johnmashilatu
JF-Expert Member
- Sep 16, 2010
- 718
- 703
Idadi ya watu wanaojitangaza kupewa uwezo na mwenyezi Mungu ili kutibu Magonjwa Sugu imezidi kuendelea baada ya mkazi mwingine wa wilaya ya kasulu kuanza kutoa dawa anayodai inatibu magonjwa sugu
Mkazi huyo wa kitongoji cha Kumsenga Bw Leveliani Ishengoma amekuwa mtu wa tano kujitokeza baada ya Mcungaji Ambakile Mwaisapile wa Loliondo mkoani Arusha kutangaza kupatiwa dawa hiyo na mungu
Bw.Ishengoma ameiambia redio Kwizera kuwa ameoteshwa na Mungu katika maono yake juu ya dawa ambayo inatibu magonjwa mbalimbali sugu ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa Ukimwi
Amesema ameoneshwa mti kama ule anaoutumia Babu wa Loliondo na kwamba mti huo una nguvu zaidi kuliko ule wa Babu wa Loliondo
Amesema ameoteshwa mti ambao huchemshwa na kumpatia mgonjwa kwa gharama ya shilingi elfu moja ambapo watu 200 wamekunywa dawa hiyo.
Mganga mkuu wa wilaya ya Kasulu Dr Gerge Mamboleo amesema hana taarifa kuhusiana na tukio hilo