Mchungaji Msigwa: Tuchague kuitunza Ngorongoro au tuache Wamasai wafuge ng’ombe kule

Maramla

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
581
642
Mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA ambaye pia ni Mwenyekiti wa kanda ya Nyasa wa chama hicho, aliyewahi pia kuwa mbunge wa Iringa mjini na waziri kivuli wa Wizara ya Maliasili na utalii Mchungaji Peter Msigwa amesema hali ni mbaya katika hifadhi ya Ngorongoro na jitihada za haraka kuinusuru hifadhi hiyo zinahitajika huku akiilaumu Serikali ya chama cha mapinduzi(CCM) kwa kutaka kuiuwa hifadhi hiyo.

Mchungaji Msigwa ameishangaa Serikali kwa kushindwa kufanya maamuzi sahihi kwa wakati kuinusuru hifadhi hiyo licha ya kuwa na ongezeko kubwa la watu na mifugo linalohatarisha ustawi wa watu ,wanyama na uhifadhi wa eneo la Ngorongoro kwa kuogopa kupoteza kura za uchaguzi bila kujali maslahi mapana ya taifa nay a eneo husika yanayotokana na shughuli mbalimbali ikiwemo utalii.

“Serikali ya chama cha Mapinduzi inatukosea sana ,kama haiwezi kutunza mali ambazo tumewapa,wanatukosea sana ,hizi mali ,Tanapa ,Serengeti,Ngorongoro,Mkomazi ,Ruaha,kila kitu kitulo,hii sio mali ya CCM ni mali ya Taifa kwahiyo CCM imepewa dhamana ya kutunza ,wanapokuwa wazembe kiasi hiki,watu mpaka wanajenga mle ndani ,mle ndani wanafuga Ng’ombe wanaozidi zaidi maanake wanatukosea sisi na ndio maana tunataka tuwatoe Madarakani wanashindwa kutunza mali za umma ambazo wamepewa dhamana wazitunze”.Alisema Msigwa.

Ameongeza kuwa hali ya watu wa Ngorongoro ni mbaya na maeishauri serikali kutoa fidia itakayowashawishi wakazi hao kuhama kwenda sehemu bora zaidi watakazopatiwa huduma na mahitaji yanayoendana na changamoto za sasa huku akiwaasa wasomi wa kabila la kimaasai ambao wanapaza sauti kutokea Dar es Salaam kushinikiza wananchi wanyonge wa Ngorongoro wasibadilishiwe maiosha yao kwa kisingizio cha sheria ambayo kimsingi sio msaafu wala biblia na imetokana na matakwa ya kikoloni ,kiasi cha kuwazuia wakazi wa eneo hilo kushindwa kujenga nyumba za kisasa miundombinu bora ya huduma za kijamii nk,huku akiwashangaa wabunge waliopita na wa sasa wa eno hilo kuwa mstari wa mbele katika uvunjifu wa sheria wanaoyoitetea.
 
Akisikia sauti za wamasai, wanaharakati kama Ole Ngurumwa walioshirikiana katika kusagia serikali, na kwamba PM kawasikiliza na kuhaidi kufanyia kazi maoni yao; atabadilisha lugha!

Ataanza kusema ngorongoro hali siyo mbaya ila serikali ya CCM ndiyo mbaya! Sababu hawa wapinzani uchwara kila wanachoongea lazima wamamalizie kwa kuonyesha ni makosa ya CCM!
 
Vichaa wote wanaotaka wamaasai waangamie hawatashinda hii vita alieanzisha ndie atakaeshindwa.

The maasai are there to stay fanyeni mumtoe huyo popo wenu Manongi hapo NCA.
 
Me nadhani kabla ya kutumia mihemko kutamka maneno honyo kuna vitu vingi vya kujiuliza

1. Mnajua wamasai walikuepo NCAA muda huu walitolewa wap kabla ya kuja hapo

2. Mnajua status/ hadhi ya NCAA Yaani ile coe existence tuu ya watu , wanyama wa kufugwa na wanyama wa porini imefanya NCAA imepokea status ngap duniani??

3. Kutolewa wamasai NCAA hadhi yake itabadilika au itabaki vipi

Busara itumike kuliko mihemko NCAA ni urithi wa dunia
 
Akalime mahindi huyo. Huu ni msimu wa masika. Atauche na mifugo yetu.
Tuna Demands zetu mezani. Yaani kama Russia alivyopeleka minimum demands ili asivamie Ukraine.
Na sisi tuna minimum demands.
Jamii yetu iko organized. Tofauti sana na jamii zingine.
Tunakaa vikao vya ukoo, kijiji, rika na jamii kwa ujumla.
PM hakurupuki kwa sababu anajua dhamana aliobeba.
Kina Msigwa waropoke tu lkn sisi tunaongea na PM. Na sio PM Majaliwa tu.
Hata PM Pinda tulishaongea naye.
Tumeshapita ngazi ya DG wa NCAA na kwanza hatuna imani naye.
Tumepita ngazi ya Waziri wa Malia asili na Utalii. Huyu dogo Damas anahangaika tu. Msomi na mwenye busara Balozi Khagasheki alishafika akaona ni ngumu.
Kwa sababu tuna genuine demands.
Hili swala lineshatoka katika ngazi ya kutoa maoni.
 
Back
Top Bottom