Mchungaji Msigwa akiri kumsingizia Kinana ujangili, amwangukia na kumwomba radhi

acidplus

Member
Jun 8, 2018
82
125
Lakini mchungaji msigwa amemuomba kinana msamaha hadharani hii ni zaidi ya kukiri kosa, sasa wewe unataka njia yako binafsi aifuate as if umekuwa msemaji wa mzee kinana... labda unaajenda ya siri dhidi ya mch.msigwa na chuki ya nyoka cobra

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni Dhambi kubwa na ovu kwa Mtumishi wa MUNGU, kumshuhudia mwingine uongo.

Mchungaji wa Kondoo, rudisha vitabu vya MUNGU na mapambo mengine Kanisani na uingie kwenye siasa za maji taka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
emanuel goa

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
218
250
Ni Dhambi kubwa na ovu kwa Mtumishi wa MUNGU,kumshuhudia mwingine uongo.
Mchungaji wa Kondoo,rudisha vitabu vya MUNGU na mapambo mengine Kanisani na uingie kwenye siasa za maji taka.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kosa lingine unafanya..., daudi nabii na mfalme alifanya mpaka mauaji na bado MUNGU mwema akamsamehe sasa itakuwa mch.msigwa unajitoa ufahamu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
27,491
2,000

Natoa tamko la kumuomba radhi Abdulrahman Kinana, ikumbukwe nilikuwa na kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania iliyofunguliwa na Kinana kutokana na matamshi niliyowahi kuyatoa kumuhusisha na ujangili. Ninakiri tuhuma hizo hazikuwa za kweli wala ushahidi wowote, bali zilikuwa na malengo potofu ya kisiasa na kizandiki.

============

FULL TEXT:

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAMKO LA KUOMBA RADHI LA MHE PETER SIMON MSIGWA (MB)

Ndugu Wanahabari,

Leo nimewaita kwa ajili ya jambo moja tu; kutoa tamko la kuomba radhi kwa ndugu yangu Abdulrahman Kinana.

Itakumbukwa kwamba nilikuwa na kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania iliyofunguliwa na ndugu Kinana dhidi yangu kwa sababu ya matamshi niliyowahi kuyatoa dhidi yake –ndani na Bunge, nikimhusisha na biashara ya ujangili na uuzaji wa nyara za serikali.

Katika hotuba yagu nikiwa Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni nikiwasilisha maoni yetu wakati wa mjadala wa makadirio ya matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya mwaka 2013/2014, nilitoa maelezo marefu ya kumhusisha ndugu Kinana na biashara hizo.

Kutokana na tuhuma zangu hizo kwake, Ndugu Kinana alinifungulia mashitaka katika Mahakama Kuu ya Tanzania kwa shauri namba 108 ya mwaka 2013. Katika kesi hiyo iliyosikiliwa na kuhukumiwa na Jaji Zainab Muruke, nilikutwa na hatia baada ya kushindwa kuthibitisha tuhuma zangu hizo mbele ya Mahakama.

Leo, nakiri mbele yenu na kupitia ninyi, mbele ya Watanzania, kwamba tuhuma hizo nilizozitoa mara kadhaa dhidi ya Kinana hazikuwa na ukweli wala ushahidi wowote. Taarifa nilizopewa na kuzitumia hazikuwa na ukweli bali zilikuwa na malengo potofu ya kisiasa na kizandiki. Nasikitika kwamba taarifa hizo nilipewa na watu waliokuwa na malengo maovu.

Mambo kama haya hutokea katika jamii na maishani. Nasi kama binadamu inapotokea kuwakosea wenzetu busara hututuma kuomba radhi na kwa waliokosewa kuwa tayari kusamehe.

Ni dhahiri kwamba kupitia kauli zangu za huko nyuma dhidi yake, nimemkosea, nimemdhalilisha na kumkashifu ndugu yangu Kinana. Nafurahi kuwaambia hapa kwamba nimekutana na kaka yangu Kinana na kumuomba radhi yeye binafsi na amekubali kunisamehe.

Nimekuja hapa hadharani kuomba radhi kwa sababu nafahamu aliyeumizwa si Kinana peke yake, bali familia yake, ndugu zake na marafiki zake.

Mtakubaliana nami kwamba Ndugu Kinana ni mzalendo, mtu muungwana na mstaarabu ambaye kwa kweli hastahili kuzushiwa, kukashifiwa wala kudhalilishwa. Ninamshukuru na kwa kweli nitaendelea kumheshimu kama alivyodhihirisha undugu, ustaarabu na uungwana wake kwangu na kwa familia yangu.

Baada ya msamaha huo wa Kinana, sasa shauri hili la kimahakama sasa litakuwa limemalizika rasmi.

Nawashukuru sana kwa kuhudhuria na kunisikiliza. Ahsanteni.Mhe Mchungaji Peter Simon Msigwa

Mbunge, Jimbo la Iringa Mjini

Aprili 19, 2020

Dar es Salaam.

============

Pia soma:

1) HOTUBA ya Kambi ya Upinzani Bungeni, Maliasili na Utalii na Peter Msigwa (FULL TEXT)

2) Kinana kupitia Wanasheria amuandikia Msigwa kumtaka amuombe radhi

3) Mchungaji Msigwa (CHADEMA) amtaka Kinana awahi kortini

4) Kinana amburuza Msigwa kortini

5) Msigwa amuomba mzee Mtei akaongee na Kinana ili wayamalize!

6) Mahakama kuamua kesi ya Kinana leo

Ukiona hivi basi ujue either Msigwa atamfuata alipo Kinana,
Au Kinana atamfuata alipo Msigwa,

Time will tell....
 
The Most Winner

JF-Expert Member
Aug 6, 2018
735
1,000
Siasa na Dini ni kitu kibaya sana hasa pale usipokuwa makini ,sasa huyu ni Mchungaji anahudumia watu kiroho tena anasema uongo au nimesoma vibaya kuwa sio mchungaji?

Kazi ipo bora aeleweke tu aache siasa awe Mchungaji au Awe Mwana siasa Maisha yaendelee anawapa !mfano gani waumimi, Ndo maana nalisifia Kanisa letu Pendwa Catholic huwa halina haya mambo ya kuanzIsha makanisa bila mpangilio kazi ipo.

pujo
 
mukaruka mzee

JF-Expert Member
Jan 22, 2020
970
500

Natoa tamko la kumuomba radhi Abdulrahman Kinana, ikumbukwe nilikuwa na kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania iliyofunguliwa na Kinana kutokana na matamshi niliyowahi kuyatoa kumuhusisha na ujangili. Ninakiri tuhuma hizo hazikuwa za kweli wala ushahidi wowote, bali zilikuwa na malengo potofu ya kisiasa na kizandiki.

============

FULL TEXT:

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAMKO LA KUOMBA RADHI LA MHE PETER SIMON MSIGWA (MB)

Ndugu Wanahabari,

Leo nimewaita kwa ajili ya jambo moja tu; kutoa tamko la kuomba radhi kwa ndugu yangu Abdulrahman Kinana.

Itakumbukwa kwamba nilikuwa na kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania iliyofunguliwa na ndugu Kinana dhidi yangu kwa sababu ya matamshi niliyowahi kuyatoa dhidi yake –ndani na Bunge, nikimhusisha na biashara ya ujangili na uuzaji wa nyara za serikali.

Katika hotuba yagu nikiwa Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni nikiwasilisha maoni yetu wakati wa mjadala wa makadirio ya matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya mwaka 2013/2014, nilitoa maelezo marefu ya kumhusisha ndugu Kinana na biashara hizo.

Kutokana na tuhuma zangu hizo kwake, Ndugu Kinana alinifungulia mashitaka katika Mahakama Kuu ya Tanzania kwa shauri namba 108 ya mwaka 2013. Katika kesi hiyo iliyosikiliwa na kuhukumiwa na Jaji Zainab Muruke, nilikutwa na hatia baada ya kushindwa kuthibitisha tuhuma zangu hizo mbele ya Mahakama.

Leo, nakiri mbele yenu na kupitia ninyi, mbele ya Watanzania, kwamba tuhuma hizo nilizozitoa mara kadhaa dhidi ya Kinana hazikuwa na ukweli wala ushahidi wowote. Taarifa nilizopewa na kuzitumia hazikuwa na ukweli bali zilikuwa na malengo potofu ya kisiasa na kizandiki. Nasikitika kwamba taarifa hizo nilipewa na watu waliokuwa na malengo maovu.

Mambo kama haya hutokea katika jamii na maishani. Nasi kama binadamu inapotokea kuwakosea wenzetu busara hututuma kuomba radhi na kwa waliokosewa kuwa tayari kusamehe.

Ni dhahiri kwamba kupitia kauli zangu za huko nyuma dhidi yake, nimemkosea, nimemdhalilisha na kumkashifu ndugu yangu Kinana. Nafurahi kuwaambia hapa kwamba nimekutana na kaka yangu Kinana na kumuomba radhi yeye binafsi na amekubali kunisamehe.

Nimekuja hapa hadharani kuomba radhi kwa sababu nafahamu aliyeumizwa si Kinana peke yake, bali familia yake, ndugu zake na marafiki zake.

Mtakubaliana nami kwamba Ndugu Kinana ni mzalendo, mtu muungwana na mstaarabu ambaye kwa kweli hastahili kuzushiwa, kukashifiwa wala kudhalilishwa. Ninamshukuru na kwa kweli nitaendelea kumheshimu kama alivyodhihirisha undugu, ustaarabu na uungwana wake kwangu na kwa familia yangu.

Baada ya msamaha huo wa Kinana, sasa shauri hili la kimahakama sasa litakuwa limemalizika rasmi.

Nawashukuru sana kwa kuhudhuria na kunisikiliza. Ahsanteni.Mhe Mchungaji Peter Simon Msigwa

Mbunge, Jimbo la Iringa Mjini

Aprili 19, 2020

Dar es Salaam.

============

Pia soma:

1) HOTUBA ya Kambi ya Upinzani Bungeni, Maliasili na Utalii na Peter Msigwa (FULL TEXT)

2) Kinana kupitia Wanasheria amuandikia Msigwa kumtaka amuombe radhi

3) Mchungaji Msigwa (CHADEMA) amtaka Kinana awahi kortini

4) Kinana amburuza Msigwa kortini

5) Msigwa amuomba mzee Mtei akaongee na Kinana ili wayamalize!

6) Mahakama kuamua kesi ya Kinana leo

Kumbe wewe ni muongo, msingiziaji, mzushi na mbabaishaji. Hii ni kwa UKIRI NA KUKIRI kwako mwenyewe. Muombe radhi "mungu" wako aliyekupa huo "uchungaji".
 
Gagnija

JF-Expert Member
Apr 28, 2006
9,467
2,000
huyu mchungaji kweli mzandiki. anadai anaomba radhi kwa kashifa alizotoa bungeni wakati alishtakiwa kwa kashfa alizotoa mbugani mwanza.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom