Mchungaji Msigwa akiri kumsingizia Kinana ujangili, amwangukia na kumwomba radhi

Natoa tamko la kumuomba radhi Abdulrahman Kinana, ikumbukwe nilikuwa na kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania iliyofunguliwa na Kinana kutokana na matamshi niliyowahi kuyatoa kumuhusisha na ujangili. Ninakiri tuhuma hizo hazikuwa za kweli wala ushahidi wowote, bali zilikuwa na malengo potofu ya kisiasa na kizandiki.

============

FULL TEXT:

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAMKO LA KUOMBA RADHI LA MHE PETER SIMON MSIGWA (MB)

Ndugu Wanahabari,

Leo nimewaita kwa ajili ya jambo moja tu; kutoa tamko la kuomba radhi kwa ndugu yangu Abdulrahman Kinana.

Itakumbukwa kwamba nilikuwa na kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania iliyofunguliwa na ndugu Kinana dhidi yangu kwa sababu ya matamshi niliyowahi kuyatoa dhidi yake –ndani na Bunge, nikimhusisha na biashara ya ujangili na uuzaji wa nyara za serikali.

Katika hotuba yagu nikiwa Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni nikiwasilisha maoni yetu wakati wa mjadala wa makadirio ya matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya mwaka 2013/2014, nilitoa maelezo marefu ya kumhusisha ndugu Kinana na biashara hizo.

Kutokana na tuhuma zangu hizo kwake, Ndugu Kinana alinifungulia mashitaka katika Mahakama Kuu ya Tanzania kwa shauri namba 108 ya mwaka 2013. Katika kesi hiyo iliyosikiliwa na kuhukumiwa na Jaji Zainab Muruke, nilikutwa na hatia baada ya kushindwa kuthibitisha tuhuma zangu hizo mbele ya Mahakama.

Leo, nakiri mbele yenu na kupitia ninyi, mbele ya Watanzania, kwamba tuhuma hizo nilizozitoa mara kadhaa dhidi ya Kinana hazikuwa na ukweli wala ushahidi wowote. Taarifa nilizopewa na kuzitumia hazikuwa na ukweli bali zilikuwa na malengo potofu ya kisiasa na kizandiki. Nasikitika kwamba taarifa hizo nilipewa na watu waliokuwa na malengo maovu.

Mambo kama haya hutokea katika jamii na maishani. Nasi kama binadamu inapotokea kuwakosea wenzetu busara hututuma kuomba radhi na kwa waliokosewa kuwa tayari kusamehe.

Ni dhahiri kwamba kupitia kauli zangu za huko nyuma dhidi yake, nimemkosea, nimemdhalilisha na kumkashifu ndugu yangu Kinana. Nafurahi kuwaambia hapa kwamba nimekutana na kaka yangu Kinana na kumuomba radhi yeye binafsi na amekubali kunisamehe.

Nimekuja hapa hadharani kuomba radhi kwa sababu nafahamu aliyeumizwa si Kinana peke yake, bali familia yake, ndugu zake na marafiki zake.

Mtakubaliana nami kwamba Ndugu Kinana ni mzalendo, mtu muungwana na mstaarabu ambaye kwa kweli hastahili kuzushiwa, kukashifiwa wala kudhalilishwa. Ninamshukuru na kwa kweli nitaendelea kumheshimu kama alivyodhihirisha undugu, ustaarabu na uungwana wake kwangu na kwa familia yangu.

Baada ya msamaha huo wa Kinana, sasa shauri hili la kimahakama sasa litakuwa limemalizika rasmi.

Nawashukuru sana kwa kuhudhuria na kunisikiliza. Ahsanteni.

Mhe Mchungaji Peter Simon Msigwa

Mbunge, Jimbo la Iringa Mjini

Aprili 19, 2020

Dar es Salaam.

============

Pia soma:

1) HOTUBA ya Kambi ya Upinzani Bungeni, Maliasili na Utalii na Peter Msigwa (FULL TEXT)

2) Kinana kupitia Wanasheria amuandikia Msigwa kumtaka amuombe radhi

3) Mchungaji Msigwa (CHADEMA) amtaka Kinana awahi kortini

4) Kinana amburuza Msigwa kortini

5) Msigwa amuomba mzee Mtei akaongee na Kinana ili wayamalize!

6) Mahakama kuamua kesi ya Kinana leo

Umemkosea Mungu umemkosea kinana
 
Hogera sana Msigwa kwa uungwana wa kukiri makosa. Umeonesha njia sahihi ya kuponya roho na nafsi za wanaoumizwa kwa madai yasiyo na uthibitisho au ushahidi. Na wengine wafuate njia uliyotuonesha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnashabikia wazushi na waongo! Ni aibu kiongozi wa chama cha upinzani kudanganya umma! Nani atawaamini kukabidhi nchi waongo. Ningelikuwa wewe kuanzia leo ningelikaa kimya
Huwezi kuwa mimi.
 
Duh Billionaire, kwa biashara gani, clearing and forwarding company. Dry cleaning kesha funga, ndio ni mwenye uwezo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi unajua kwamba anawakilisha.kampuni.ngapi za meli?
Unajua kila meli ikitia nanga anakata kiasi gani cha consolidation fees?
Unajua kwamba kila meli.anakata kiaai gani kama service charge kwa kila B/L?
Yote hayo ni kwa USD
Acha kuangalia watu kijuu juu tu kama alivyofanya msigwa
 
Unajua ukweli ukijitokeza uongo unajificha, lakini TZ, uongo hauna aibu hadi ukweli unaona haya na kujificha.

Hilo shirika la diamond shipping wako ubia yeye na kampuni ya njee inayoitwa sharaf Shipping, yeye ni 40% kwa tanzania tuu. Kwa mwezi mzima wanaweza kupokea 10 hadi 20 kutegemea na biashara zilivyo.

Ndugu sidhani kuna ukweli kwa usemalo, tunaweza kukubaliana kuwa ni mtu mwenye uwezo na anajimuudu, analo shirika la internet broadband renting kama sikosei. Na anaweza kuwa na hisia kwenye makampuni mengi na yakamletea mapato.

Kitu muhimu kwenye uzi huu ni kuwa yeye na msigwa wamesameheana kiungwana, tuwaombee kheri na tuombe wanasiasa wetu wawe watu wakweli na kuweza kuwa huru kupigania haki za wananchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sitegemei serikali iseme ukweli ila upinzani ukizusha ni dhambi kubwa. Nampenda Mbowe ila tatizo lake ni njaa na tumbo lake lisiloshiba.

Huu ndiyo mwisho wa Chadema ingawa naona kuna mpango wa Chadema kunyanyua NCCR mageuzi kwa kutumia ukanda ingawa ni zamu ya ACT, jiandae mapema nawe kubinuka
Hilo la kuinyanyua NCCR ki-ukabila ndo tatizo jingine la kabila hili. Piga-ua wao ni lazima wamfuate wa kabila lao. Asipofanya hivyo wengine wanasema kanunuliwa. Hiyo ndo inamfanya Mbowe asifiwe kila siku hapa JF.

Ni kabila lao na siyo kwamba ni bora kama inavyooneshwa. Eti anaitwa ni mwamba, wakati kila leo ana tuhuma za kula pesa za wenzake.

Hakika iliyopo ni kwamba mtu hawezi kuwa rais kwa kuchaguliwa na kabila moja, idadi yao ikiwa haifiki hata milioni 3. Never!
 
Natoa tamko la kumuomba radhi Abdulrahman Kinana, ikumbukwe nilikuwa na kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania iliyofunguliwa na Kinana kutokana na matamshi niliyowahi kuyatoa kumuhusisha na ujangili. Ninakiri tuhuma hizo hazikuwa za kweli wala ushahidi wowote, bali zilikuwa na malengo potofu ya kisiasa na kizandiki.

============

FULL TEXT:

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAMKO LA KUOMBA RADHI LA MHE PETER SIMON MSIGWA (MB)

Ndugu Wanahabari,

Leo nimewaita kwa ajili ya jambo moja tu; kutoa tamko la kuomba radhi kwa ndugu yangu Abdulrahman Kinana.

Itakumbukwa kwamba nilikuwa na kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania iliyofunguliwa na ndugu Kinana dhidi yangu kwa sababu ya matamshi niliyowahi kuyatoa dhidi yake –ndani na Bunge, nikimhusisha na biashara ya ujangili na uuzaji wa nyara za serikali.

Katika hotuba yagu nikiwa Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni nikiwasilisha maoni yetu wakati wa mjadala wa makadirio ya matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya mwaka 2013/2014, nilitoa maelezo marefu ya kumhusisha ndugu Kinana na biashara hizo.

Kutokana na tuhuma zangu hizo kwake, Ndugu Kinana alinifungulia mashitaka katika Mahakama Kuu ya Tanzania kwa shauri namba 108 ya mwaka 2013. Katika kesi hiyo iliyosikiliwa na kuhukumiwa na Jaji Zainab Muruke, nilikutwa na hatia baada ya kushindwa kuthibitisha tuhuma zangu hizo mbele ya Mahakama.

Leo, nakiri mbele yenu na kupitia ninyi, mbele ya Watanzania, kwamba tuhuma hizo nilizozitoa mara kadhaa dhidi ya Kinana hazikuwa na ukweli wala ushahidi wowote. Taarifa nilizopewa na kuzitumia hazikuwa na ukweli bali zilikuwa na malengo potofu ya kisiasa na kizandiki. Nasikitika kwamba taarifa hizo nilipewa na watu waliokuwa na malengo maovu.

Mambo kama haya hutokea katika jamii na maishani. Nasi kama binadamu inapotokea kuwakosea wenzetu busara hututuma kuomba radhi na kwa waliokosewa kuwa tayari kusamehe.

Ni dhahiri kwamba kupitia kauli zangu za huko nyuma dhidi yake, nimemkosea, nimemdhalilisha na kumkashifu ndugu yangu Kinana. Nafurahi kuwaambia hapa kwamba nimekutana na kaka yangu Kinana na kumuomba radhi yeye binafsi na amekubali kunisamehe.

Nimekuja hapa hadharani kuomba radhi kwa sababu nafahamu aliyeumizwa si Kinana peke yake, bali familia yake, ndugu zake na marafiki zake.

Mtakubaliana nami kwamba Ndugu Kinana ni mzalendo, mtu muungwana na mstaarabu ambaye kwa kweli hastahili kuzushiwa, kukashifiwa wala kudhalilishwa. Ninamshukuru na kwa kweli nitaendelea kumheshimu kama alivyodhihirisha undugu, ustaarabu na uungwana wake kwangu na kwa familia yangu.

Baada ya msamaha huo wa Kinana, sasa shauri hili la kimahakama sasa litakuwa limemalizika rasmi.

Nawashukuru sana kwa kuhudhuria na kunisikiliza. Ahsanteni.

Mhe Mchungaji Peter Simon Msigwa

Mbunge, Jimbo la Iringa Mjini

Aprili 19, 2020

Dar es Salaam.

============

Pia soma:

1) HOTUBA ya Kambi ya Upinzani Bungeni, Maliasili na Utalii na Peter Msigwa (FULL TEXT)

2) Kinana kupitia Wanasheria amuandikia Msigwa kumtaka amuombe radhi

3) Mchungaji Msigwa (CHADEMA) amtaka Kinana awahi kortini

4) Kinana amburuza Msigwa kortini

5) Msigwa amuomba mzee Mtei akaongee na Kinana ili wayamalize!

6) Mahakama kuamua kesi ya Kinana leo

Mchungaji tapeli. Wanasaccos tuliwaeleza mapema kuwa Saccos tunaizika October 2020 sasa naona mmeanza kuona dalili za wazi.
 
Back
Top Bottom