Mchungaji Lwakatare azuia hekalu lake kortini

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
19,629
34,172

MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Ardhi imezuia nyumba anayoishi Mchungaji wa Kanisa la Assemblies of God Mikocheni, Dk. Getrude Lwakatare kubomolewa.

Uamuzi huo wa mahakama ulitolewa juzi na Jaji John Mgeta, baada ya Wakili wa Lwakatare, Emmanuel Muga kuwasilisha maombi ya kupinga ubomoaji huo chini ya hati ya dharura.

Jaji Mgeta alizuia ubomoaji wa jengo hilo ama kuchukua hatua yoyote kuhusu jengo hilo lililopo Kawe Beach.

Muga aliwasilisha maombi akimwakilisha mdai ambaye ni mtoto wa Mchungaji Lwakatare, Robert Brighton dhidi ya wadaiwa NEMC, Manispaa ya Kinondoni na wadau wengine wote.

“Mheshimiwa jaji, nawasilisha maombi ya zuio la kubomoa nyumba ya mteja wangu chini ya kifungu namba 95 cha Sheria ya Mwenendo wa Madai na kifungu namba 2(3) cha JALA vinavyotoa mamlaka kwa mahakama kutoa nafuu stahili pale kunapokuwa na ukiukwaji wa kuvunja haki ya wazi,” alidai.

Akitoa uamuzi huo alisema tayari pande husika zilikuwa na kesi namba 70 ya mwaka 2012 na ikamalizika kwa kutoa hukumu na kukazia hukumu iliyompa haki ya ushindi mdai.

“Mahakama ilimpa haki mdai, lakini chakushangaza mdaiwa anakiuka matakwa ya hukumu na kutaka kubomoa nyumba, kwa hali isiyokuwa ya kawaida mdai anahitaji ulinzi wa mahakama hii ya haki,”alisema Jaji Mgeta.

Alisema nyumba hiyo ipo katika kiwanja namba 2019 na 2020 ambapo hati yake ilitolewa mwaka 1979.

Inadaiwa mwaka 2011 NEMC ilitoa notisi ya kuvunja nyumba hiyo baada ya kushinikizwa na wakazi wa eneo hilo wakidai ujenzi wake unaziba Mto Ndumbwi na uko jirani na mikoko.

Wakili Muga aliwasilisha maombi ya kuzuia nyumba ya mteja wake kubomolewa baada ya Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia wakala wa misitu Tanzania (TFS ), kuweka alama ya X wakidai imo katika hifadhi ya bahari.
 
Attachments

  • 10372594_628609260613838_1819447281616401235_n.jpg
    10372594_628609260613838_1819447281616401235_n.jpg
    59 KB · Views: 74
Hiyo nyumba nahisi imejengwa kwa kuvunja sheria, ila kwa sababu mhusika ni anauwezo anajaribu kucheza na muda tu.

Kama imevunja sheria ya uhifadhi mazingira ibomolewe tu, sheria ni msumeno.
 
Watu wazito hao jamani wanalipa kodi nyingi kwa serikali ni vigumu kuwagusa tena hao sio makosa makubwa ni mambo ya mitas tu kutoka usawa wa bahari athari ni katika uzio tu na sio nyumba nzima
 
Mwenye uelewa please; hivi sharia hi ya mazingira ambayo inapelekea kuvunja nyumba za watu ilitungwa lini? Naomba kujua tafadhari.
 
Maskini ya Mungu, hapa duniani ukikosa hela, hata kuku watakuzidi ufahari.

Ukiwa na pesa utaishia kushinda hata ukiua mtu. Kwa hiyo hawa wenzangu na mimi walibomolewa kwa kukosa pesa ya kuwapa mawakili.

Huyu mama amekuwa na Maguvu kuliko Lukuvi. Jamani mawakili wamsaidie na WASTARA.
 
Hiyo nyumba nahisi imejengwa kwa kuvunja sheria, ila kwa sababu mhusika ni anauwezo anajaribu kucheza na muda tu.

Kama imevunja sheria ya uhifadhi mazingira ibomolewe tu, sheria ni msumeno.
Sitetei kuvunja sheria, ebu fikiria hati ya kiwanja imetolewa mwaka 1979 wengi humu walikuwa hawazaliwa. Sasa leo hii nyumba iko kinyume cha sheria? hata waliotoa hiyo hati huenda wote walishafariki na kama watu wameongezeka ndo wakaona inaziba mto basi ni jukumu la serikali kujenga mfereji mbadala na siyo kuumiza watu.
 
Sakata la hiyo nyumba tangu 2012 na hapo layman ataona anapendelewa,maana kuna nyumba zina kesi mahakaman na zimevunjwa:(
 
Sitetei kuvunja sheria, ebu fikiria hati ya kiwanja imetolewa mwaka 1979 wengi humu walikuwa hawazaliwa. Sasa leo hii nyumba iko kinyume cha sheria? hata waliotoa hiyo hati huenda wote walishafariki na kama watu wameongezeka ndo wakaona inaziba mto basi ni jukumu la serikali kujenga mfereji mbadala na siyo kuumiza watu.
Hakuna sheria inayovunja sheria nyingine.

Hapo anatakiwa alipwe fidia kama anamiliki kihalali kisha wabomoe kwa mujibu wa sheria ya mazingira.

Ni kama hifadhi ya barabara, barabara ikikukuta unalipwa na kubomolewa na sio barabara ikukwepe.
 
  • Thanks
Reactions: GSL
Hawa wameshindwa kwenda mahakaman,huenda hawana uwezo
 
Attachments

  • IMG_20160107_151102.JPG
    IMG_20160107_151102.JPG
    62.5 KB · Views: 58
Huyo jaji mwenyewe aliyetoa hayo maamuzi anasali kanisa la lwakatare..... ajabu sana
 
Sitetei kuvunja sheria, ebu fikiria hati ya kiwanja imetolewa mwaka 1979 wengi humu walikuwa hawazaliwa. Sasa leo hii nyumba iko kinyume cha sheria? hata waliotoa hiyo hati huenda wote walishafariki na kama watu wameongezeka ndo wakaona inaziba mto basi ni jukumu la serikali kujenga mfereji mbadala na siyo kuumiza watu.

Mkuu, hizo ndo zile hati alizozisema MAGU siku ile anaongea na wafanyabiashara Ikulu , hati za kuchovya kwenye maji ya majani ya chai! Mwaka 1979 eneo hilo lilikuwa limejaa mikoko acha sanaa hapa!
 
Hiyo nyumba lazima ipigwe nyundo tu. Ingekuwa utawala wa Kikwete tungesema sawa mahakama imeshinda...Lakini sio sasa. Yote itasambaratishwa hiyo. Hapa Kazi Tu.
 
Sitetei kuvunja sheria, ebu fikiria hati ya kiwanja imetolewa mwaka 1979 wengi humu walikuwa hawazaliwa. Sasa leo hii nyumba iko kinyume cha sheria? hata waliotoa hiyo hati huenda wote walishafariki na kama watu wameongezeka ndo wakaona inaziba mto basi ni jukumu la serikali kujenga mfereji mbadala na siyo kuumiza watu.
Na wewe kwa akili zako timamu unaamini hiyo Hati ya kiwanja imetolewa mwaka 1979!!???? Kama haujui unachozungumzia pita tu sio lazima uandike. Kaulize wenyeji wa eneo husika ndio utaujua ukweli wa hivyo viwanja.
 
Back
Top Bottom