Mchungaji Mastai: Maendeleo ya taifa letu yameletwa na Dkt. Magufuli kama " individual" siyo chama, CCM ilikuwepo miaka yote!

Magufuri yupo na tunamuhitaji,best current president of Africa.kwangu moja wapo ya njia ya kumpima kiongozi hasa katika nchi za Africa, ni kuangalia mahusino yake na nchi za magharibi kama ni uhusiano wa njaa na chakula huyo raisi hatufai.
 
Mchungaji Matsai wa Kanisa la KKKT Kimara amewakemea wote wenye nia ovu dhidi ya Rais Magufuli na amesema Rais hatapatwa na baya lolote na wale waovu wote watasubiri sana.

Mchungaji Matsai amesema vyombo vya habari vya Kenya vimekuwa mstari wa mbele kutoa taarifa potofu wakiwatumia vibaraka wao walio nje ya Tanzania.

Matsai amesema Rais Magufuli ameliletea taifa hili maendeleo makubwa yeye kama yeye " as an individual" na wala siyo chama kwani CCM iko miaka mingi na fedha walikuwa nazo lakini hatukuwahi kuona lolote.

Kwa maana hiyo lazima mafisadi na manyang'au watamjengea chuki.

Mchungaji Matsai ameongoza maombi mafupi ya kuyakataa na kuyafuta maneno mabaya aliyonenewa Rais Magufuli na watu wenye nia ovu, ni katika jina la Yesu amina.

Nawatakia kwaresma yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
Endelea kutetea ulaji wa sadaka bwana mchungaji. Maendeleo siyo vitu bali usitawi wa watu wakiwemo na kondoo wako.
 
KKKT Dayosisi yw Mashariki na Pwani shakuwa kichaka cha wachumia tumbo...huu si ushabiki kwa JPM Bali ni upuuzi kwa Taasisi Kama KKKT kuwa na mropokaji kama huyu !
Hivi haelewi maana ya Maendeleo!
 
Chama Cha Mazezeta. Haiwezekani uwepo na maendeleo yasiwepo, only if uko timamu, uwepo wako na maendeleo yako lazima vishabihiane.

Nina sababu million mia tisa za kuichukia CCM
Chama cha wahuni kinazusha tu mitandaoni
 
Hii ni si mara ya kwanza Mch Mastai anajiingiza katika siasa nyepesi na kulichafua Kanisa.

Nakumbuka kipindi cha kuitimisha kampeni za 2020 alijiingiza tena kwa kuongolea habari maendeleo ya watu against maendeleo ya vitu.

Mch anatakiwa kuitumia madhabau ya Bwana sawa sawa na kiapo chake.Mch anatakiwa kuhubiri habari ya Kristo na si vinginevyo.KKKT ni Kanisa ambalo msingi wa wake ni kuhubiri INJILI ya Kristo.

Bahati mbaya sana sijawahi kumsikia Mch huyu akikemea uvunjifu wa katiba,uonevu hata Lissu alipotwanga risasi alinyamaza kimya ni bora akanyamza kimya hata kipindi hiki kwababu ajira yake KKKT si kwa hisani ya chama chochote cha siasa au serekali.

Asiliingize kanisa katika mambo hovyo hovyo ambayo kwa namna yoyote halihusiki nayo.Ikiwa anataka au anapenda siasa milango ipo wazi hatuachie Kanisa letu salama.
Hilo ni angalizo kwa Mch Mastai, sikiliza sauti ziliazo nyikani!
 
Kama Magufuli alikuwa busy ofisini kwa wiki mbili, nadhani leo Jumapili ni muda mzuri kwake kutoka na kwenda Church kumuabudu Mungu wake

Hana haja ya kuhutubia Umma au kusema chochote ila tu aonekane. Huu uvumi kwamba ameshavuta ni hatari sana kwa usalama wa Nchi na ni lazima sasa atoke nje na watu wamuone

Kama TISS walilazimika kumtoa nje Waziri wa Fedha tu ili aongee na Media wakati alikuwa bado hajapona, kwa nini Rais na yeye asitoke?

Otherwise hizi rumors zitazidi kushika kasi na kuleta taharuki kwa jamii
Dah,umenikumbusha mzee wa watu philip mpango alivokuwa anaongea kwa tabu sana yote hayo kutuprove wrong!jamani jamani
 
Hii ni si mara ya kwanza Mch Mastai anajiingiza katika siasa nyepesi na kulichafua Kanisa.

Nakumbuka kipindi cha kuitimisha kampeni za 2020 alijiingiza tena kwa kuongolea habari maendeleo ya watu against maendeleo ya vitu.

Mch anatakiwa kuitumia madhabau ya Bwana sawa sawa na kiapo chake.Mch anatakiwa kuhubiri habari ya Kristo na si vinginevyo.KKKT ni Kanisa ambalo msingi wa wake ni kuhubiri INJILI ya Kristo.

Bahati mbaya sana sijawahi kumsikia Mch huyu akikemea uvunjifu wa katiba,uonevu hata Lissu alipotwanga risasi alinyamaza kimya ni bora akanyamza kimya hata kipindi hiki kwababu ajira yake KKKT si kwa hisani ya chama chochote cha siasa au serekali.

Asiliingize kanisa katika mambo hovyo hovyo ambayo kwa namna yoyote halihusiki nayo.Ikiwa anataka au anapenda siasa milango ipo wazi hatuachie Kanisa letu salama.
Huyo ni kada mtiifu wa mbogamboga,hana tofauti na yule shehe wa Mkoa wa Dar es salaam.
 
Amewakemea pia wenye nia ovu waliomshambulia Lissu kwa risasi

Back
Top Bottom