Mchungaji Msigwa: Rais Magufuli huenda kanisani kama muumini au Rais?

Huo ndio mfano bora kabisa wa kuchanganya dini na siasa! Ila kwa kuwashutumu wengine; hawajambo! Katika Liturgy ya Kanisa Katoliki hakuna mahali popote pa "Rais kuzungmza/kuhubiri" wakati wa ibada tena Yesu akiwa mbele pale katika maumbo ya mkate na divai.
Aiseeee!
 
Huyu bwana anatapatapa nazani anajua muda wake kunyakuliwa na corona u karibu,maana anatilia mashaka kila kitu kuanzia barakoa,furmigation,mpaka chanjona hisi kwa kuwa hana tena viumbe hai(wapinzani) wa kuwarushia lawama
Unazungumzia kifo hikihiki ambacho hata wewe hujui kitakupata lini au?
 
Kwa Mzee kama wewe ni aibu sana kuwa muongo
Msigwa katuuzia sana suluari za shule cadet pale Highlands wakati katoka Matamba kule uwanji na kufungua meza ya mitumba pale !iyomboni.

Baadae akachukuliwa na Mateso wa pale Cates hotel kama muangalizi wa hema.
 
Bwana Msigwa, kuna watu wameumbwa au wana tabia ya kupenda kuonekana kila walipo! kupenda kusifiwa, kunyenyekewa na kuabudiwa kuliko hata Mungu aliyeumba kila kitu. Mfano wa watu hawa ktk biblia ni akina Yerode aliyemuoa Herodia.
 
Peter Msigwa sio mchungaji na hawezi kuwa mchungaji kwa tabia zake alizokuwa nazo.

Mjumuisho wa sifa zifuatazo zinamtoa huyo mwanasisa kwamba ni mchungaji kwa kuwa hana uthibitisho wa uadilifu wake katika jamii na watu wa imani yake ya kiroho:

"..
SIFA NNE(4) ZA KIONGOZI MZURI KANISANI. 1. MWENYE UWEZO. -Mwenye uwezo kiakili. -Mwenye uwezo wa kujua afanye nini katika kutimiza kusudi la MUNGU kupitia uongozi wake. -Mwenye uwezo wa kuelewa afanyeje anapokabiliana na magumu katika uongozi wake. -Mwenye uwezo wa kujiamini na kujiheshimu. -Mwenye uwezo wa kutumia uongozi wake kwa faida ya kanisa zima na jamii. -Anajielewa, anajali na yuko makini katika mambo ya MUNGU. -Mwenye uwezo wa kuongoza. -Mwenye uwezo wa kujieleza. -Mwenye uwezo wa kujua mambo mengi li uwezo huo umsaidie katika uongozi wake kanisani. -Anajua matokeo mabaya ya uongozi wake yatampa nini na matokeo mazuri ya uongozi wake yatampa nini. -Mwenye uwezo wa kuthubutu, mbunifu na mwangalifu. -Mwenye uwezo wa kumtegemea MUNGU na sio akili zake.

Uwezo unahitajika sana kwa kiongozi wa kanisa. BWANA YESU alipochagua viongozi ambao kwa hao injili ya uzima ilitufikia mimi na wewe, jambo la kwanza BWANA YESU aliwapa uwezo kisha mengine yakafuata. Luka 9:1-2 ''Akawaita wale Thenashara, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi. Akawatuma wautangaze ufalme wa MUNGU, na kupoza wagonjwa. '' Hawa mitume wa MUNGU ambao ni viongozi walioleta injili ya BWANA kwetu, wasingekuwa na uwezo hakika wasingeweza kutimiza kusudi la MUNGU kwenye uongozi wao, ndio maana BWANA YESU akawapa uwezo ili wakamilike. 2. MWENYE KUMCHA MUNGU. -Anaishi maisha matakatifu maana kuishi maisha matakatifu ndiko kumcha MUNGU. -Anamcha MUNGU kupitia mali zake. -Anamcha MUNGU katika ndoa yake.

-Anamcha MUNGU wakati wote, iwe wakati wa mabaya au wakati wa mazuri. -Ana nia ya KRISTO ndani yake yaani hakuna jinsi unaweza kumtoa kwa YESU. -Anawapenda watu wote. -Amejifunza Neno la MUNGU vizuri na huwa anatendea kazi Neno lile analojifunza. -Kama kiongozi atahakikisha na wote anaowaongoza na wao wanamcha MUNGU. -Kama kiongozi basi atakuwa ana muda wa kuwaelekeza anaowaongoza ili wamche MUNGU siku zote. -Tumaini lake ni uzima wa milele, hivyo atatumia nafasi yake kiuongozi kanisani kuwasaidia wengine nao ili wamcha MUNGU na wamweke MUNGU mbele katika maisha yao. -Anamtii ROHO MTAKATIFU na siku zote anaenenda kwa ROHO na sio kwa mwili. SIFA SABA ZA MTU MCHA MUNGU NI; (A).

Anaishi maisha matakatifu ndani ya wokovu wa KRISTO. (B). Ni mtoaji wa matoleo yote kama inavyoagizwa na Biblia. (C). Ni muombaji. (D). Anashirikiana na wateule wenzake katika kazi ya MUNGU kanisani. (E). Anajali wengine na kuwasaidia kiroho na kimwili. (F). Anamtii ROHO MTAKATIFU maana ROHO MTAKATIFU ndiye msimamizi mkuu wa kanisa la KRISTO Duniani. (G). Ni kielelezo chema kwa wengine katika mambo mema. Kumcha MUNGU ni jambo la lazima kwa kiongozi wa aina yeyote kanisani.

Ni lazima viongozi kanisani wawe velelezo vyema vya kumcha MUNGU. Kama viongozi katika idara zao watakuwa wanamcha MUNGU hakika hawatakubali kutenda jambo baya hata kama jambo hilo linaagizwa na kiongozi mkuu. Hapa chini ni andiko ambalo linaonyesha kiongozi mkuu asiyemcha MUNGU anavyowalazimisha viongozi wadogo ambao ni wakunga wawe wanauwa watoto wanaume wanapowazalisha wajawazito, lakini kwa sababu hawa viongozi katika ukunga walikuwa wanamcha MUNGU hakika hawakuuwa watoto maana walikuwa wanamcha MUNGU.

Kutoka 1:17 " Lakini wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, wasifanye kama walivyoamriwa na huyo mfalme wa Misri, lakini wakawahifadhi hai wale wanaume.'' Hawa wazalishaji ambao ni viongozi katika idara yao ya kuzaliwa wajawazito, wasingekuwa wanamcha MUNGU hakika wangemtii kiongozi wao mkuu hivyo wangeuwa watoto wa kiume akiwemo na Musa ambaye kwa Waisraeli ni nabii mkubwa kuliko manabii wote. Ucha MUNGU kwa kiongozi mzuri ni jambo la lazima. 3. MKWELI. -Kiongozi mzuri ni lazima awe mkweli katika mambo yote. -Awe mkweli katika matendo yake. -Awe mkweli katika mambo yote.

Mtu mkweli maana yake sio muongo. -Ndiyo yake iwe ndiyo na siyo yake iwe siyo. -Akisema jambo fulani zuri atalitenda hakika atalitenda, na akisema jambo fulani hatalitenda hakika hatalitenda. -Ana msimamo sahihi wa kiMUNGU katika maisha yake. -Anajua kwamba faida ya mtu mkweli ni kuaminiwa na anaowaongoza na hasara ya mtu muongo ni kutokuaminiwa na anaowaongoza. -Ni mkweli kwenye maneno yake na matendo yake. -Ni mkweli kanisani na nyumbani pia. -Anapenda kweli na anaiishi kweli ambayo ni Neno la MUNGU. -Anafundisha kweli na ni mkweli katika yote. -Anaaminika kwa anaowaongoza maana huwa hasemi uongo bali ukweli tu. -Anapanga mipango ya kweli na kuitekeleza kwa wakati na kwa usahihi. MUNGU anawapenda watu wakweli na ndio maana Neno lake linasema;

'' Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo. Mambo mliyojifunza kwangu na kuyapokea, na kuyasikia na kuyaona kwangu, yatendeni hayo; na MUNGU wa amani atakuwa pamoja nanyi. -Wafilipi 4:8-9'' 4. ANACHUKIA MAPATO YA UDHALIMU. -Mapato ya udhalimu ni mapato ambayo Biblia inayakataza mfano Mali ya wizi n.k. -Kwanza yeye mwenyewe kiongozi anatakiwa asiwe mdhalimu. -Ni kielelezo chema katika kumtolea MUNGU zaka na sadaka mbalimbali, maana kutokutoa Zaka ni udhalimu mbele za MUNGU.

Pesa ya wizi ni udhalimu. Malaki 1:13 '' Tena mwasema, Tazama, jambo hili linatuchokesha namna gani! Nanyi mmelidharau, asema BWANA wa majeshi; nanyi mmeleta kitu kilichopatikana kwa udhalimu, na kilema, na kilicho kigonjwa; ndivyo mnavyoleta sadaka; je! Niikubali hii mikononi mwenu? Asema BWANA.'' -Kiongozi mzuri hamwibii MUNGU zaka. -Hatoi wala kupokea Rushwa. Mapato ya udhalimu ni mali au pesa ambayo kupatikana kwake sio kwa njia sahihi wala njia ya utakatifu. Mfano kupata mdhamini wa kanisa ambaye anawataka kanisa mmfanyie kitu fulani ambacho ukiangalia kwa makini kitu hicho kinawatoa kanisa katika utakatifu. -Kiongozi lazima ajitenge na pesa au mali ya wizi.

-Kiongozi lazima ajitenge na pesa au mali zilizopatikana kishirikina. -Kiongozi lazima ajitenge na pesa feki au fedha bandia. -Kiongozi lazima atangulize maagizo ya Biblia katika mambo yote ya Pesa. -Kiongozi asipokee hongo, rushwa wala takrima maana kiongozi mzuri lazima awe ni yule anayechukia mapato ya udhalimu. -Hata pesa za zawadi anazopewa kiongozi, kama pesa hizo zina lengo la kumfanya apendelee watu, huo ni udhalimu na anatakiwa ajitenge na udhalimu wote. -Watu wote kanisani ni watu wa MUNGU hivyo kiongozi hatakiwi kuwabagua au kuwatenga kwa sababu tu ya utoaji wao kanisani au kwa sababu tu ya vipato vyao.

-Kiongozi wa kanisa kuwanyenyekea wenye mali hiyo ni dalili kuu ya kupenda mapato ya udhalimu. -Kiongo lazima awe anafichua mapato ya udhalimu na lazima ahakikishe haliibiii kanisa wala kikundi ndani ya kanisa. MUNGU anaonya viongozi kuhusu udhalimu akisema; ''Ufue mnyororo; kwa maana nchi hii imejaa hukumu za damu, nao mji umejaa udhalimu.-Ezekieli 7:23 '' ..."
 
Huo ndio mfano bora kabisa wa kuchanganya dini na siasa! Ila kwa kuwashutumu wengine; hawajambo! Katika Liturgy ya Kanisa Katoliki hakuna mahali popote pa "Rais kuzungmza/kuhubiri" wakati wa ibada tena Yesu akiwa mbele pale katika maumbo ya mkate na divai.
kama na umri huo unadhani kanisani ni kwa ajiri ya kusali pekee, wewe ndio wa kusikitikiwa.
 
Magufuli badala ya kwenda kanisani kusikiliza injili na mawaidha. Akifika huko yeye ndiye anakuwa mhubiri na kuhutubia taifa. Hakuna rais aliye wahi kwenda kanisani au msikitini na kuanza kuhubiria taifa.

Ikitokea rais muislam akawa anazungumza na taifa tokea mimbari ya msikiti hapatatosha maana ndugu zangu manaswara nawajua
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom