Mchungaji Msigwa atakiwa kutoa Uthibitisho wa Madai yake Bungeni leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchungaji Msigwa atakiwa kutoa Uthibitisho wa Madai yake Bungeni leo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GHOST RYDER, Jun 17, 2011.

 1. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mmoja wa Wenyeviti wa Bunge Mh. Jenista Mhagama amemtaka Mbunge wa Iringa mjini Mh. Mchungaji Peter Msigwa kuwasilisha kwa maandishi madai yake kuwa serikali ya CCM imepiga na kuuwa watu.

  Mambo yalianzia pale Mch Msigwa aliposima kuchangia hoja ya wizara ya fedha na mambo yalikuwa kama ifuatavyo:

  Mch. Msingwa: Anahoji Utawala bora na Sheria anasema Serikali ya CCM inapiga watu inaua watu, imekuwa ikigandamiza na kukandamiza wananchi wa kutozingatia utawala wa Sheria

  Ghafla napigwa Utaratibu wa Kanuni na LUKUVI
  Utaratibu Lukuvi: Kwa utaratibuwa Kanuni za Bunge Mbunge yeyote hatakiwi kuzungumzia jambo lolote ambalo liko nje ya mjadala unaoendelea jambo ambalo Mh. Msigwa kalifanya, Nikiwa kama kiongozi wa Serikali napingana na madai ya Mh. Mbunge pia namtaka anithibitishie ni mahala gani serikali ya mapinduzi imefanya mambo haya. Atoe uthibitisho
  Jenista Mhagama: Anasema suala hilo halipo katika hoja ya Msingi ya Agenda ya Fedha na anamtaka Mh. Mchungaji Msigwa athibitishe au aondoe kauli yake
  Mh. Mchungaji Msigwa: Serikali imeua watu Arusha na Nyamongo na imepiga wanafunzi wa UDOM ambao ni majeruhi na kwa sasa wamelazwa Hospitali
  Mhagama: Unathibitisha
  Msigwa: Ndiyo
  Mhagama: Nileletee uthibitisho kwa maandishi na kama utashindwa sheria itachukua mkondo wake
  Msigwa: anaanza tena kwa kutoa ufafanuzi maandamano
  Mhagama: anasimama na kumtaka kurejea katika mjadala na vinginenvyo amwite mchangiaji mwingine
  Msingwa: anaendelea na Hoja na deni lakuwasilisha kwa maandishi madai ya kuwa serikali ya CCM imeua na kupiga watanzania

  Nani asiyejua haya yanatokea, wanakataa nini sasa, narejea katika waraka wangu kwa Wabunge wa CDM kuna jambo hapa la msingi sana linalopaswa kushughulikiwa haraka.
  Vita inaendelea katika ya Mhagama na MsigwaÂ…Kazi ipo leo
  Hatimaye Msigwa anarejea katika Hoja.
   
 2. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Lete mambo mkuu.....tunakupata vizuri sana huku...hatuna redio wala TV mkuu,
  Ni wewe tuu unayetupakulia utamu...watakoma hao maburushi wa Kihafidhina toka CHICHIEM.
  OLE WAO NGOME KONGWE ITEKWE NA WENYEWE.Watakuwa wameisha.
   
 3. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,127
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  News Alet bungeni sasa hivi mchungaji msigwa (Mbunge Chadema) anawachachafya wabunge wa ccm bungeni kuhusiana na waziri mkuu Mizengo Pinda kwenda Iringa na kutumia ndege mbili na magari 50 kwenye msafara wake! Anaambiwa athibitishe!
   
 4. J Rated

  J Rated JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  bunge limewaka kweli kweli...
   
 5. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #5
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,491
  Trophy Points: 280
  Duuh! Leo Mch. Msigwa amepewa wakati mgumu sana, tena ilikuwa kishabiki zaidi.
   
 6. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Lukuvi anaendelea kutoa ufafanuzi wa kuhusu madai kuwa magari yamewahi kusimama kwa muda wa masaa 10 na pia kuwa na msafara wa magari 52 Iringa na ndege 2 katika msafara wa Waziri Mkuu katika ziara yake Iringa ambayo anayataja kama matumizi mabaya ya Rasilimali za Umma...Hebu tazameni Bunge kama mpo karibu na TV kuna mambo hayapo sawa

  Mhagama: Anaongea kwa jazaba kali kumwelewesha Mchungaji nini cha Kufanya kwa kumtaka kuthibitisha ama kufuta kauli yake kama alivyotakiwa katika muongozo wa Mh. Lukuvi

  Mchungaji: Anathibitisha kuwa madai yake ni kweli

  Mhagama: Anamwambia Mchungaji sawa na kuwa utaratibu utafuatwa

  Anapigwa utaratibu tena kwa kusema kuwa Mbunge wa kwanza Mwanamke si Ana Makinda walikuwepo akina Bini Titi Mohamed na kwamba inaonekana mchungaji hakusoma vizuri takwimu alipokuja katika siasa awe makini asije kuwapoteza kondoo wake (Hili la nini sasa)

  Wadau tazameni mambo haya kuna kampeni nzito hapa
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Huyo bro wangu kichwa kweli
   
 8. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #8
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Time will tell
   
 9. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #9
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Uthibitisho gani anaotaka spika. Askari akiua raia kwa nini tusiseme kuwa ni serikali imeua na hasa kama hakuna hatua yoyote ya kisheria iliyochukuliwa dhidi ya muuaji!!
   
 10. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,491
  Trophy Points: 280
  • Ole sendeka: kamwambia Msigwa ashughulikiwe kwa kuifanananisha serikali na mtoto wa miaka 2, kwa misingi kwamba ni lugha ya kuudhi. Msigwa alisema serikali inakuwa kama mtoto wa miaka 10, anayefanya mambo kama mtoto wa miaka 2
  • Lukuvi: Amemtaka Msigwa athibitishe kama kweli waziri mkuu alienda Iringa na ndege 2, magari 50, kufunga barabara kuu za Iringa kwa saa 5
  • Amepewa taarifa kwamba spika wa kwanza mwanamke sio makinda
  • Ameambiwa athibitishe kama ni kweli serikali ya CCM inaua raia
  • Mch. Msigwa amekubali kuthibitisha yote hapo juu (isipokuwa taarifa)
   
 11. RUMANYIKA

  RUMANYIKA JF-Expert Member

  #11
  Jun 17, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 315
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mhagama kambania mchungaji kutoa taarifa ya kudhalalishwa. Kweli magamba wanajiendesha kwa upendeleo.
   
 12. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #12
  Jun 17, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  Duh!.. Kama kweli kazi ipo Tanzania... Magari 50!?..
   
 13. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #13
  Jun 17, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,127
  Trophy Points: 280
  Kaaaaazi kwelikweli...
   
 14. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #14
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Na jana Mnadhimu Mkuu alimuuliza waziri Mkuu katika ufafanuzi wake baada ya kupigwa muongozo katika taratibu hizi zinazoendelea sasa za kuhujumu kambi ya CDM ana alimmuliza kama kuna kesi yeyote ambayo Polisi kashitakiwa mahakami kwa kuuwa kama ipo. Hapakuwa na jibu zaidi ya kuipotezea kiaina.

  Hivi dola ni akina nani hawa polisi hawamo kumbe?????!!!!!!

  Viongozi watambue majibu yao yanawaweka pabaya 2015...Huu mtaji mzuri wa kisiasa jukwani wacha waendelee kuropoka wakisubiri makofi ya meza watakutana na makofi ya sanduku la kura 2015
   
 15. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #15
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,966
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Si atathibitisha,tabu iko wapi?Tunasubiri.
   
 16. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #16
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,491
  Trophy Points: 280
  Wakati Lukuvi anachangia akatamka maneno "Sijui huyu ni Mchungaji gani? Zamani nilidhani mchungaji ni mchungaji wa Kondoo".
  Mchungaji Msigwa ameomba alindwe na kiti (mwenyekiti), mwenyekiti akapotezea na kumwambia afuate kanuni (kuhusu utaratibu), tatizo ni kwamba hakupewa tena nafasi ya kusikilizwa kwa sababu ya muda-"tunaendelea na mchangiaji anayefuata, sitaki muongozo wala taarifa tena"

  Toka bunge limeanza, nimeona kama wapinzani hawapewi nafasi ya kutoa hoja bila kukatizwa na hawapewi nafasi ya kulalamika (kuomba mwongozo wa spika au mwenyekiti).
   
 17. The dirt paka

  The dirt paka JF-Expert Member

  #17
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni bajeti ya chama, mnataka atembee kwa miguu? Kwani ye punda wa dobi?
  Pato la vitega uchumi vya CCM KAMA CCM kirumba uwanja bora, wafanyaje? Kiongozi na raia hawawezi kuwa sawa mwachen mzee wetu atumikie taifa lake kwa nafasi yake. Mlipokodi helikopta na matumizi yenu kuzidi ruzuku!
  CHADEMA ITAKUJA LAKINI CCM ITASIMAMA DAIMA.
   
 18. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #18
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  JIBU:
  Dola ni Barrick Goldmine na SYMBIOM ......haa ha ha ha ha te ete...
  ccm bana wananifurahisha sana.
   
 19. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #19
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,491
  Trophy Points: 280
  Unajua kuna mambo ni magumu kuthibitisha, hata wao wanajua ndo maana wamemlengesha. Tatizo ni kwamba ukweli kuhusu uthibitisho unaamriwa kwa kura-ambazo CCM wanazo nyingi.
   
 20. a

  anney Senior Member

  #20
  Jun 17, 2011
  Joined: Jul 9, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mchungaji Msigwa ushahidi mwingine upo kijiji cha Kiru wilaya ya Babati, Polisi walimpiga mtuhumiwa mpaka amekufa na Bado yupo chumba cha kuhifadhia maiti baada ya mzozo wa uchunguzi. Huyu marehemu alikamatwa na polisi akiwa mahakamani, wakamchukua kwa mahojiano mahali pasipojulikana, kilichofuatia baada ya hapo ni kuonekana hospitalini akiwa mahututi na akafa baadaye kutokana na kupigwa na polisi.
   
Loading...