hokani
Senior Member
- Mar 26, 2013
- 102
- 77
Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amememtaka Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw Abdulrahman Kinana kutokusubiri muda wa siku 21 alizozitoa Wakili wake kumfikisha mahakamani.
Mch. Msigwa amesema kuwa yupo tayari kwenda mahakamani hata kesho.
Mbunge Msigwa amesema kuwa katika ukweli kamwe hata kuwa tayari kumwogopa mtu na siku zote atasimama katika ukweli katika kupigania maslahi ya Taifa hili.
Msigwa amesema hatua ya katibu mkuu wa CCM kukimbilia katika vyombo vya habari kutishia kumfikisha mahakamani bila yeye mhusika kupelekewa taarifa ni sawa na kumwogopa.
Akasema suala la Kinana kwenda Mahakamani ni sawa na kumtishia nyau mtu mzima.
Msigwa ameseme CHADEMA ina mawakili waliojitosheleza na hawatanyamaza kusema ukweli kwa kuogopa vitisho.
Msigwa ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wafanyabiashara ndogondogo (wamachinga) mjini Iringa katika stendi ya mabasi ya Mikoani, akiwataka wafanya biashara hao kuendelea kufanya kazi katika eneo la Mashine Tatu bila kufanya vurugu zozote.
Amesema suala lao la kunyanyasika ameshaanza kulipigania bungeni kwa Waziri mwenye dhamana, hivyo machinga wa Iringa wasikubali kamwe, kunyanyaswa.