Mchungaji nchini Uganda afunga kabisa baada ya kushinda milioni 100

Amos David Mathias

JF-Expert Member
Sep 3, 2022
1,574
3,028
Kama kichwa cha habari kinavyosema, "Mchungaji Huyu Amefunga Kanisa Baada ya Kushinda Sh Milioni 100 za Uganda Baada ya Kucheza Sports Betting."

Anakiri kusema kwamba alikuwa anakazana kutoboa kwa kuwasisitiza watu watoe fungu la kumi vizuri, lakini mambo hayakuwa yakienda kama alivyotegemea. Alifikiri atapata pesa nyingi sana, lakini ikawa ndivyo sivyo.

Anakiri pia alianzisha kanisa lake kwa ajili ya tamaa za kupata hela, kwani alikuwa anawaona wachungaji wengi humo nchini Uganda wanajaza makanisa na kukusanya fedha nyingi sana, na walikuwa wakitoa utabiri wa uongo ili kuwavuta watu, na kweli watu walifurika.

Mchungaji anaripotiwa kukiri kwamba alichukua hela za sadaka pamoja na hela zake na kupata shilingi milioni moja ya Uganda, ambayo aliifanya kama mtaji wa kubeti.

Juhudi zake zilifua dafu na ndipo akashinda shilingi milioni 100 za Uganda, hivyo akachukua hatua ya kufunga kanisa.

Sababu ya kufunga kanisa anasema hizo pesa alizoshinda zimemsaidia kupata njia nyingi sana za kutengeneza vipato vingi, kwahiyo hakuna maana ya kuendelea na biashara ya kanisa. Anakiri amefurahi sana na hajawahi shika hela nyingi kiasi hicho tangu azaliwe.
Screenshot_20230403-011029.jpg
 
Back
Top Bottom