Mchungaji na Mbunge Getrude Rwakatare azikwa na Serikali kanisani kwake (Mlima wa Moto) na watu wasiozidi 10

Ushauri wangu. Kwa kuwa kaburi liko mazingira ya Kanisa lake. Wanakondoo jumapili watataka waende hapo kwa wingi kumuaga kipenzi chao.

Pawe na mtu wa kulinda utaratibu hapo. Machozi nayo ni maji maji yatokayo mwilini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Usidanganyike!! Mwili wa Mama Getrude Lwakatare ulizikwa Jumanne maeneo ya Mbweni.

Pale kanisani kwake wamezika mbao za jeneza tu.
 
Idiot, msiba wa baba yake Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Mambo ya Ndani ulihudhuriwa na mamia ya waombolezaji ( this week).
Kwa hiyo kila anayekufa sasa kwa ugonjwa wowote msiba unaratibiwa na serikali?

Kwa hiyo kila familia yenye msiba, muongozo wa serikali watu wasizidi 10?



Mojawapo ya mbinu za kujikinga na maambukizi ya Corona ni kuepuka mikusanyiko, ndicho kilichofanywa hapo, na mbinu nyingine ya kujikinga ni kuvaa mask, kama walivyozivaa hapo.

Bado sijaona uthibitisho wa maana kwa wale wanaodhani Mama Rwakatare amefariki kwa Corona, wanatoa sababu nyepesi tu.

Kwa wakati tulionao; ni vyema mkumbuke hata misiba mingine mtaani, au sherehe zozote, hazitakiwi pawepo mikusanyiko kwa sababu ya Corona, sasa sio kila ataekufa wakati huu aonekane amekufa kwa Corona sababu tu shughuli za mazishi zinafanywa na serikali.

Serikali ina jukumu la kulinda raia wake, japo kwa wingi wao itakuwa vigumu kuwazika wote kwa uangalizi wake, na wakati wa mazishi yoyote wakati huu, hata kama marehemu hajafa kwa Corona, lazima wachukue tahadhari zote ili kujikinga na maambukizi, sababu wapo kwenye mkusanyiko.

Apumzike kwa amani Mama Getrude P. Rwakatare, ametuachia alama ya kumkumbuka hapa nchini.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe umeona eeee. Hizo picha mimi ndo wa kwanza kuzitupia mtandaoni(humu) zimetoka direct kwa original source. Moderators wamezipandisha lwebyw uzi mara paap naona zimetiwa nembo ya millard ayo.
Huyu Ni kumdai fidia tu
 
Baba ake Simbachawene hakua na wadhifa Serilalini wa Bungeni ndo maana alizikwa na wananchi kwa utaratbu wao. Serikali ikisimama kushiriki mazishi lazima kucontrol nyomi tu
 
Baba ake Simbachawene hakua na wadhifa Serikalini wala Bungeni ndo maana alizikwa na wananchi kwa utaratbu wao. Serikali ikisimama kushiriki mazishi lazima kucontrol nyomi tu
 
Ila Corona ni kiboko.
Fikiria huu msiba wa mama corona isingekuwepo.
Watu wa maua wangeuza sana maua.
Watu wa chakula.
Watu wa magari na kampuni za mazishi.
Wauza nguo sare za kina mama.
Waandishi wa habari.
Watu wa kuplan mazishi.
Wote hao wamekosa hela.
Huu mji ungekuwa na heka.
Mikocheni B mtaa ungefungwa.
Naimani wasingesafirisha Bukoba lakini wadau kutoka pembe za dunia na wale wanaijeria ingekuwa hapatoshi.
Corona hii jamaniiiiiii
Ndugu wamekosa shavu la michango.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom