutupwa motoni katika lile ziwa liwakalo moto wa kiberiti usiozimika....

Nikiendelea kusema najiua....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom