Mchungaji Msigwa na Joseph Mbilinyi wafungua kesi ya Kikatiba dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupinga unyanyasaji Magerezani

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,363
217,401
Msigwa Jongwe.jpg

Jongwe 11.jpg

Wamesema kwamba wanafungua kesi hiyo ili kulinda heshima ya Wafungwa wawapo Jela, ambako haki na utu wao unapuuzwa.

Walalamikaji hao ambao pia ni wabunge wa Zamani na WAFUNGWA WASTAAFU wanadai kwamba Wafungwa wa Tanzania wawapo gerezani wanalazimishwa Kupima Ukimwi huku Majibu ya vipimo hivyo yakisomwa hadhani mbele ya Kadamnasi , jambo ambalo wanaliona kama udhalilishaji usio na tija yoyote .

Katika madai yao hayo wamedai pia kwamba kitendo cha kuwavua nguo wafungwa mbele ya hadhara kwa madai ya kuwakagua kinatweza Utu wa Wafungwa na ni Kinyume cha haki za binadamu .

=====

TAARIFA KWA VOMBO VYA HABARI

Ndugu Wanahabari,

Tunapenda kutoa taarifa hii muhimu kwenu, ili mtusaidie kusambaza kwa wananchi lengo kuu likiwa ni sehemu ya uchechemuzi juu ya Haki za Msingi ambazo ziko ndani ya katiba na ambazo ni stahili ya kila raia wa Tanzania.

Sisi Mchungaji Peter Msigwa na Mheshimiwa Joseph Mbilinyi ambao tulikuwa wabunge wa majimbo ya Iringa Mjini Na Mbeya Mjini, tumefungua kesi ya kikatiba katika mahakama kuu ya Tanzania Masijala Kuu Ya Dar es salaam dhidi ya Mwanasheria mkuu wa serikali na Kamishna wa Magereza Tanzania tukipinga kukiukwa kwa haki zetu za msingi na za kikatiba wakati tunatumikia adhabu tulizopewa na mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya.

Labda kwa kifupi kwa wale ambao hawakumbuki, mimi Mheshimiwa Peter Msigwa na viongozi wenzangu tulikuwa tunakabiliwa na kesi ya Jinai Namba …….ya Mwaka 2019 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Baada ya kukamilika kwa kesi hiyo Tarehe 10 Mwezi Machi Mwaka 2020 tulipatikana na hatia na kutakiwa kulipa faini ya TZS 40,000,000/= au kutumikia kifungo cha miezi mitano (5) jela. Hatukuweza kulipa kiasi hicho kwa wakati, kitu kilichopelekea kutumia kifungo jela mpaka pale kiasi hicho kilipopatikana ambapo tulilipa faini hiyo na kuachiwa huru.

Kwa upande wa Mwenzangu Joseph Mbilinyi yeye alikuwa anakabiliwa na kesi ya Jinai katika mahakama ya hakimu mkazi Mbeya ambapo alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miezi sita (6) bila faini. Mwenzagu alitumikia kifungo mpaka alipopata msamaha wa jumla wa rais Tarehe 26 Mwezi 4 Mwaka 2018.

Kwa minajili hiyo kufungua kesi hii ya kikatiba kunatokana na kukiukwa dhidi yetu kwa haki zetu za kikatiba na za msingi katika kipindi ambacho tulikuwa tunatumikia adhabu zetu.

Baada ya hapo tuseme kuwa nchi yetu anaendeshwa na Katiba amabayo ndio sheria Mama, Sura ya kwanza, sehemu ya Tatu ya katiba yetu inaanza na ibara 12 na kumalizikia ibara 32, sehemu hii ndio ambayo inabainisha Haki na wajibu Muhimu wa wananchi na vile vile inatoa fursa chini ya Ibara 30(3) kwa mtu yoyoyte kufungua shauri Mahakama Kuu endapo ataona kuwa haki yake imevunjwa.

Labda tueleze pia kuwa Nchi yetu sio kisiwa kwa hali hiyo katika nyanja ya mahusiano ya kikanda na kimataifa nchi yetu imesaini na kuridhia mikataba kadhaa kuhusu haki za msingi za wananchi wake hii ikiwa ni pamoja na Tamko la Haki za Binadamu, mkataba wa Afrika juu ya haki za watu na mkataba wa kimataifa wa haki za kiraia na kisiasa.

Nyaraka hizo nne zilizotajwa zinaeleza bayana pamoja na haki nyingine haki za msingi zifuatazo:

KATIBA YA JAMBURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MWAKA 1977 KAMA ILIVYOREKEBISHWA

IBARA YA 12 (1) na (2)

(1) Binadamu wote huzaliwa huru, na wote ni sawa.

(2) Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.

  • IBARA YA 13 (6)
Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria, Mamlaka ya Nchi itaweka taratibu zinazofaa au zinazozingatia misingi kwamba–

wakati haki na wajibu wa mtu yeyote vinahitaji kufanyiwa uamuzi wa mahakama au chombo kinginecho kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa na haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia haki ya kukata rufaa au kupata nafuu nyingine ya kisheria kutokana na maamuzi ya mahakama au chombo hicho kinginecho kinachohusika;

(b) ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo;

(e) ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha.

  • IBARA YA 14 :
  • Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka katika jamii hifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sharia
  • IBARA YA 16
  • Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi yake binafsi na familia yake na unyumba wake, na pia heshima na hifadhi ya maisha yake na mawasiliano yake ya binafsi
  • IBARA YA 18
  • (1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa kutoingiliwa kati mawasiliano yake.
  • IBARA YA 19
  • Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu kubadilisha dini au imani yake.

7. IBARA YA 23(1) NA (2)

1) Kila mtu, bila ya kuwapo ubaguzi wa aina yoyote, anayo haki ya kupata ujira unaolingana na kazi yake, na watu wote wanaofanya kazi kulingana na uwezo wao watapata malipo kulingana na kiasi na sifa za kazi wanayoifanya.

2) Kila mtu anayefanya kazi anastahili kupata malipo ya haki.

Ibara za katiba tulizozitaja hapo juu kwa namna moja au nyingine zipo pia kwenye mikataba kadhaa ya haki za binadamu ambayo tumesaini na kuridhia matumizi yake. Mikataba hiyo ni Mkataba wa haki za binadamu wa Afrika, tamko la Haki za Bianadamu na mkataba wa haki za kisiasa na Kiraia. Ibara ya 9(f) ya katiba inatamka bayana kuwa mamlaka ya nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake katika lengo la kuhakikisha kwamba heshima ya binadamu inahifadhiwa na kudumishwa kwa kufuata kanuni za Tangazo la dunia kuhusu Haki wa Binadamu.

Katika kipindi chote ambacho tulikuwa gerezani kutumikia adhabu tulizopewa na mahakama kulikuwa na ukiukwaji mkubwa sana wa haki za msingi kama inavyoanishwa katika katiba yetu na Katika mikataba kadhaa ambayo nchii hii imetia sahihi, katika vifungu vilivyo orodheshwa hapo juu.

Mifano halisi ya ukiukwaji huo ni:

  • Kushindwa kutambua utu wa wafungwa: ndugu wanahabari katika kitu kinachodhalilisha utu wa mtu gerezani ni kitendo cha kuambiwa kuvua nguo mbele ya hadhara kwa ajili ya upekuzi wa mwili. Utaratibu unaotumika ni wa kizamani na wa kinyama sana ambao hauzingatii umri wa mtu na faragha ya mtu. Huu ni utaratibu unaotweza na kudhalilisha binadamu.
  • Kulazimishwa kupimwa UKIMWI na kupewa majibu mbele ya hadhara na bila kufuata masharti ya kitabibu yanayohitaji vipimo viwe kwa ridhaa na majibu kutolewa kwa siri.
  • Utaratibu wa kutoa adhabu gerezani hauzingatii kabisa kanuni ya msingi ya haki ya kusikilizwa
  • Kitendo cha kuwafanyisha kazi wafungwa bila kuwalipa kutokana na kazi wanazofanya
  • Utaratibu wa jeshi la magereza kuwapa wafungwa sare moja anapoingia bila kuwa na sare ya kubadili endapo sare imechafuka na anataka kuisafisha.
  • Utaratibu wa kuwalazimishwa wafungwa kutotumia sehemu za haja kubwa pasipo kupata ruhusa na askari magereza na kitendo cha kuweka ni mara ngapi kwa siku mfungwa anatakiwa kutumia sehemu za haja
  • Utaratibu wa kuwapa madaraka maafisa magereza kuwaadhibu wafungwa bila kuwapa wafungwa hao haki ya kusikilizwa
  • Kuwa na utaratibu wa kutoa adhabu za viboko kwa wafungwa wanaokutwa na hatia ni adhabu ambayo ni ya kudhalilisha na kutweza utu wa binadamu na hasa kwa namna ambavyo adhabu hiyo inapaswa kutekelezwa kwa mujibu wa sheria na kanunu za magereza.
  • Kutoa adhabu ya kumyima mfungwa na au kumpunguzia chakula ni ukiukwaji mkubwa wa haki ya kuishi.
  • Kutoa adhabu ya kumfungia mfungwa peke yake kwa muda Fulani kwenye chumba maalumu (solitary confinement).
  • Kujaza wafungwa wengi na kuwalaza kwenye chumba kimoja na kutokuwapa nguo maalumu ya kutumia wakati wa kulala kwa mfano mashuka na mablanketi ni hatari kwa afya wa wafungwa hata katika kipindi hiki dunia inapitia katika changamoto ya janga la COVID19
  • Kuwalazimishwa wafungwa kunyoa nywee zao na kubaki na vipara bila kujali Imani za dini za wafungwa.
  • Kutokuwa na utaratibu wa kuwapa fursa wafungwa kukata rufaa pale wanapokutwa na makossa chini ya utaratibu wa adhabu kwaa wafungwa magerezani.
Tumalize kwa kusisistiza kuwa kitendo cha mtu kupewa adhabu ya kutumikia kifungo gerezani hakina maana ya kuondoa utu wake aliopewa na Mwenyezi Mungu, kitu pekee anachotakiwa kukikosa ni uhuru wake na kuzuiliwa kwenda atakapo. Haki zake zingine zote zilizoainishwa na sheria na mikataba ya kimataifa zinaendelea kuwepo na inabidi zilindwe na kuheshimiwa kama amabavyo mtu amabaye sio mfungwa anapata.

Pamoja na kuwa anatumikia adhabu lakini kuzuiwa kwake kukosa uhuru wake unatakiwa uchukuliwe kwa njia za kistaarabu (The least intrusive and reasonable measures what would achieve the objective).

Katika jicho la sheria mfungwa si mnyama bali ni biadamu kama binadamu wengine wowote. Haki zake zote za kisheria na kikatiba ni lazima zilindwe na ziheshimiwe, utu wake usitwezwe na kudharauliwa na hatikiwi kupewa adhabu za kikakatili na za kudhalilisha utu, na wala hatakiwi kuteswa kiakili na kimwili kwani kufanya hivyo ni sawa na kumuadhibu mara mbili kwa kosa moja.

Chini ya sheria za haki za binadamu kama zilivyoainishwa hapo juu ikiwemo katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, serikali ina wajibu wa kulinda na kuheshimu haki za msingi za binadamu.

Jukumu hili linajumuisha serikali kutokuvunja haki hizo lakini pia kuchukua hatua pale ambapo haki hizo zimevunjwa na watu wengine na kuhakikisha kwamba wahanga wanapata afua mbalimbali. Kwa vile jukumu la kulinda Haki zetu za kikatiba lipo kwa mahakama chini ya Ibara 30(3) na kwa vile tuna haki na wajibu wa kulinda katiba chini ya ibara 26(2) ya katiba yetu ndio maana sisi tumeamua kupiga hodi mahakamani kutaka mahakama kutamka kwamba vitendo vinavyolalamikiwa ni kinyume na missing ya haki za binadamu na vinavunja katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuielekeza serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani na Idara ya Magereza kufanya maboresho yenye lengo la kuhakikisha kwamba haki za msingi za binadamu kwa wafungwa na mahabusu zinazingatiwa wakiwa magerezani.

Wafungwa ni kama binadamu wengine, wasishalilishwe, kutwezwa na kuteswa.
 
Ushahidi utakuwa mgumu
Sidhani kama ushahidi utakuwa mgumu kwa Msigwa na Sugu kama watakua na wanasheria wazuri. Kwasababu hoja zao wanaweza kuzithibitisha kwa kutumia;

1) Wafungwa ambao wapo mahabusu wakipitia huo unyanyasaji (Ila siwashauri kutumia wafungwa waliokwisha hukumiwa vifungo, kwasababu mwanasheria mkuu atawapiga za uso kwa kutumia "Rekodi Ya Kuwa Na Kosa La Jinai/Criminal Records" zao kuwavua nguvu ya kuwa Mashahidi Wa "kuaminika/Liable/Trustworthy Witness" mbele ya mahakama - (Theory Ya Character Assasination Of Witness hapo ndio itaingia kazini).

● Wafungwa ni wengi sana gereza la Ruanda ambao watasimama kama mashahidi. Hata Sugu anaweza kusimama kama shahidi (Hana rekodi ya kutenda kosa la jinai, rekodi yake ya jinai ilifutwa katika rufaa aliokata - As for now Sugu has a clean record).

2) Record za Mahabusu Kama Ushahidi -Zinazo elezea mienendo ya vyakula na mahitaji mengine wanayopewa wafungwa wakiwa gerezani/mahabusu.

● Hoja, mfungwa kula mlo mmoja kwa siku nzima ni unyanyasaji.

● Hoja, mfungwa kula mlo wa aina moja zaidi ya siku 3 ni unyanyasaji, kwasababu wanahitaji balanced diet pia.

3) Haki za kimwili kwa wake/waume zao ambao ni halali kisheria, ambao walio nje ya magereza.

● Hoja, kama wafungwa wanapatiwa nafasi ya kukutana nao kimwili.

4) Usafi wa magereza na vyakula vya wafungwa.

5) Mahali salama pakulala wafungwa.

● Hoja, chumba cha kulala kimoja unakuta wanalala wafungwa 50 au 100 au zaidi ni unyanyasaji.

Hoja hii ni rahisi kuthibitisha mbele ya mahakama, tena ushahidi utatolewa na mashahidi wa mshtakiwa mwenyewe (Mwanasheria Mkuu Wa Serikali Lazima atapeleka Askari Magereza Kutoa Ushahidi Wa Utetezi).

"MY TAKE" Askari Magereza atakaepelekwa kutoa ushahidi wa kuitetea Jamhuri ndio atakae zamisha jahazi la Jamhuri. Binafsi namuonea huruma sana huyo askari magereza atakaesimama kizimbani, maana atapigwa maswali mpaka achanganyikiwe. Na kama akikutana na Tundu Lissu au Jebra, ndio anaweza akapoteza fahamu juu ya kizimba - Tundu Lissu na Jebra wana maswali magumu na mabaya sana, hayakwepeki, hayajibiki, yanachanganya na juu ya yote yanamtia shahidi wazimu, kichaa na hasira = Shahidi hata apangwe vipi huko nje ya mahakama jinsi ya kujibu na kudanganya maswali, akikutana na hivo viumbe viwili lazima apoteze kumbukumbu ya alichopangwa kudanganya huko nje.

Akiulizwa swali moja tu amechoma kibanda.

1) Gereza La Ruanda lina vyumba vya kulala vingapi na wafungwa jumla wapo wangapi??? Akijibu lina vyumba 15 na wafungwa 2,000 = Ina maana wafungwa 133 kwa chumba kimoja. Huu ni unyanyasaji.

2) Wafungwa wanakula milo mingapi kwa siku??? Akijibu wanakula mlo mmoja. Anaweza akaulizwa kwa hio hao ni mbuzi au kondoo na sio binaadamu. Huu ni unyanyasaji.

NOTE THAT: Unyanyasaji kwa wafungwa sio tu kwa kupigwa au uonevu wa kutumia nguvu (Mfungwa apigwe mpaka atolewe meno ya sebuleni au atiwe ulemavu wa miguu), hapana, hata kuwanyima lishe bora kutwa mara 3 (Balance Diet) na kuwanyima haki za kukutana na wake/waume zao wa ndoa kimwili ni unyanyasaji.

Mambo mengi wanayofanyiwa wafungwa yapo kinyume na Katiba ya nchi yetu (Hasa katika Articles Za Haki Za Binaadamu, Natural Justice, Morality, Ethics n.k).

Kwa mtazamo wangu, kesi hii Msigwa na Sugu watashinda kirahisi sana, tena watashinda asubuhi na mapema.
 
Bila shaka wataitwa na Mahakama , unachotakiwa kufahamu ni kwamba hizi kesi za kikatiba hafungwi mtu kinachobadilika ni katiba na kanuni zake
Je, hilo ni hitaji la watz?

..muda na resources wanazotumia kutetea wafungwa kwanini wasiutumie kutetea wakulima, wafugaji, vijana wasio na ajira, wastaafu,..

..nadhani wangetumia muda huu kujipendekeza kwa wapiga kura.
 
..je hilo ni hitaji la watz?

..muda na resources wanazotumia kutetea wafungwa kwanini wasiutumie kutetea wakulima, wafugaji, vijana wasio na ajira, wastaafu,..

..nadhani wangetumia muda huu kujipendekeza kwa wapiga kura.
Wafungwa wa leo ni wapiga kura wa kesho
 
Back
Top Bottom