Mchungaji na Mbunge Getrude Rwakatare azikwa na Serikali kanisani kwake (Mlima wa Moto) na watu wasiozidi 10

Mojawapo ya mbinu za kujikinga na maambukizi ya Corona ni kuepuka mikusanyiko, ndicho kilichofanywa hapo, na mbinu nyingine ya kujikinga ni kuvaa mask, kama walivyozivaa hapo.

Bado sijaona uthibitisho wa maana kwa wale wanaodhani Mama Rwakatare amefariki kwa Corona, wanatoa sababu nyepesi tu.

Kwa wakati tulionao; ni vyema mkumbuke hata misiba mingine mtaani, au sherehe zozote, hazitakiwi pawepo mikusanyiko kwa sababu ya Corona, sasa sio kila ataekufa wakati huu aonekane amekufa kwa Corona sababu tu shughuli za mazishi zinafanywa na serikali.

Serikali ina jukumu la kulinda raia wake, japo kwa wingi wao itakuwa vigumu kuwazika wote kwa uangalizi wake, na wakati wa mazishi yoyote wakati huu, hata kama marehemu hajafa kwa Corona, lazima wachukue tahadhari zote ili kujikinga na maambukizi, sababu wapo kwenye mkusanyiko.

Apumzike kwa amani Mama Getrude P. Rwakatare, ametuachia alama ya kumkumbuka hapa nchini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
guys kwel tujiulize kwanin azikwe na serikali kwani hana ndugu huyu mama


Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi kuna msiba wowote kwa wakati huu ambao serikali haihusiki kuzika? Labda kwa kuwa wanazingatia kuzuia msongamano/mkusanyiko…..wakiwaachia ndugu wazike ndugu wana uwezo wa kuzuia watu wasije kumzika mpendwa wao?...… Sidhani kama kuzikwa na serikali kunamaanisha ni corona case.
 
Back
Top Bottom