Kuelekea 2025 Mchungaji Msigwa apendekeza kuwe na Midahalo ya Wazi hadi katika ngazi ya Kitaifa ili kupata Wagombea wa kupambana na CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,538
8,547
DEMOKRASIA: Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa amesema ili kupata Viongozi wanaoweza kukabiliana na CCM, chama hicho kinapaswa kutumia njia ya Midahalo ya Wazi kupima uwezo wa Wagombea

Msigwa ameeleza hayo wakati akizungumza na Wanahabari na kusema "Napendekeza katika ngazi ya Taifa kwa mfano kunatakiwa kuwe na Midahalo si chini ya Mitano kwenye Kanda ili watu wajue huyu Kiongozi anaweza kukabiliana na CCM?"

Amesema Wagombea hawapaswi kujificha kwenye koti la Chama wakati ili chama kiweze kushinda katika Chaguzi kinapaswa kuwa Mgombea Anayekubalika, Mwenye Agenda, Mipango na Fedha

Kauli za Msigwa zinakuja siku chache baada kutangazwa matokeo ya Uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti Kanda ya Nyasa ambapo Joseph Mbilinyi alishinda nafasi hiyo dhidi ya Msigwa.

 
Msigwa ana kisirani cha kitoto, haya mawazo yake hayana mashiko pia.
 
CCM wafanye midahalo ya wazi???
Labda Midahalo ya aina hii🫢🤭🫣😅😆👇

View: https://youtu.be/WuGKID_Uf_E?si=kCqjw9N9T-ZIQ_-9

Au Midahalo ya kupeleka Wasanii wakata viuno kwa Wananchi badala ya kuwapelekea Maendeleo.

Au Midahalo ya Kucheka Migogoro ya CHADEMA
PnruDNTWABm8qRq7I5FRJ_wRlvKooRKy7wbqjrxJqUg.jpg
 
Msigwa ana hoja nzito na ya maana! midahalo inasaidia wagombea na wapiga kura kwa pamoja

Pili, Msigwa alilalamikia msimamizi J.Mrema kabla ya kura. Lakini pia si kuna taratibu zinazoendesha uchaguzi?
Ikiwa ni hivyo, kwanini Katibu Mkuu na Mwenyekiti wa CDM hawakuona umuhimu wa kutengeneza mazingira mazuri ya kufuata taratibu na kanuni zao ili kukiweka chama chao pamoja

Hili jambo lina tatizo kubwa, kimya cha Katibu Mkuu ambaye ni mtendaji na Mwenyekiti anayepsawa kuunganisha chama chao ni tatizo. Hata kama Msigwa hana hoja lakini mazingira tu yanamjengea hoja.

CDM wanapaswa kusafisha safu yauongozi wa juu, kuna tatizo kubwa sana

JokaKuu
 
Kama kweli hayo makundi ya wajumbe (wapiga kura) anayoyataja Msigwa, hayakuruhusiwa kupiga kura Kanda ya Nyasa peke yake, basi Msigwa ana hoja
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom