Mchungaji Msigwa akiri kumsingizia Kinana ujangili, amwangukia na kumwomba radhi



Natoa tamko la kumuomba radhi Abdulrahman Kinana, ikumbukwe nilikuwa na kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania iliyofunguliwa na Kinana kutokana na matamshi niliyowahi kuyatoa kumuhusisha na ujangili. Ninakiri tuhuma hizo hazikuwa za kweli wala ushahidi wowote, bali zilikuwa na malengo potofu ya kisiasa na kizandiki.


============

FULL TEXT:

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAMKO LA KUOMBA RADHI LA MHE PETER SIMON MSIGWA (MB)

Ndugu Wanahabari,

Leo nimewaita kwa ajili ya jambo moja tu; kutoa tamko la kuomba radhi kwa ndugu yangu Abdulrahman Kinana.

Itakumbukwa kwamba nilikuwa na kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania iliyofunguliwa na ndugu Kinana dhidi yangu kwa sababu ya matamshi niliyowahi kuyatoa dhidi yake –ndani na Bunge, nikimhusisha na biashara ya ujangili na uuzaji wa nyara za serikali.

Katika hotuba yagu nikiwa Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni nikiwasilisha maoni yetu wakati wa mjadala wa makadirio ya matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya mwaka 2013/2014, nilitoa maelezo marefu ya kumhusisha ndugu Kinana na biashara hizo.

Kutokana na tuhuma zangu hizo kwake, Ndugu Kinana alinifungulia mashitaka katika Mahakama Kuu ya Tanzania kwa shauri namba 108 ya mwaka 2013. Katika kesi hiyo iliyosikiliwa na kuhukumiwa na Jaji Zainab Muruke, nilikutwa na hatia baada ya kushindwa kuthibitisha tuhuma zangu hizo mbele ya Mahakama.

Leo, nakiri mbele yenu na kupitia ninyi, mbele ya Watanzania, kwamba tuhuma hizo nilizozitoa mara kadhaa dhidi ya Kinana hazikuwa na ukweli wala ushahidi wowote. Taarifa nilizopewa na kuzitumia hazikuwa na ukweli bali zilikuwa na malengo potofu ya kisiasa na kizandiki. Nasikitika kwamba taarifa hizo nilipewa na watu waliokuwa na malengo maovu.

Mambo kama haya hutokea katika jamii na maishani. Nasi kama binadamu inapotokea kuwakosea wenzetu busara hututuma kuomba radhi na kwa waliokosewa kuwa tayari kusamehe.

Ni dhahiri kwamba kupitia kauli zangu za huko nyuma dhidi yake, nimemkosea, nimemdhalilisha na kumkashifu ndugu yangu Kinana. Nafurahi kuwaambia hapa kwamba nimekutana na kaka yangu Kinana na kumuomba radhi yeye binafsi na amekubali kunisamehe.

Nimekuja hapa hadharani kuomba radhi kwa sababu nafahamu aliyeumizwa si Kinana peke yake, bali familia yake, ndugu zake na marafiki zake.

Mtakubaliana nami kwamba Ndugu Kinana ni mzalendo, mtu muungwana na mstaarabu ambaye kwa kweli hastahili kuzushiwa, kukashifiwa wala kudhalilishwa. Ninamshukuru na kwa kweli nitaendelea kumheshimu kama alivyodhihirisha undugu, ustaarabu na uungwana wake kwangu na kwa familia yangu.

Baada ya msamaha huo wa Kinana, sasa shauri hili la kimahakama sasa litakuwa limemalizika rasmi.

Nawashukuru sana kwa kuhudhuria na kunisikiliza. Ahsanteni.



Mhe Mchungaji Peter Simon Msigwa

Mbunge, Jimbo la Iringa Mjini

Aprili 19, 2020


Dar es Salaam.

============

Pia soma:

1) HOTUBA ya Kambi ya Upinzani Bungeni, Maliasili na Utalii na Peter Msigwa (FULL TEXT)

2) Kinana kupitia Wanasheria amuandikia Msigwa kumtaka amuombe radhi

3) Mchungaji Msigwa (CHADEMA) amtaka Kinana awahi kortini

4) Kinana amburuza Msigwa kortini

5) Msigwa amuomba mzee Mtei akaongee na Kinana ili wayamalize!

6) Mahakama kuamua kesi ya Kinana leo


Ni dhahiri sasa kinana ndio rais ajaye kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, tulifanya kosa kubwa Lowassa hatukumuomba radhi kwenye ishue ya rada kwenye kampeni tulipata tabu kidogo kumsafisha lakini kwa Kinana tumewahi muda muafaka kabisa.

Karibu Kinana Tanzania inakuhitaji, ulitisha sana wakati wa JK bado alama zako zipo katika Mikoa mbali mbali "aujuae huu haujui huu"
 
Hawajaanza Leo kuwalaghai Watanzania kama walidiriki kumsingizia Rais Yu mahututi Ujerumani watashindwaje kumwambia Kinana ni Jangiri tuwapuuze haya ndio maisha yao wanachadema
 
Ni hukumu ya Kesi ya Madai (Civil case) namba 108 ya mwaka 2016.

Nimeona niiambatanishe hapa JF ili wadau ambao ni wataalam wa Sheria waichambue na kutupa mafunzo sisi wengine juu ya hatari zilizo mbele kwa kuamua kutoa tuhuma dhidi ya wengine bila ushahidi.
 

Attachments

  • High Court Judgment Civil Case 108 of 2013.pdf
    7.9 MB · Views: 1
Ni hukumu ya Kesi ya Madai (Civil case) namba 108 ya mwaka 2016.

Nimeona niiambatanishe hapa JF ili wadau ambao ni wataalam wa Sheria waichambue na kutupa mafunzo sisi wengine juu ya hatari zilizo mbele kwa kuamua kutoa tuhuma dhidi ya wengine bila ushahidi.
Mchungaji anapotenda dhambi ya " Uzushi" ni jambo ovu sana mbele zake Mungu.

Mchungaji Msigwa inabidi aende Kanisa Katoliki akafanye toba ya wazi na kuwataja waliomtuma amsingizie mzee Kinana!
 
UONGO huohuo ukaja kurudiwa na bosi wa takukuru ili kumlinda bwana mkubwa.

Mitambo ya treni ina gharama kubwa sana. Haiwezi kutengenezwa bila order maalum.

Serikali ya JK iliagiza mitambo hiyo lakini bwana mkubwa akaamua kudanganya umma ili kupata kiki ya kisiasa.

Bwana mkubwa ana tabia mbaya ya kusema UONGO.
Uzuri sio mchungaji.
 
Mchungaji anapotenda dhambi ya " Uzushi" ni jambo ovu sana mbele zake Mungu.

Mchungaji Msigwa inabidi aende Kanisa Katoliki akafanye toba ya wazi na kuwataja waliomtuma amsingizie mzee Kinana!
Lakini mchungaji Msigwa amemuomba Kinana msamaha hadharani hii ni zaidi ya kukiri kosa, sasa wewe unataka njia yako binafsi aifuate as if umekuwa msemaji wa mzee Kinana... labda unaajenda ya siri dhidi ya mch.Msigwa na chuki ya nyoka cobra

Sent using Jamii Forums mobile app
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom