Mchungaji Msigwa asema: Bila kusimamia misingi (principles) vyama vinakosa uhalali wa kuwepo

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,498
51,090
Akiongea na Darmpya, mchungaji Msigwa amekosoa vikali hatua ya Maalim Seif na Zitto Kabwe kujiunga na serikali ya umoja wa kitaifa huko Zanzibar, Mchungaji Msigwa amekiita kitendo hicho kama ni flipfloping. Amesema ni kuwachanganya wananchi kutoa misimamo inayokinzana katika jambo lilelile.

Kwa mfano mwezi uliopita Mkuu wa Chama cha ACT Zitto Kabwe alitia saini tamko la pamoja akiwa na Mwenyekiti wa Chadema, na Makamu Mwenyekiti wa Chadema tamko la kutokubaliana na uchaguzi mkuu uliopita, katika tamko hilo walikubaliana pia kutotambua matunda yoyote ya uchaguzi huo, lakini kabla hata vumbi la uchaguzi halijatulia, Zitto kageuka, anatetea ACT kuingia katika serikali waliyoiita haramu hapo mwanzo.

Msigwa anavunja hoja ya Zitto anayedai kuwa kama ukimdai mtu kitu kisha akakupa kidogo basi chukua kidogo hicho kisha endelea kudai, Msigwa anasema hiyo ni hoja mfu, ni sawa na jambazi akuvamie kwa mabunduki akupore kila kitu akubakishikie kitanda kisha kwa kunyenyekea umshukuru jambazi huyo kuwa umemuona ana nia nzuri na wewe!

Pia Mchungaji Msigwa anasema kuwa walichokifanya akina maalimu ni kugawana vyeo tu na wala siyo hoja ya maendeleo, akahoji kuwa je kwani Zanzibar haiwezi kuendekea bila Maalim? Na akahoji pia je Kwa Maalim kuingia kwenye hiyo serikali kunafanikisha vipi uwepo wa tume huru ya uchaguzi na demokrasia ambayo vyama vya upinzani vimekuwa vikipigania? - Msigwa amesema, hapo ishu ni vyeo tu na wala siyo kuadvance mambo ambayo wapinzani walikuwa wakipigania kinyume cha CCM.

Unaweza kuona mahojiano zaidi hapa.

 
Zitto nimemfuta katika orodha ya watu makini na wapigania maslahi ya taifa
Hana maana.
Ni juzi tu baada ya uchaguzi, ametiliana saini ya pamoja akiwa yeye, Mbowe, Lissu, Mnyika na makamu mwenyeiti wa ACT ya makubaliano ya kutotambua uchaguzi mkuu na matunda yake.

Leo kageuka, huu ukigeugeu ni wa karne!

Asije akatudanganya kuwa ameshindwa nguvu ya kimaamuzi na kamati kuu yake, kama kweli anasimamia principle basi angejiuzulu ukuu wa chama kuonyesha kuwa hakubaliani na msimamo wa chama kuingia SUK kinyume na yeye kama mkuu wa chama alivyokwishatuaminisha hapo awali!.
 
Msigwa ameulizwa ukiteuliwa na Rais Magufuli kuwa Mbunge utakataa au utakubali? Naomba ujibu ndio au hapana.

Jamaa akashindwa kujibu ndio au hapana badala yake akaanza kuleta maneno mengi ambayo hayana jibu la ndio au hapana!

Wanasiasa wa Tanzania ni wajasiriamali tu kama wajasiriamali wengine!
 
Kwanini usiiambie ccm ilompa mkabila na mdini nchi
Nakubaliana na hoja yake lakini pia bado nasubiria Msigwa na CHADEMA kwa ujumla kuwaomba watz msamaha kwa kumpokea Lowassa na kumfanya kuwa mgombea Urais mwaka 2015. I believe this was such a huge confusion and a contradiction...
 
Zitto Kabwe alitia saini tamko la pamoja akiwa na Mwenyekiti wa Chadema, na Makamu Mwenyekiti wa Chadema tamko la kutokubaliana na uchaguzi mkuu uliopita, katika tamko hilo walikubaliana pia kutotambua matunda yoyote ya uchaguzi huo, lakini kabla hata vumbi la uchaguzi halijatulia, Zitto kageuka, anatetea ACT kuingia katika serikali waliyoiita haramu hapo mwanzo.
Ukigeugeu wa watanzania ndiyo tatizo ktk harakati za kisiasa

Nape, Kinana, na Makambas hawamtaki jiwe lkn ghafla wakageuka.

Dr. Slaa, Kitila, Katambi, Shonza Mtulia ,Waitara, Mashinji, Gekulu, Silinde, Covid 19, e.t.c hawakuipenda CCM lkn ghafla waligeuka.

Kama kila mtu angekuwa anasimamia anachokiamini CCM siku nyingi ingekuwa maktaba.
 
CDM wao hawana madhara, walikuwa wanategemea mbeleko ya ACT Zenji, waendelee kususa hadi 2025 tu , Magu haendekezi ujinga, wasuse hadi wavimbe baadae akili itarudi.
 
Msigwa anajifanya kusahau kuwa kabla ya jambo lolote kitu cha kwanza kwa mwanasiasa ni maslahi..hayo mengine yanabaki kuwa kusadikika..sijui haki, kuwajibika, demokrasia ni nyimbo zinazoimbwaga ukikosa fursa.

Pia akizungumzia demokrasia labda ye amesahau uchaguzi wa mwenyekiti kanda ya nyasa kuwa ole sosopi alikatwa na mbowe siku ya uchaguzi baada ya kuonekana tishio na kisha zikapigwa kura za ndio na hapana na yeye msigwa akakubali na kuwa mwenyekiti akijua wazi mshindani wake kakatwa kibabe..angekuwa anajua maana ya demokrasia asingekubali.
 
Akiongea na Darmpya, mchungaji Msigwa amekosoa vikali hatua ya Maalim Seif na Zitto Kabwe kujiunga na serikali ya umoja wa kitaifa huko Zanzibar, Mchungaji Msigwa amekiita kitendo hicho kama ni flipfloping. Amesema ni kuwachanganya wananchi kutoa misimamo inayokinzana katika jambo lilelile...
Zitto alipotea kwenye siasa baada ya kutoka CHADEMA kwa sasa ni busy body tu
 
Msigwa ameulizwa ukiteuliwa na Rais Magufuli kuwa Mbunge utakataa au utakubali? Naomba ujibu ndio au hapana.

Jamaa akashindwa kujibu ndio au hapana badala yake akaanza kuleta maneno mengi ambayo hayana jibu la ndio au hapana!

Wanasiasa wa Tanzania ni wajasiriamali tu kama wajasiriamali wengine!

Nje ya mada, kile chama cha upinzani ulisema kitaanzishwa na tiss baada ya kuiua cdm kinaanza lini vile?
 
Back
Top Bottom