Mchungaji na mwimbaji wa Gospel asimulia enzi zake za Bongo Fleva

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
19,643
33,427
Anaitwa Addo November ..soma hapa chini

Hivi maisha gani sijayaishi? Najua kuwa na Pesa najua Kufulia katika Mambo Yote nimegundua Bila Mungu basi hatima yako iko mashakani. Kipindi hicho naambiwa lazima Nioane na Mzungu Mtoto wa Tajiri Mkubwa Ujerumani Nikakimbia Kuja Afrika kufuata Hatima Yangu Kama Musa alivyoacha Ufalme kwa Farao (Filauni) Akaenda akaandaliwa kuongoza nchi yake.

Ngoja niwaambie Vijana wa leo unaweza ukaona wewe ndio wewe sasa bila kutazama kesho yako ipoje.
Kipindi kabla sijaenda Majuu marafiki zangu waliokua akina Inspekta Harun sijui kama wananikumbuka.. kuna binti anaitwa Zay B ndio nilimpeleka Studio kwa mara ya kwanza tukatoa heat Radio One.

Baadae nyuma kidogo kabla sijaenda Ulaya Ndugu yangu naye sasa ni Mchungaji kama mimi nikamuachisha kuimba kwaya tukiwa Sekondari nikampeleka Studio tukarekodi heat song anaitwa Muzaula Kashumba au KBazil leo nimekumbuka hao wachache ipo siku nitakuletea historia ya Kundi la Muziki la Emergency Poison likiongozwa na Peace E na Master Crazy na baadae kundi kubwa la Hip Hop Toig'z Crew na jamaa anaitwa Crazy Dog mwingine KG (Kajeli Chambo) ambapo tulikua tunafanya matamasha anayeweza kukumbuka baadhi ya haya ni DJ John Dillinga Matlou na Godwin Gondwe kwa sehemu enzi za Sosteness Ambakisye au SOS B.

Wakati Mr II anatamba na kibao Chao cha Dola Yuko Wapi Dola kenda Wapi alikuwepo wapi now...!! Soggy aliimba Napigiza Pande zote mimi bado ninakutesa.. turingeringe kwa Amani. Kipindi tukienda show Mr Nice Basi zima la wasanii hajulikani mnahisi ni utingo.

Hili nalo likapita Yote haya nasema ili mjue bila Mungu basi dunia ni kama kichaka leo nikipita nikiwaona baadhi ya bongo fleva wanamini wao ndio kila kitu kumbe ni Muda tu watazeeka na kutoweka Kwenye ramani.. Okay basi nikaokolewa ndugu yangu Sam Sasali anajua hili nikajua kwa Yesu tambarare...!! Leo Muziki wa Injili ni Biashara na Ujiko siyo huduma tena Enzi naokoka Heat SongMALEBOtuliacha biashara kuja kwa Yesu halafu kwa Yesu nako tunakuta biashara tunakuta sanaa.. zinaa.. yaani Church limevamiwa... ukisema ukweli unaambiwa unapinga watumishi... dah.. Rai yangu Vijana turudi kwa Mungu siku ni chache mno

Ooh Lord Teach me how to number my Days. Jesus is coming soon

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu ndio Addo November sasa na kabla hajaamua kuokoka.
Screenshot_20190406-181828_Instagram.jpeg
Screenshot_20190406-181722_Instagram.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom