Mchungaji Peter: Wanawake wanaotafuta wachumba wenye mafanikio wana safari ndefu katika maisha

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Leo wakati nimefungulia redio kuna mchungaji alikuwa anafundisha maswala ya mke mwema na mume mwema anaitwa Mchungaji Peter.

Moja kati ya vitu alivyovizungumza upande wa wadada ya kwamba mwanadada yeyote anaetafuta mchumba au mume ambae tayari ana mafanikio yaani ana nyumba, mali na magari ana SAFARI NDEFU katika maisha yake ya sasa na baadae uko anapoelekea.

Aliendelea kwa kusema ukiona mwanaume yeyote tayari ana mafanikio ya kumiliki mali na vitu vyote unavyomuona navyo kabla ya kumiliki hizo mali kipindi akiwa hajamiliki hizo mali tayari alishakuwa na mchumba wake ambae alimsapoti mpaka kufikia hatua hiyo hivyo mwanaume huyo anajua alipoanzia na alipotokea.

Aliendelea kwa kusema mwanadada yeyote ambae hadi sasa anasubiri mchumba ambae tayari ana mafanikio atambue ya kwamba SAFARI yake ni ndefu sana na mwisho wa siku atajikuta amefika sehemu ambayo hajaitambua yupo wapi na amefikaje huko alipo.

Hiyo ni kwa kifupi hayo ni maneno ya mchungaji sijui mnayazungumziaje.
 
Nimemshikia mwenye kiti chake!

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Nchi nyingi za africa mafanikio ni safari ndefu inayohitaji juhudi na uvumilivu...

Kwenye hiyo safari utakumbana na mengi na wengi pia.. Ila kuna ambao watakosimama na wewe mpaka utakapofika juu...

Mwanamke yoyote atakayekuja au kujitokeza kipindi tayari upo juu, ajue tu kuna watu wamesimama na wewe mpaka hapo ulipofikia...



Cc: mahondaw
 
Tatizo la kutumia r badala ya l na l badala ya r nadhani linatokana sana na mazingira alikotokea mhusika. Makabila mengine tuvumiliane tu maana hakuna namna

Post sent using JamiiForums mobile app
 
KWAHYO SIKUIZI ZALI LA MENTALI HAKUNA

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Bila shaka huyo ni Mchungaji Peter Mitomingi wa TAG Mwenge Church jamaa ni mzuri sana kwenye semina za Uchumba,Ndoa,Vijana na Mahusiano
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom