Mchungaji Msigwa sasa aja na hoja ya kumwondoa Naibu Spika

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Msigwa.jpg

Zikiwa zimepita siku kadhaa tangu wabunge wa Ukawa kuanza kususia vikao vinavyoendeshwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa amewasilisha hoja ya kumwondoa madarakani kwa madai ya kukiuka kanuni za Bunge wakati wa uwasilishwaji wa mjadala wa Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2016/17.

Msigwa amewasilishwa barua kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai kuiomba Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iangalie na kujiridhisha na hoja hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari bungeni jana, Msigwa alidai kuwa Dk Tulia aliondoa mapendekezo ya mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe na Jitu Son wa Babati Mjini (CCM) katika Bunge kwa sababu hayakufuata kanuni ilhali wabunge hao walipeleka marekebisho yao katika Kamati ya Bajeti ya Bunge.

“Dk Tulia amekiuka kanuni kwa kuzuia marekebisho ya waheshimiwa wabunge kwa kuzuia hoja zao zisijadiliwe na kamati ya Bunge huku akijua kuna uamuzi wa Spika wa Bunge kuhusu utaratibu wa kutekeleza kanuni ya 109 fasili ya pili ya Kanuni za Bunge toleo la Januari 2016,” alisema.

Pia, alisema Muswada wa Sheria ya Fedha wa 2016/17 uliosomwa kwa mara ya kwanza bungeni uliopewa namba tisa haukuwa ule uliowasilishwa kwa mara ya pili kwa kujadiliwa na kupitishwa na wabunge.

Alisema muswada huo uliowasilishwa mara ya pili uliwasilishwa kinyume cha kanuni za Bunge kwa sababu haukufuata taratibu na kupewa namba 12.

Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano ya Bunge, Owen Mwandumbya alisema muswada huo ulifuata taratibu za kikanuni kuanzia uwasilishaji, mijadala na upitishwaji.

Alisema maoni ya wadau katika muswada huo yalikuwa mengi, hivyo kulazimu kuchapishwa mara ya pili ili maoni ya wadau yazingatiwe.

Mbunge wa Rufiji, Mohamed Mchengerwa alisema kama maudhui ya muswada ni sawa hata kama namba zikikosewa haina madhara.
 
Me najiuliza kwa bunge lililobaki bila wenzao wa upinzani wanafanya kazi gani pale?sina maana kwamba bila upinzani bunge haliendi linaenda ila sio km ilivyo sasa!bunge limepoteza mvuto imekuwa kama darasa la 1 shule ya msingi!au kazi zao don anawafanyia?!hivyo wao kukosa cha kujadili na kufanya pale?!kama vipi me pia naona don anaweza kupiga kazi zote bila bunge maana namkubali anaweza!
 
Msigwa anajua biblia hizi zheria zilizokosewa amejuaje wakati yeye alisusia vikao ndio maana nasema hivi kila mpuuzi akionge ni lazima asikilizwe?
 
Msigwa.jpg

By Sharon Sauwa, Mwananchi; ssauwa@mwananchi.co.tz

Dodoma. Zikiwa zimepita siku kadhaa tangu wabunge wa Ukawa kuanza kususia vikao vinavyoendeshwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa amewasilisha hoja ya kumwondoa madarakani kwa madai ya kukiuka kanuni za Bunge wakati wa uwasilishwaji wa mjadala wa Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2016/17.

Msigwa amewasilishwa barua kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai kuiomba Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iangalie na kujiridhisha na hoja hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari bungeni jana, Msigwa alidai kuwa Dk Tulia aliondoa mapendekezo ya mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe na Jitu Son wa Babati Mjini (CCM) katika Bunge kwa sababu hayakufuata kanuni ilhali wabunge hao walipeleka marekebisho yao katika Kamati ya Bajeti ya Bunge.

“Dk Tulia amekiuka kanuni kwa kuzuia marekebisho ya waheshimiwa wabunge kwa kuzuia hoja zao zisijadiliwe na kamati ya Bunge huku akijua kuna uamuzi wa Spika wa Bunge kuhusu utaratibu wa kutekeleza kanuni ya 109 fasili ya pili ya Kanuni za Bunge toleo la Januari 2016,” alisema.

Pia, alisema Muswada wa Sheria ya Fedha wa 2016/17 uliosomwa kwa mara ya kwanza bungeni uliopewa namba tisa haukuwa ule uliowasilishwa kwa mara ya pili kwa kujadiliwa na kupitishwa na wabunge.

Alisema muswada huo uliowasilishwa mara ya pili uliwasilishwa kinyume cha kanuni za Bunge kwa sababu haukufuata taratibu na kupewa namba 12.

Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano ya Bunge, Owen Mwandumbya alisema muswada huo ulifuata taratibu za kikanuni kuanzia uwasilishaji, mijadala na upitishwaji.

Alisema maoni ya wadau katika muswada huo yalikuwa mengi, hivyo kulazimu kuchapishwa mara ya pili ili maoni ya wadau yazingatiwe.

Mbunge wa Rufiji, Mohamed Mchengerwa alisema kama maudhui ya muswada ni sawa hata kama namba zikikosewa haina madhara.

Source: Mwananchi

Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mch. Peter Msigwa amepeleka barua kwa Spika wa Bunge yenye hoja ya kutaka kumng'oa madarakani Naibu spika wa Bunge Dk Tulia Ackson Mwansasu.
 
Afadhali wamtoe haraka maana wananchi tumechoka kuona wabunge tuliowachagua wananyanyaswa na mbuge wa jimbo la Raisi
 
Itakuwa ni jambo la maana akitoka huyu tulia akatulie atulie akwatuliwe, maana amepitisha bajeti ya hovyo.
 
Some time ndg msigwa uwe unanyamaza tuu kama mlivyoamua kunyamaza , nn kimekutuma leo kuongea ili hali umefunga mdogo kwa kitambaa kuongea na .spika
 
Akitokewa dr Tulia nitahama nchi kwa sbb anaongoza bunge vzr tena anajiamini sana na anafuata sheria, tena atakuwa mwanamke wa kipekee kuongoza bunge vzr. Achenu wivu tunawajua mkiona kiongozi mzuri mnamchukia.
 
Hivi nyie ukawa mnaweza kutaja ni kiongozi gani wa ccm mnamkubali? Maana nyie kila mtu anayefanya kazi vzr lazima mumchukie mpoje?
 
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mch. Peter Msigwa amepeleka barua kwa Spika wa Bunge yenye hoja ya kutaka kumng'oa madarakani Naibu spika wa Bunge Dk Tulia Ackson Mwansasu.

Sina shaka, UKAWA wamehama njia, hawajui wanaelekea wapi
 
Anna Makinda alikuwa bora mala mia zaidi ya Tulia. Kweli nimeamini utu uzima dawa. Busara na hekima haviko na Tulia.
 
Msigwa.jpg

Zikiwa zimepita siku kadhaa tangu wabunge wa Ukawa kuanza kususia vikao vinavyoendeshwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa amewasilisha hoja ya kumwondoa madarakani kwa madai ya kukiuka kanuni za Bunge wakati wa uwasilishwaji wa mjadala wa Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2016/17.

Msigwa amewasilishwa barua kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai kuiomba Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iangalie na kujiridhisha na hoja hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari bungeni jana, Msigwa alidai kuwa Dk Tulia aliondoa mapendekezo ya mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe na Jitu Son wa Babati Mjini (CCM) katika Bunge kwa sababu hayakufuata kanuni ilhali wabunge hao walipeleka marekebisho yao katika Kamati ya Bajeti ya Bunge.

“Dk Tulia amekiuka kanuni kwa kuzuia marekebisho ya waheshimiwa wabunge kwa kuzuia hoja zao zisijadiliwe na kamati ya Bunge huku akijua kuna uamuzi wa Spika wa Bunge kuhusu utaratibu wa kutekeleza kanuni ya 109 fasili ya pili ya Kanuni za Bunge toleo la Januari 2016,” alisema.

Pia, alisema Muswada wa Sheria ya Fedha wa 2016/17 uliosomwa kwa mara ya kwanza bungeni uliopewa namba tisa haukuwa ule uliowasilishwa kwa mara ya pili kwa kujadiliwa na kupitishwa na wabunge.

Alisema muswada huo uliowasilishwa mara ya pili uliwasilishwa kinyume cha kanuni za Bunge kwa sababu haukufuata taratibu na kupewa namba 12.

Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano ya Bunge, Owen Mwandumbya alisema muswada huo ulifuata taratibu za kikanuni kuanzia uwasilishaji, mijadala na upitishwaji.

Alisema maoni ya wadau katika muswada huo yalikuwa mengi, hivyo kulazimu kuchapishwa mara ya pili ili maoni ya wadau yazingatiwe.

Mbunge wa Rufiji, Mohamed Mchengerwa alisema kama maudhui ya muswada ni sawa hata kama namba zikikosewa haina madhara.
Aliyopeleka Ole Miliya iliishia wapi? Au ndio kila mtu nitoke vipi.
 
Back
Top Bottom